Seba aliyeandika meseji kwa rafiki yake amtunzie mwanae na anakata roho kwenye ghorofa ya Kariakoo lililoanguka, akutwa amefariki

Seba aliyeandika meseji kwa rafiki yake amtunzie mwanae na anakata roho kwenye ghorofa ya Kariakoo lililoanguka, akutwa amefariki

Hilo jengo la Kariakoo halijaporomoka kutokana na sababu za kuwepo kwa tetemeko la Ardhi..
Anyway, Ukweli unabaki kuwa Serikali inapaswa kuwa na taasisi imara na madhubuti kabisa za kuweza kupambana na majanga mbalimbali kama haya. Taasisi hizo zinapaswa kuwezeshwa kikamilifu kwa Mafunzo ya Utayari wa Kupambana na Majanga sambamba na kuwezeshwa kwa Vifaa vya Uokozi kwa ajili ya utayari wa kupambana na majanga mbalimbali.

Wananchi nao pia wapewe mafunzo ya utayari wa kuweza kupambana au mafunzo ya mbinu za kuweza kujihami na majanga mbalimbali, Mamlaka zinazohusika na masuala ya kupambana na majanga ziwe zinatoa mafunzo ya namna hii kwa umma.

Aidha, Watu wote waliozembea na kusababisha ajali hii huko Kariakoo wanapaswa kuwajibishwa kwa kufikishwa Mahakamani kwa makosa ya kusababisha vifo vya Watu kwa makusudi. Uwazi unatakiwa sana kwenye suala hili. Wahusika wafikishwe Mahakamani na wawajibishwe. Wafuatao ni Watu wa kuanza nao:-
1.Mmiliki wa Jengo.
2. Mhandisi wa Ujenzi Manispaa ya Ilala, pamoja na Maafisa wengine wote kabisa waliohusika na mchakato wa Kutoa Kibali cha Ujenzi na/au Ukaguzi wa Jengo.
3. Contractor.
4. Consultant.
5. Wahusika wa Usalama Mahali pa kazi (OSHA).,n.k, n.k.
Nakubaliana na wewe kwamba serikali iwekeze sana kwenye mbinu za uokozi, majanga kama haya yanakuja kwa namna tofauti tofauti hivyo mbinu tofauti zinahitajika ili kuwaezesha waokozi, pamoja na hayo serikali inches kuwekeza kwenye mambo yasiyo ya msingi, vifaa vya kisasa ni muhimu, posho na maslahi kwa watu wanaofanya hizo kazi pia.

Lakini pamoja na hayo, bado tukumbuke hilo ni janga kama majanga mengine, ni ngumu sana kufukua vifusi ndani ya 72hrs na kuweza kuokoa watu walifukiwa, kwa kiasi fulani kama kuna vifaa wanaweza kupunguza ila sio rahisi na wala tusiwe watu wa kulalamika kuwa kwa nini kwa nini...
 
Mi pia najiuliza kuna namna gani ya kuharakisha mana lile janga nalo ukikimbia nshale ukisimama nshale..
Kama namna zipo tuziweke wazi mambo kama haya yasijitokeze tena
Ni ngumu mkuu,
Ukisema utumie machinery, unaweza kuua watu zaidi maana linaweza kuporomoka zaidi. Ukisema ufukue taratibu kuna watu wanakosa hewa ndani na wanahitaji uokozi wa haraka. Sio rahisi hata kidogo.
 
Kijana Seba aliyeandika message kwa rafiki yake amtunzie mwanae na anakata roho siku mbili zilizopita.

View attachment 3158342

Mwili wake umeopolewa mda huu ukiwa tayari umeshaanza kuaribika kwenye jengo la Kariakoo.. Tayari mwili wake umepelekwa kwenye hospitali ya Amana kwa kwa taratibu nyingine za kuhustili..Roho ya marehemu ipumzike mahara pema peponi 😭😭 Inasikitisha sana jamani Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un💔🙏
Kuna wale akina LUCAS MWASHAMBWA na wenzake waje hapa kusifia
 
Its painful 😣

Hiv kam jengo moja ndio limeanguk tena ndan ya jiji kubwa na karbu krbu na fire (waokozi) lakn zoez la ukoaji watu halijakamilika itakuwaje siku magorofa 5/20 yakiangukia watu huko mikoa ya pembezon 😐😐
Palestine wapo kwenye vita Kila siku maghorofa yanaangushwa,ila Per capital ya raia wa Palestine ni mara 5 ya raia wa Tanzania ambao hata tu maandamano hamna,then waarabu wakitudharau munasema wana udini sana
 
Imagine dakika ya mwisho mtu ana kufa anachowaza ni kutunza mtoto wake, ina maana Maisha na harakati zake zipo katika malezi ya mtoto!

Wanawake wanatakiwa wajue kwamba kuvunja ndoa kwa upumbavu wao kunakopelekea watoto kuteseka ni mateso Makubwa sana kwa wanaume!
 
Deep sorrow!

But all in all, vifo vya Watu hawa kamwe havikusababishwa kwa kudra ya Mungu, Bali ni kutokana na kuwepo kwa janga la rushwa, uzembe wa makusudi, ufisadi na kushindwa kuwajibika ipasavyo.
Duh! Kama ni hivyo basi hawa wala rushwa, wazembe na mafisadi ni kiboko. Yaani hadi wana ubavu wa kumkaidi Mungu!? Tukimbilie wapi sasa!!!? 🥺🥺🥺🥺
 
Imani yangu inaniambia walokufa ni wengi sana kuliko tunaotangaziwa kwa sasa wanaotangazwa ni wale waliopostiwa mtandaoni ndugu zao wakiwatafuta
Sure thing.. Kuna wale mateja wanalalaga pemben ya maduka, kuna wale wanatembeza mifuko, etc, kuna wale wanaopanga kwenye meza na ngazi, bado wabeba mizigo wale, wapita njia, apo umetoa hao wanaojulikana mawinga na wenye frem zao.. Too sad😭😭😭
 
Back
Top Bottom