Seba aliyeandika meseji kwa rafiki yake amtunzie mwanae na anakata roho kwenye ghorofa ya Kariakoo lililoanguka, akutwa amefariki

Seba aliyeandika meseji kwa rafiki yake amtunzie mwanae na anakata roho kwenye ghorofa ya Kariakoo lililoanguka, akutwa amefariki

Ni ngumu mkuu,
Ukisema utumie machinery, unaweza kuua watu zaidi maana linaweza kuporomoka zaidi. Ukisema ufukue taratibu kuna watu wanakosa hewa ndani na wanahitaji uokozi wa haraka. Sio rahisi hata kidogo.
Nakubaliana na wewe kwamba serikali iwekeze sana kwenye mbinu za uokozi, majanga kama haya yanakuja kwa namna tofauti tofauti hivyo mbinu tofauti zinahitajika ili kuwaezesha waokozi, pamoja na hayo serikali inches kuwekeza kwenye mambo yasiyo ya msingi, vifaa vya kisasa ni muhimu, posho na maslahi kwa watu wanaofanya hizo kazi pia.

Lakini pamoja na hayo, bado tukumbuke hilo ni janga kama majanga mengine, ni ngumu sana kufukua vifusi ndani ya 72hrs na kuweza kuokoa watu walifukiwa, kwa kiasi fulani kama kuna vifaa wanaweza kupunguza ila sio rahisi na wala tusiwe watu wa kulalamika kuwa kwa nini kwa nini...
Kifusi kingewezekana kabisa kufukuliwa kwa muda mfupi, tatizo lililokuwepo ni kwamba hapakuwa na mpaka Sasa bado Hakuna taasisi imara iliyo madhubuti yenye Utayari na nyenzo sahihi za kuweza kupambana na majanga Kama hayo. Hakuna watu/waokozi wenye mafunzo sahihi ya kushughulikia majanga ya namna hiyo na Wala Hakuna nyenzo au vifaa sahihi kwa kazi ya uokozi wa namna hiyo.
Kuna uzembe uliopitiliza kwenye suala hili.
Mathalani, hivi kwa mfano AMRI ingetolewa haraka mara tu ajali ilipotokea ya kuwaleta Wanajeshi wapatao elfu Moja (1000) kwa ajili ya kazi hiyo ya Uokoaji, Je, kweli kwamba kifusi cha jengo hilo tangu ajali ilipotokea hadi leo hii tarehrle 22 Novemba 2023 kingekuwa bado tu hakijaisha??

Vile vile, vifo vya Watu wengi kwenye jengo hilo inaonekana vilisababishwa na ukosefu wa hewa safi (suffocation), jaribu kujiuliza: Je, Serikali ilikuwa na mipango gani ya dharula ili kuhakikisha kwamba Watu waliokuwa chini kwenye basement floor wanapatiwa hewa safi ili wasife kwa kukosa hewa huku zoezi la uokozi likiwa linaendelea? Je, uliona Serikali ilileta mitungi ya kuzalisha gesi ya Oxygen ya dharula hapo kwenye eneo la ajali ili kuwapatia hewa safi Waathirika wa janga hilo waliokuwepo chini ya vifusi kwenye basement floor??

Hosea 4:6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.
 
Lawama zote tunazielekeza kwa serikali pasipo kujua jitihada hazizidi kudra!

Pole nyingi kwa familia, ajaliwe pumziko la amani 🙏, inauma sana, sana ila conclusion maisha si yetu, ashukuriwe aliye tudhamini maisha.
Jitihada gani hizo?

Watu Wana haki zote za kuilaumu Serikali kwenye janga hili. Janga hili Kamwe halikusababishwa kwa kudra za Mungu, this is not a natural disaster, but it is a man-made disaster due to the negligence, corruption, and the total lack of the competent institutions for disasters management and control.

But all in all, Serikali kila siku inakusanya Kodi kutoka kwa Wananchi, lengo kuu kabisa la hizo Kodi zinazokusanywa na Serikali ili kuiwezesha Serikali hiyo kutoa huduma za kijamii kwa umma/Wananchi ikiwemo na hilo suala la kupambana na majanga kama haya ya ajali kama hii ya Kariakoo.
 
Deep sorrow!

