Scars haaamini kwenye uwepo wa Mungu lakini anaomba dua na kufanya maombi

Scars haaamini kwenye uwepo wa Mungu lakini anaomba dua na kufanya maombi

Huyo hayupo familia na mpira

Yeye anajua maswala ya hija ya kumrushia mawe shetani wakati kiuhalisia lile ni jiwe
sasa yeye kachukulia mfano,
Na mimi nikamwambia chukulia mfano within30 sec likapigwa bomu au mashabiki wakaingia uwanjani kufanya vurugu,

Alikuwa na hakika mpira utaisha?
Mfano wake yeye anaona sawa ila hataki wa mwenzake as if kuna limitation ya vitu vya probability kutokea!
 
Sasa hapo si umeeleza tu tukio na si mchango wa atheism kwenye jamii, hata sasa kuna waumini wenye kuamini dini na Mungu ila wanasema hii miujiza ya manabii ni uzushi si kweli.

Au labda ungefafanua hilo tukio la huyo atheist limeleta mchango gani kwenye jamii? Ni kwamba watu wenye kudai kujua taarifa binafsi za watu pasina kuambiwa huwa wana mtandao wa kukusanya taarifa?
Kwani hilo tukio halijafanywa na Atheist ku debubk nadharia potofu iliyokuwa ina mea katika jamii?

Na sijakuongezea

Kuna challenge ya 1M dollar iliwekwa na huyo huyo James Randi. Kwa watu wote wanaodai kuwa uchawi upo basi wakiweza kuthibitisha uchawi upo watapokea hizo pesa.

Shindano lilianza mwaka 1964 huku maelfu ya watu wakijitokeza kufanya challenge lakini mpaka 2015 shindano linakuja kuwa terminated hakuna hata mmoja aliyeweza kuthibitisha uchawi.

Shindano limedumu kwa miaka zaidi ya 50 lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kuthibitisha uchawi upo.

Je hiyo sio advantage ya atheism katika jamii kutoa mwangaza kwa watu ambao wamekuwa wakidanganyika na mambo ya kishirikina?
 
Si kweli, binaadamu tunatofautiana na tuna mapungufu hivyo uhalisia huwezi kutegemea kila mtu atamtendea mema jirani yake lazima tu wawepo wa kukutendea mabaya.

Kila mafanikio hapa duniani ni kuwa na positive mindset+

Hata kuanzishwa Kwa jamiiforum ilikuwa Kwa ajili ya +mindset
 
Dua si lazima iombwe kwa Mungu. Kuna Polytheistic religions ambapo ndani yake kuna Mystical traditions, Kuna na non-religious perspective kama vile Psychotherapeutic view, Secular humanist view n.k hao wote haya makundi yote yana dua zao lakini hayazielekezi kwa Mungu.
So Scars yupo sawa kuomba Dua bila kumuelekea Mungu.
Chochote unachokiabudu ni mungu kwako.
 
Neno lake lipi?

Kuna maandiko mengi sana yanayo daiwa ni maneno ya huyo Mungu yanayo tofautiana maelezo ya chanzo cha uhai.

Kuna Biblia ya wakristo, Quran ya waislamu, Veda ya wahindu,Tiptaka ya wabudha, Kojik ya washinto n.k
Miungu ipo mingi ila Mungu wa kweli ni mmoja tu. Ni muumba wa ulimwengu wote.
Hakuna neno la Mungu zaidi ya hadithi za kutungwa na kusadikika sawa na Hekaya za Abunuwasi au riwaya za Alfu Lela ulela.

Haiwezekani Mungu huyo awe na maandiko mengi mengi yanayo daiwa ni maneno yake.
Hayo sio maandiko ya Mungu mmoja wa kweli bali miungu mingi pia imeandika.
Mara wakristo wadai biblia ndio neno la Mungu na waislamu wadai Quran ndio neno la Mungu huyo.
Sio Mungu huyohuyo, ni miungu tofauti.
Automatically Mungu huyo Hayupo katika uhalisia ila ni dhana ya kufikirika katika mawazo na imani za watu mbalimbali.

Hakuna neno la Mungu.

Kuna hadithi za kutungwa na kusadikika za kuelezea fictional character Mungu asiye kuwepo.

Biblia, Quran na maandiko yote ya kidini ni sawa na Hekaya za Abunuwasi au riwaya za Alfu Lela ulela.
Haya ni maoni yako, mimi nayaheshimu.
 
Na sio neno dua tu

Hata katika surprise naweza kusema "oh my god"

Just kama wewe unavyokuwa comfortable kutumia neno Thursday bila kujali kuwa umetaja jina la Mungu wa Thor.

Sidhani kama kwa kutaja kwako neno hilo unakuwa ni muumini wa huyo Mungu
Wewe ni muumini katika imani ya atheist. Nyie pia mna mungu wenu anayewaongoza huko na mnamuabudu kwelikweli.
 
Kama roho haionekani, Wewe uli iona wapi ukajua ipo?

