Scars haaamini kwenye uwepo wa Mungu lakini anaomba dua na kufanya maombi

Jambo ambalo nauhakika nalo ni Simba kushinda 3-0 dhidi ya Kagera sugar

Kuna chansi katika hilo ya matokeo kubadilika kuja tofauti?
Hapo haujajibu nilichouliza, kwa huo mfano unanibakiza na maswali kwamba uhakika unapatikana kwa mambo ambayo yamepita tu kama hiyo mechi ya simba na kagera au vp?
 
Hana msimamo, au labda anasimamia msimamo wa Mtu mwingine, sio wake
 
Wakana Mungu wengi ni kama vile walikuwa wanaruka dimwi la maji(dini) na kujikuta wanatua kwenye shimo(kukana uwepo wa Mungu). Hoja zao nyingi ni level ya dini tu kwamba unakuta kuna mambo hakuyaelewa kwenye dini yake na kujikuta wameangukia kuwa wakana Mungu.
 
Hapo haujajibu nilichouliza, kwa huo mfano unanibakiza na maswali kwamba uhakika unapatikana kwa mambo ambayo yamepita tu kama hiyo mechi ya simba na kagera au vp?
Kwani unawezaje kuwa na uhakika kwa mambo ambayo yapo mbeleni?
 
Hana msimamo, au labda anasimamia msimamo wa Mtu mwingine, sio wake
Msimamo ni nini?

Kwamba mimi kwasababu ni Atheist unanitazamia kutoniona kanisani kwenye event yeyote?

Nikienda kanisani kuaga mwili wa ndugu yangu hapo nakuwa sina misimamo?

Nikipewa mualiko wa harusi na rafiki yangu napaswa nikatae kwasababu siamini Mungu hivyo sipaswi kwenda kanisani?
 
Scars
Ni nini kilikuongoza kuhoji au kukataa wazo la uwepo wa Mungu?

Mawazo yako ni yapi juu ya mchango/ kazi ya dini katika jamii?

Ikiwa ungeweza kubuni dini yako au mfumo wa imani, ungekuwaje ?
 
Mchango wa dini kwenye jamii tunauona sana

Juzi tumepokea taarifa kutoka mahakama kuu ya Arusha kuhusu hukumu ya Masheikh waliorusha mabomu kanisani.

Mchango wa dini katika jamii umekuja kunufaisha kundi dogo la watu huku kundi kubwa likizidi kuangamia.

Kumuona Mzee wa Upako ni 10,000. Kukufanyia maombi maalumu hapo mtakaa chini mfanye makubaliano ya bei.

Kuna yule Kuhani Mussa wa Mbezi, saizi anajenga ghorofa lingine na limefikia hatua za mwishoni kabisa.

Ya Pastor Mackenzie sijui yalivyoishia ila nadhani yupo nyuma ya nondo.

Lakini hilo sio la kustaajabisha, la kustaajabisha ni wale waumini waliookolewa wakiwa katika hali ya udhoofu baada ya wenzao wengi kufariki naskia walienda kumtetea mahakamani Pastor Mackenzie.
 
Basi usichanganye maana unatumia sifa za Mungu kutaka kuzitumia kudai hakuna Mungu,
Huwezi kutenganisha sifa za Mungu na uwepo wa Mungu.

Vyote hivi huenda pamoja.
kama unataka kujadili hakuna Mungu basi usichanganye na habari za upendo na wema wa Mungu humo humo.
Hakuna ulazima huo.

Dhana ya uwepo wa Mungu mwema, mwenye upendo na huruma Kwenye Dunia iliyojaa uovu ukatili na ubaya Automatically Mungu huyo Hayupo.

Otherwise Mungu huyo ni Mkatili na muovu sana.
 
Jambo ambalo nauhakika nalo ni Simba kushinda 3-0 dhidi ya Kagera sugar

Kuna chansi katika hilo ya matokeo kubadilika kuja tofauti?
Aisee unajichanganya sana mjomba, hauna uhakika na kile unachosimamia, hebu kaa chini jiulize vizuri; ni kweli hauamini uwepo wa Mungu?

Pointi zako nyingi unazotumia kutetea hoja zako hazina mashiko, zinaelea sana, ndio maana unaficha udhaifu wa hoja zako kwa majibu yako marefu kwenye maswali mafupi unayoulizwa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
We ulishawahi kukaa chini na kujiuliza ni kweli hauamini Thor?
 
