Self-Contained Houses: Kuna umuhimu gani wa kuwa na choo pamoja na bafu "separately"? Kwanini hivyo nyumba viwili visiwe na matumizi yanayofanana?

Mbona siku hizi tunajenga tu hivo, unakuwa na 2 combined choo na bafu, instead ya choo na bafu separately.
Hii inafaa kama unanyumba ya watu wengi ila kama ni 3bedroom house unaweka tu 1combined choo na bafu na master pia yenye combined choo nabafu
 
Hii ni kutoa nafasi kwa anayeoga aendelee wakati wewe unajisaidia.
 
Shida zipo ukichanganya bafu na choo. Maji ya bafuni yana sabuni ambayo huuwa bacteria wanaobadirisha haja kubwa kuwa maji. Ndio maana kuna tank 2, ya pembe 4 na ya mduara.
Yanakutana baada ya kinyesi kumeng'enywa kwenye tank la pembe 4 ambalo kwa ndani lina sehemu 2 .
Mkuu kama nimekuelewa vizuri;una maana bomba zinazotoka vyooni zielekezwe kwenye tank la pembe nne wakati bafuni na sink za jikoni bomba zielekezwe moja kwa moja kwenye tank la duara?

Mafundi wengine siyo kabisa yani!!!
 
Good point but kule nje yale mashimo ya choo (septic na soak away pit) ya mviringo na lile la mstatili mbona yanapokea uchavu wote wa chooni na bafuni?
Kutokana na post chache nilizozipitia hapo juu inaonekana kuwa hili ni tatizo haikutakiwa kuwa hivi na hii hutokana na mafundi wetu wengi hawakupitia kusoma au hawaijui science ya majitaka na wengi wetu pia hatujui.

Mf mimi,majitaka ya ndani vyoo bafu sink za jikoni na bomba la choo cha nje ambako pia hutumika kuoga yameelekezwa kwenye chamber ndogo ya mstatili kisha ndo yaingie kwenye shimo la mduara na ukiangalia kulikuwa na uwezekano wa kuyatenganisha,mafundi ndo tatizo haikupaswa kuwa hivi.
 
Jibu hili kidogo lina mantiki kitaalamu.
Wengine wamepuyanga tu hakuna aliyetoa jibu lenye uzito.
 
Uko sahihi mkuu.
Hata mimi nyumba yangu vyoo vyake nimejenga hivyo.
Yaani kuna vichumba viwili public toilets ambacho kila kimoja kina choo na bafu ni humo humo,na nje ya nyumba tena kuna vingine viwili vya staili hyo hyo.
Maana mimi huwa nikiamka kwenda kuoga huwa namaliza kila kitu humo humo,nitaanza kuswaki kisha nakata gogo halafu namalizia kuoga.
Huwa sipendi nikate gogo nimalize halafu nivae nguo nitoke niingie chumba kingine kwa ajili ya kuoga tena inakuwa ni usumbufu usio na faida.
Sasa ukishakuwa na vyoo viwili vyenye bafu humo hata uwe na familia kubwa hakutakuwa na foleni ya kwenda chooni maana vyoo na bafu vipo vingi.
 
MARAHABA
 
Siku atakutembelea mama mkwe wako yupo chooni na wew unataka kuoga uwahi kazini. Hapo ndo utatamani ujenge bafu separateli
Ivi mama mkwe ni nani mpaka mnamwogopa ivi? yani ushaoa, lakini bado hujiamini!
Mbona wanatongozeka tu!
 
Mbona siku hizi tunajenga tu hivo, unakuwa na 2 combined choo na bafu, instead ya choo na bafu separately.
Hii inafaa kama unanyumba ya watu wengi ila kama ni 3bedroom house unaweka tu 1combined choo na bafu na master pia yenye combined choo nabafu


Mkuu dist111 upo sawa but master yenye combined choo na bafu hiyo ni gharama bora gharama utakayotumia kujenga bafu kwenye master ukajenge choo nje kwa ajili ya wageni,kiusalama inashauriwa siyo kila mgeni anatakiwa atembee hovyo kwenye nyumba yako wengine wanaweza kuwa wachora ramani ukashangaa usiku unavamiwa na wezi.
 
Mkuu mbona ni kawaida master kuwa na bathroom yake? Una maana wewe master bedroom yako haina bathroom yake? Mimi naona ni vizuri kuwa na master yenye bathroom yake na bathroom ingine ya jumuia.
NB: bathroom namaanisha kuna Choo na bafu humo humo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…