So Scars kutumia neno dua maana yake anaamini Mungu?
Maana yake na mimi nitakuwa sahihi kusema hata Wakristo na Waislamu watakuwa wanaabudu Miungu ya kigiriki iwapo tutabaini kuna maneno fulani yamayopingana na dini zenu mkiyatumia?
Kwasababu wamekuwa wakitaja miezi ya mwaka kwa kuiita Januari ambapo kimsingi Januari ni jina la Mungu wa kigiriki aitwaye Janus.
Au niseme mnaabudu miungu ya kirumi kwasababu mmekuwa mkiita mwezi wa tatu "March" wakati hilo ni jina la Mungu wa kivita wa kirumi?
Vipi kuhusiana na siku za wiki Monday, Tuesday, Wednesday, Friday, Thursday, Saturday hadi Sunday ambaye ni Mungu jua?
Hujui kwamba hiyo ni Miungu?
Kwahiyo tunapokuona ukitamka tusemeje sasa? Tuseme unatamka hayo maneno kwasababu unaamini hiyo Miungu?
Au tuseme na nyie mnatuektia kusema mnaamini Mungu na wakati tunawaona mnatumia Dollar ya marekani ambayo ina chata ya kishetani ambayo imeelezwa kwenye vitabu vyenu?
****************************
Kujibu swali lako
Kwa bahati mbaya unaonekana kushindwa kuelewa baadhi ya maneno yana double meaning kwa kuchukua maana ile iliyo kaririwa ambayo imekuwa ikitumika sana kimazoea
Neno dua linaweza kuwa na maana nyingine na kutumika kama "wish" au "hope"
Kumtakia mtu heri ya jambo lolote linaloenda kufanyika mbele hiyo sio dua kwa mtazamo wa kidini ni jambo la kiutu katika morality
Lakini kama upo katika circle ya udini lazima uwe na perception ya tofauti unaweza kusema ni dua
Kwa hiyo hayo ni maswala tu ya utata wa maneno hususani pale inapotokea neno kuwa na maana zaidi ya moja huku maana fulani ndio ikiwa inatumika kimazoea kwenye jambo fulani.