Kwahiyo uhakika ni kwa mambo ambayo yameshapita na si wakati ujao au hivi sasa?
Mechi inayoendelea saizi unaweza kuwa na uhakika na matokeo ya mwisho?

Bila shaka utakuwa na uhakika na matokeo ya wakati huo wakati wa mechi ikiwa bado inaendelea.

Kwa hiyo hapo sasa mtu akikuuliza nipe maoni yako ya matokeo ya mwisho kwenye mechi hii inayoendelea, majibu yako yatakuwa ni uhakika?
 
Mchango wa dini kwenye jamii tunauona sana

Juzi tumepokea taarifa kutoka mahakama kuu ya Arusha kuhusu hukumu ya Masheikh waliorusha mabomu kanisani.

Mchango wa dini katika jamii umekuja kunufaisha kundi dogo la watu huku kundi kubwa likizidi kuangamia.

Kumuona Mzee wa Upako ni 10,000. Kukufanyia maombi maalumu hapo mtakaa chini mfanye makubaliano ya bei.

Kuna yule Kuhani Mussa wa Mbezi, saizi anajenga ghorofa lingine na limefikia hatua za mwishoni kabisa.

Ya Pastor Mackenzie sijui yakivyoishia ila nadhani yupo nyuma ya nondo. Hilo sio la kustaajabisha, la kustaajabisha ni wale wamumini waliookolewa wakiwa katika hali ya udhoofu naskia walienda kumtetea mahakamani Pastor Mackenzie.
Mchango wa atheism ni upi kwenye jamii?
 
Mechi inayoendelea saizi unaweza kuwa na uhakika na matokeo ya mwisho?

Bila shaka utakuwa na uhakika na matokeo ya wakati huo wakati wa mechi ikiwa bado inaendelea.

Kwa hiyo hapo sasa mtu akikuuliza nipe maoni yako ya matokeo ya mwisho kwenye mechi hii inayoendelea, majibu yako yatakuwa ni uhakika?
Chukulia mfamo wa mechi ambapo timu A inaongoza goli 5 na timu B ina goli 1, imebaki sekunde 30 mpira uishe kutoka kwenye dakika 2 za nyongeza. Je hapo siwezi kuwa na uhakika wa matokeo ya timu A kuwa ndio mshindi wa hiyo mechi inayoendelea?
 
Huwezi kutenganisha sifa za Mungu na uwepo wa Mungu.

Vyote hivi huenda pamoja.

Hakuna ulazima huo.

Dhana ya uwepo wa Mungu mwema, mwenye upendo na huruma Kwenye Dunia iliyojaa uovu ukatili na ubaya Automatically Mungu huyo Hayupo.

Otherwise Mungu huyo ni Mkatili na muovu sana.
Kwahiyo mtu akikwambia Mungu yupo ni mkatili na muovu utakubali uwepo wa Mungu?
 
Mchango wa atheism ni upi kwenye jamii?
Mchango wa atheism upo kwenye curiosity kutofautisha vitu myths na reality.

Atheism inakuja kuikomboa jamii kwenye hayo madhoruba niliyokutajia kwa kutoa elimu ya kuwafanya watu wawe na free thinking waweze kutambua kuwa hayo mambo ni uongo.

Atheism ni sumu ya kutokomeza indoctrination walizopandikizwa watu na dini.
 
Unaweza ukatoa mifano hai ya hiyo michango ya atheism katika jamii?
 
Chukulia mfamo wa mechi ambapo timu A inaongoza goli 5 na timu B ina goli 1, imebaki sekunde 30 mpira uishe kutoka kwenye dakika 2 za nyongeza. Je hapo siwezi kuwa na uhakika wa matokeo ya timu A kuwa ndio mshindi wa hiyo mechi inayoendelea?
Sekunde 30 zinatosha kukufanya ukosee.

Na ndio maana hata timu ipate magoli 10 kwa bila hata ifike dakika ya mwishoni itahesabika kuwa inaongoza goli 10 na sio kushinda goli 10 kwasababu mechi haijaisha lolote linaweza kutokea.

Mfano wewe unaweza kudhani ni rahisi kusema sekunde 30 zilizobaki huyo mwenye goli 5 ndio atakuwa mshindi mwisho wa mechi.

Lakini vipi sekunde za mwisho wa mchezo ikatokea vurugu na mechi ikahairishwa?

Maana yake huo ushindi wa magoli 5 hautambuliki, mshindi anapatikana baada ya filimbi ya mwisho.

Vipi katika sekunde za mwisho kukatokea ajali hapo kiwanjani na mechi isiendelee tena?
 
Back
Top Bottom