Sawa tumefika mbinguni. Je! tutakuwa tunaongea lugha Gani?

Sawa tumefika mbinguni. Je! tutakuwa tunaongea lugha Gani?

Swali la kipuuzi maana jibu lake umeshaliandika... Hapo kwenye huo mstari uliouandika umesema mwenyewe walikuwa wanazungumza lugha moja halafu Mungu akawabadili usemi wao basi ni yeye mwenyewe Mungu ndiye atakayerejesha ule usemi wa awali.
 
ni kama ukienda china kule ndani ndani kabisaa vijijini, hawajui lugha nyingine zaidi ya kichina. ukiskia kiu na njaa ya haki lazima utajua tu namna ya kuwasilina nao ili upate maji na chakula, na matokeo yake utajikuta ni sehemu ya jamii ile 🐒
Njaa kitu kingine mkuu ooooh ooooh sema huko kaburini show yake ni too heavy ujue yaan
 
Kama akili zako kweli ziko sawa,swali la kwanza lilitakiwa liwe utapanda bus gani kuelekea mbinguni,au itakuwa bajaji,train au boat kama za azam may be!!!

Umerukia swali section B,wakati majibu ya section A yanahitajika huko,pata majibu ya A kwanza😄
🤣🤣🤣🤣🏃🏃🏃
 
Lugha ni moja tuu kiarabu..
Alafu wote tutakua katika umri mmoja yaani vijana mashabab...

Hakutokua na mtoto..
Kila mwanaume utapewa wadada mia ambao hao utawatumia kadri utakavyo tena Mungu mwingi wa rehma atakupa na nguvu za kuwakanda hao warembo.

Mkuu ni hatare sana unaambiwa
Mtakuja kutufanya tusilimu ohooo! 😁
 
Wakuu Bwana ni mwema!!

Maandiko yanatuambia ya kuwa👇👇Mwanzo 11:1-7 (KJV) Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.
Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.
Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.
Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.
Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.
Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.
Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.

Vilevile yanatuambia baada ya taabu zetu hapa duniani basi tutaenda mbinguni Kwa Mungu wetu.

Huko mbinguni nikustarehe na kula Bata tu Hadi basi

Swali ambalo Huwa najiuliza Kila mara NI SAWA TUMEFIKA MBINGUNI JE TUTATUMIA LUGHA GANI?

imagine hii Dunia Ina lugha nyingi mno huenda ni maelefu ya lugha je TUTATUMIA LUGHA ipi kuwasiliana au tutatengwa?

Mfano sisi waswahili tunakuwa na kamkoa ketu. Vivyo hivyo na wakenya,Japan, USA,nk?

Kwa upande wa wenzetu mi naona lugha Yao ni Moja tu yaani kiaarabu pekee je sisi ambao Hadi Kuna bible zenye lugha ya kichagana kisukuma itakuaje?

Karibuni.
Kama hapa duniani tu mmeshindwa kujifunza lugha tukufu ya kizaramo. Ndio mtaweza lugha za motoni na mbinguni ?
 
Back
Top Bottom