Sefue: Marufuku kutengeneza kadi za Christmas/Mwaka Mpya kwa gharama ya Serikali

Hongera sana JPM, naamini pia matumizi ya magari V8 na mengine yenye matumizi makubwa ya mafuta utayapiga marufuku,
 
Wazee wa 10% wanalo safari hii, mirija yote inakatwa, tutaheshimiana tu hakuna namna
 
Sijui ni cheap popularity au ndo mind games tunachezewa. Yani hata hili ni la kuita press Kweli?

Unaona kabisa ni waraka umeandikwa na kurugenzi ya ikulu kwa vyombo vya habari wewe unasema kaita vyombo vya habari🙄
 
Unaona kabisa ni waraka umeandikwa na kurugenzi ya ikulu kwa vyombo vya habari wewe unasema kaita vyombo vya habari🙄

hajui kwamba hata press conference zinatumia ela nyingi press conference apeleke kwa wasanii Hapa kazi tu
 
HIYO SASA SIFAAAAAAAAAAAAAA,Semeni ukweli mmekuta chochote hazina Vasco Dagama amekomba zote nini? mmezuia safari kwa akina nani tu Mbona nasikia Vasco Dagama wenu yupo Adiss Ababa au mnatoa shukrani kwake kwa kuwaingiza madarakani.Kila kitu kina mwisho.
 

Mashirika ya umma na taasisi za serikali nazo zinategemea hazina!? Au hujui mfuko wa hazina unahusika kwa nani? Hizi kelele kuwa hazina hakuna kitu wakati kila siku tunalipa kodi sijui tuwaeleweje...ni elimu ndogo ama nini!?
 
Kalenda za mashirika ya umma, nazo zifutwe..T-shirt za mashirika nazo zifutwe. Maana huo ni ulaji tu....

Tshirt zina umuhimu wake mkuu llabda watafute njia mbadala za kupata tshirt hizo kwa kalenda nakuunga mkono
 
Suppose press release hii ingetolewa kipindi cha JK? hali ingekuwaje!

Isingewezekana kwa hiyo hakuna sababu ya kupoteza muda kujadili.

JK alikuwa ana exposure zaidi. Vitu kama kadi, billboards etc ni marketing strategy. Sioni kwa nini zipigwe marufuku waziwazi.I hope hii halihusu mashirika ya umma.
 
Kama Hazina haina kitu, abadilishe aseme; Ni marufuku kukopa hizo fedha na atakaye kubali kukopesha asisumbue kuzidai haraka. Tutamuelewa tuu. Huwezi piga marufuku kula nyama ati kwa sababu tu mshahara uliunywea baa. Mshahara ukitoka nyama zitaliwa tu. Wapinzani walikuwa wanalilia nini ka si haya mambo mnayo fanya? Si mliwabeza wapinzani? Fanyeni haya na zaidi tutawakubali tuu. Mlikuwa mmefanya haya, si mngejitokeza na kuonesha umma kuwa mlifanya nini??
 

Wakiristo mwaka huu wataisoma Namba mwaka!waislam hawajazoea kupewa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…