John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Niseme ukweli tu Rais wangu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jemedari mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama tangu aingie madarakani ile hotuba ya jana ndio hotuba bora zaidi kupata kuitoa ikizidi ile ya siku ya kuapishwa kwake.
Amenifurahisha kwa kuudhirishia umma kuwa nchi ina raisi mmoja tu naye ni kutoka chama tawala na amiri jeshi mkuu ni mmoja tu Mama samia Suluhu Hassani.
Sasa kama wengi wao waliokuwa wana mjaribu kwa kujua mama akishindwa na watoto wake viburi hubaki kwa kusema subirini baba yenu arudi nitawasemea.
Jueni yeye hana huo udhaifu na anajia kila kitu nasema hivi hata yale matembezi ya mshikamano mliyoachiwa muda wowote jemedari anaweza yafuta ,
tena tabia zao za kuita press kila baada ya hotuba ya amiri jeshi mkuu ikomeshwe mara moja.
Walijua ni mwanamke wa mchezo mchezo tu JPM hakukosea kumchagua,
Hongera mama kwa hotuba bora kabisa ya kufungia mwaka na ya kufungilia uchaguzi wa serikali z mitaa.
Hata Hayati Magufuli amefurahi kwa kusikia nchi ipo kwenye mikono salama.
N.B: Wale mabaria wa kanada na ubeligiji kama hamna shughuli hapa nyumbani haya fungasheni mwende nchi inayo kiongozi hamtowachwa kama mpo juu ya sheria!
Nafikiri Rais awe mwangalifu sana katika kuchagua maneno au lugha ya kuongea mbele za hadhara za Watu, asiwe anaamini kila kitu anachoambiwa na wale Watu wanaomzunguka. Sometimes anadanganywa au amekuwa akiambiwa Habari ambazo zimetiwa chumvi Sana. Awe anachuja maneno ya kuongea hadharani.
Rais asipende kuanzisha malumbano na Mabalozi wa nchi za nje waliopo hapa Tanzania. Azingatie Sana Mikataba ya kimataifa, hususani Vienna Convention 1961.
Aidha, asipende kuanzisha au kuhamasisha uadui wa kisiasa hapa nchini.