But all in all, vifo vya Watu hawa kamwe havikusababishwa kwa kudra ya Mungu, Bali ni kutokana na kuwepo kwa janga la rushwa, uzembe wa makusudi, ufisadi na kushindwa kuwajibika ipasavyo.
Pamoja na hayo,kiongozi wa nchi akaishia kuagiza Tsh 700mill zigawiwe kama bashasha sijui iitwe zawadi kwa timu ya taifa kisa wameshinda mchezo hizo nguvu zisielekezwe kwenye janga kama hili.

Obviously tuna lack of equipment upande wa uokozi so ilikuwa vizuri serikali itafute msaada wa dharura mapema kutoka makampuni mbalimbali yenye vifaa wakashirikiana kufanya kitu.
 
Imagine dakika ya mwisho mtu ana kufa anachowaza ni kutunza mtoto wake, ina maana Maisha na harakati zake zipo katika malezi ya mtoto!

Wanawake wanatakiwa wajue kwamba kuvunja ndoa kwa upumbavu wao kunakopelekea watoto kuteseka ni mateso Makubwa sana kwa wanaume!
Daaah kumbe mkuu sometimes una huruma sana..
Sikutegemea wewe wa kuongea hivi...

Ni kweli ulichoongea mkuu
 
Ata akipatikana na akafungwa au kuhukumiwa kifo itasaidia nini mkuu.

Lazima, lazima ahukumiwe, kwani akiachwa hivi hivi ni kosa kubwa sana, sbb habari zilizoko Kkoo na mitaani ni kuwa alianza ujenzi ambao ni hatari sana kwa kufukua msingi wa ghorofa akitaka kuongeza underground floors ili apate vyumba vingine apate fedha zaidi na ikumbukwe, huwezi fanya ujenzi wa hivyo, ni hatari sana na hakuna kibali cha ujenzi wa aina hiyo, so alifanya ujenzi kiuhuni, kizembe na kusababisha janga kubwa na baya sana kwa Taifa letu, na janga kama hili lingeweza epukika, ni uhuni na upuuzi mkubwa kafanya, kaua watu na huzuni kubwa kwa watanzania wote, hivyo lazima sheria ichukue mkondo wake ili wengine wasidhubutu kamwe kufanya ujenzi wa aina hiyo..!!
 
Wakubwa wapunguze safari, wapeleke watu nje za njee wakajifunze utaalam mbali mbali ikiwa ni pamoja na uokozi.
 
Kifusi kingewezekana kabisa kufukuliwa kwa muda mfupi, tatizo lililokuwepo ni kwamba hapakuwa na mpaka Sasa bado Hakuna taasisi imara iliyo madhubuti yenye Utayari na nyenzo sahihi za kuweza kupambana na majanga Kama hayo. Hakuna watu/waokozi wenye mafunzo sahihi ya kushughulikia majanga ya namna hiyo na Wala Hakuna nyenzo au vifaa sahihi kwa kazi ya uokozi wa namna hiyo.
Kuna uzembe uliopitiliza kwenye suala hili.
Mathalani, hivi kwa mfano AMRI ingetolewa haraka mara tu ajali ilipotokea ya kuwaleta Wanajeshi wapatao elfu Moja (1000) kwa ajili ya kazi hiyo ya Uokoaji, Je, kweli kwamba kifusi cha jengo hilo tangu ajali ilipotokea hadi leo hii tarehrle 22 Novemba 2023 kingekuwa bado tu hakijaisha??

Vile vile, vifo vya Watu wengi kwenye jengo hilo inaonekana vilisababishwa na ukosefu wa hewa safi (suffocation), jaribu kujiuliza: Je, Serikali ilikuwa na mipango gani ya dharula ili kuhakikisha kwamba Watu waliokuwa chini kwenye basement floor wanapatiwa hewa safi ili wasife kwa kukosa hewa huku zoezi la uokozi likiwa linaendelea? Je, uliona Serikali ilileta mitungi ya gesi ya dharula hapo kwenye eneo la ajali ili kuwapatia hewa safi Waathirika wa janga hilo waliokuwepo chini ya vifusi kwenye basement floor??

Hosea 4:6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.
Dogo tuliza mihemko hiyo kazi haikuhitaji nguvu ilihitaji akili, kama unafikiri lilikua linahitaji nguvu basi hadi muda huu kifusi chote kingekua kimezolewa ila hata ambao wametoka hai pengine wangefia pale wote kwahiyo heshimu juhudi za watu au nenda wewe kaonyeshe ujuzi
 
Hivi kumbe Wanajeshi kazi zao zote huwa ni za kutumia nguvu tu peke yake bila akili??
 
Back
Top Bottom