Roho isiyo onekana, ilifahamikaje ipo?

Aliyesema roho ipo, Ali iona wapi akajua ipo?

Mtu huyo aliwezaje kuiona roho isiyo onekana?
Aliyesema roho ipo ni Mungu ambaye ndio aliiumba na kuiweka hapo kwenye moyo. Mimi nafahamu ipo kwa imani.
 
Msimamo ni nini?

Kwamba mimi kwasababu ni Atheist unanitazamia kutoniona kanisani kwenye event yeyote?

Nikienda kanisani kuaga mwili wa ndugu yangu hapo nakuwa sina misimamo?

Nikipewa mualiko wa harusi na rafiki yangu napaswa nikatae kwasababu siamini Mungu hivyo sipaswi kwenda kanisani?
Suala la kanisani nani kazungumzia? Kuna mahala nimezubgumza habari ya kanisa?
 
Wakana Mungu wengi ni kama vile walikuwa wanaruka dimwi la maji(dini) na kujikuta wanatua kwenye shimo(kukana uwepo wa Mungu). Hoja zao nyingi ni level ya dini tu kwamba unakuta kuna mambo hakuyaelewa kwenye dini yake na kujikuta wameangukia kuwa wakana Mungu.
Huu ni ukweli kwa asilimia mia moja.
 
Msimamo ni nini?

Kwamba mimi kwasababu ni Atheist unanitazamia kutoniona kanisani kwenye event yeyote?

Nikienda kanisani kuaga mwili wa ndugu yangu hapo nakuwa sina misimamo?

Nikipewa mualiko wa harusi na rafiki yangu napaswa nikatae kwasababu siamini Mungu hivyo sipaswi kwenda kanisani?
Tuambie maombi yako ulikuwa unayaelekeza kwa nani.
 
Mchango wa dini kwenye jamii tunauona sana

Juzi tumepokea taarifa kutoka mahakama kuu ya Arusha kuhusu hukumu ya Masheikh waliorusha mabomu kanisani.

Mchango wa dini katika jamii umekuja kunufaisha kundi dogo la watu huku kundi kubwa likizidi kuangamia.

Kumuona Mzee wa Upako ni 10,000. Kukufanyia maombi maalumu hapo mtakaa chini mfanye makubaliano ya bei.

Kuna yule Kuhani Mussa wa Mbezi, saizi anajenga ghorofa lingine na limefikia hatua za mwishoni kabisa.

Ya Pastor Mackenzie sijui yalivyoishia ila nadhani yupo nyuma ya nondo.

Lakini hilo sio la kustaajabisha, la kustaajabisha ni wale waumini waliookolewa wakiwa katika hali ya udhoofu baada ya wenzao wengi kufariki naskia walienda kumtetea mahakamani Pastor Mackenzie.
Hapa ni sawa na kusema ndege, gari au treni ikipata ajali basi ndege zote, gari zote na treni zote hazina maana na hazina faida.
 
Hapo kwenye gravitational forces acha kuongopa na acha kujifanya mjuaji wa kila kitu. Unaelewa kwamba kuna sehemu nguvu ya uvutano haipo?
Acha propaganda kijana, gravitational force ipo kila mahali.
 
Sasa hapo hakuna tutachoongea!
Hakuna limitation ya kwamba hilo ni nje ya mchezo umetumia neno chukulia mfano na mimi nikajikita katika angle hio hio ya chukulia mfano.

Sababu umetumia propability ya sec30 zilizobaki na mimi natumia hio notion kwamba ndani ya sekunde hizo limeripuka bomu na sekunde hazikuisha

Swali ulikuwa na uhakika mpira utaisha?
Basi kumbe unajadili kitu chengine kabisa ndio maana hatuelewani, suala la mpira kukatishwa kwa dharula yeyote hicho sicho nachojadili mimi bali mie uhakika wangu upo ndani ya mchezo wenyewe. Hayo kupigwa bomu yapo nje kabisa ya mchezo ndio maana nikasema kama mechi ingekuwa inachezwa huko Gaza kweli ningelizingatia hilo la bomu.
 
Basi kumbe unajadili kitu chengine kabisa ndio maana hatuelewani, suala la mpira kukatishwa kwa dharula yeyote hicho sicho nachojadili mimi bali mie uhakika wangu upo ndani ya mchezo wenyewe. Hayo kupigwa bomu yapo nje kabisa ya mchezo ndio maana nikasema kama mechi ingekuwa inachezwa huko Gaza kweli ningelizingatia hilo la bomu.
Yaani nashangaa kwanini unaweka limitation mkuu,
Kwamba ingekuwa gaza ungezingatia hilo? Lakini masheikh waliotuhumiwa kurusha bomu hotel arusha? Je bomu kanisani kule arusha?

Acha kujilimit na hii ni sababu swali lako limekuja chukulia mfano probability haina limitation lolote linaweza kutokea ndani ya sekunde hizo.

Ukitaka toka huko jadili mada.
 
Back
Top Bottom