Sauli ni mfano wa wamiliki wa mabasi waliofilisiwa na madereva fake

Sauli ni mfano wa wamiliki wa mabasi waliofilisiwa na madereva fake

Biashara ya mabasi ya abiria kwa Dunia ya leo si ya kushadadia ma mbio yasiyo na tija bali ni akili yenye wingi wa ubunifu ndaniye kwa mambo yatakayomvutia abiria taraji.

Mfano Sauli ni wazi alifilisiwa na madereva wake kwa kushadadia sifa za kijinga za mwendo kasi hali iliyosababisha mabasi mengi kuharibika na kwayo kutumia gharama kubwa kwenye matengenezo na mwisho kushindwa kujiendesha na wadai wakafilisi vyao.

Mwisho wa siku Sauli imebaki simulizi.

NB: Kisbo ana bahati ya kung'amua mapema kurejea kwenye ustaarabu vinginevyo naye ingeshabaki simulizi.
Nomeona Katalama pia madereva wanayaendesha rough sana sijui kama yatadumu
 
Unit za yiutong bado asingetoboa, for the record sauli kama alivyo katarama mwanza wanakua tofauti na wapinzani wao kwa sababu wanatumia unit za scania,
Yuotong haiwezi pambana na zhongtong ambazo tayari wapinzani wake wakuu, newforce na Achimwene wanatumia. Angefeli mapema kweupe.
Nini kinafanya yutong ishindwe kupambana na zhongtong mkuu?
 
Biashara ya mabus walifaulu Scandinavia pekee, na ndio walioleta mapinduzi makubwa sana kwenye sekta ya usafirishaji wa abiria kwa njia ya mabasi hapa Tanzania
 
Mtanzania gani utampa investment ya mamilioni akakutafutie pesa kama wanavyoita wao?

Ukweli mchungu hakuna mwenye bus au Lori atatoboa.

Hata latra hilo wanajua.

Wote unaowaona ni just a matter of time.
Mbna kina Kilimanjaro express,happy nation,machame investment,tilisho,dar express,osaka,lim safari,ibra line,marangu coach,arusha exp, Kandahar nk wapo toka kitambo
 
Mbna kina Kilimanjaro express,happy nation,machame investment,tilisho,dar express,osaka,lim safari,ibra line,marangu coach,arusha exp, Kandahar nk wapo toka kitambo

Wanaganga njaa tu hao.

Mswahilu hapewi jukumu la kuleta mapato.

Mtegemee kuongeza michepuko tu.

Wako wapi Hood, Scandinavia, Mombasa Raha, akamba, city boy, sumry, lushanga, nk?

Wabunge usiweke kwenye list hapo tafadhali.

Rule of the thumb, nunua bus unufaishe konda, dereva, mpiga debe, fundi, polisi na latra.

Wenye mabasi na malori ni wenye kustahili pole!
 
Biashara ya mabus walifaulu Scandinavia pekee, na ndio walioleta mapinduzi makubwa sana kwenye sekta ya usafirishaji wa abiria kwa njia ya mabasi hapa Tanzania
Nadhani Abood ndio the GOAT wa mabasi yote nchini,miaka takribani 40,ascandinavia kavuma maika michache sana haizidi 20
 
Wanaganga njaa tu hao.

Mswahilu hapewi jukumu la kuleta mapato.

Mtegemee kuongeza michepuko tu.

Wako wapi Hood, Scandinavia, Mombasa Raha, akamba, city boy, sumry, lushanga, nk?

Wabunge usiweke kwenye list hapo tafadhali.

Rule of the thumb, nunua bus unufaishe konda, dereva, mpiga debe, fundi, polisi na latra.

Wenye mabasi na malori ni wenye kustahili pole!
Naona afadhali ya Malori
 
Kuna tajiri nilikuwa na ukaribu nae mwaka 2016 alipewa business plan ya kuwekeza kwenye magari(eicher) za town trip. akawekeza gari takribani 60 zikanunuliwa akajenga na Yard.

Leo hana hata Eicher moja inayotembea barabarani yote yanaliwa na kutu yard. picha ilianza na msimamizi mkuu anaomba hela ya tyre ananunua used week 2 nyingi tyre hamna mara spare zinabadilishwa toka huku zinafungwa kule hela inanunua used spare za bei rahisi.Madereva nao pasua kichwa, gari moja baada ya nyingine zikaanza kukaa hazitoki mpaka zote zikatimia hazitoki na mradi ukafa.
 
Biashara ya mabasi ya abiria kwa Dunia ya leo si ya kushadadia ma mbio yasiyo na tija bali ni akili yenye wingi wa ubunifu ndaniye kwa mambo yatakayomvutia abiria taraji.

Mfano Sauli ni wazi alifilisiwa na madereva wake kwa kushadadia sifa za kijinga za mwendo kasi hali iliyosababisha mabasi mengi kuharibika na kwayo kutumia gharama kubwa kwenye matengenezo na mwisho kushindwa kujiendesha na wadai wakafilisi vyao.

Mwisho wa siku Sauli imebaki simulizi.

NB: Kisbo ana bahati ya kung'amua mapema kurejea kwenye ustaarabu vinginevyo naye ingeshabaki simulizi.
Hiyo pekee haiwezi kuwa sababu, biashara kubwa kama ina kanuni zake za kiuweledi kuzingatia kusema tu mwendo mkali ndio imeua biashara sio kweli, mbona wengine kama Allys ,katarama n.k wanaendelea vizr tu' au unawatabiriaje?
 
Back
Top Bottom