Sehemu gani nzuri Kwa Dar es Salaam Ya kutoka na Mpenzi?

mmh labda ikulu,pale magogoni
 
inategemea mzee chakula ni gharama kubwa tofauti na kitu kingine hasa kwenye hotel labda aende kwa mama lishe ila hotelini laki ndogo
Itabidi next year niende hotel hizi za kawaida tuu, nione

Maake wengine hiyo laki nakula na kunywa mpaka asubuhii
 
Hapa chakula cha bei ya chini kinaanzia 35, acha kumuingiza king
Jamani mnapania sana out! Fries au chips mayai bei gani? mocktail au juice je?

Hizo sehemu mnataka muende peke yenu wenye hela labda.

Binafsi kwasababu ni team seafood chakula changu huwa ghali.. Vyakula vingine vyote huwa bei za kawaida kila sehemu.
 
Coco kuna kiwanja kipo same wall na wavuvi "The reef" ni kipya ukikaa pale unakunywa bia buku tatu huku unamuona aliyekaa wavuvi na bia hiyohiyo kwa buku tisa, hata vyakula ni affordable pia huku mkitizama bahari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…