Self-Contained Houses: Kuna umuhimu gani wa kuwa na choo pamoja na bafu "separately"? Kwanini hivyo nyumba viwili visiwe na matumizi yanayofanana?

Self-Contained Houses: Kuna umuhimu gani wa kuwa na choo pamoja na bafu "separately"? Kwanini hivyo nyumba viwili visiwe na matumizi yanayofanana?

Mbona siku hizi tunajenga tu hivo, unakuwa na 2 combined choo na bafu, instead ya choo na bafu separately.
Hii inafaa kama unanyumba ya watu wengi ila kama ni 3bedroom house unaweka tu 1combined choo na bafu na master pia yenye combined choo nabafu
 
Hii ni kutoa nafasi kwa anayeoga aendelee wakati wewe unajisaidia.
 
Shida zipo ukichanganya bafu na choo. Maji ya bafuni yana sabuni ambayo huuwa bacteria wanaobadirisha haja kubwa kuwa maji. Ndio maana kuna tank 2, ya pembe 4 na ya mduara.
Yanakutana baada ya kinyesi kumeng'enywa kwenye tank la pembe 4 ambalo kwa ndani lina sehemu 2 .
Mkuu kama nimekuelewa vizuri;una maana bomba zinazotoka vyooni zielekezwe kwenye tank la pembe nne wakati bafuni na sink za jikoni bomba zielekezwe moja kwa moja kwenye tank la duara?

Mafundi wengine siyo kabisa yani!!!
 
Good point but kule nje yale mashimo ya choo (septic na soak away pit) ya mviringo na lile la mstatili mbona yanapokea uchavu wote wa chooni na bafuni?
Kutokana na post chache nilizozipitia hapo juu inaonekana kuwa hili ni tatizo haikutakiwa kuwa hivi na hii hutokana na mafundi wetu wengi hawakupitia kusoma au hawaijui science ya majitaka na wengi wetu pia hatujui.

Mf mimi,majitaka ya ndani vyoo bafu sink za jikoni na bomba la choo cha nje ambako pia hutumika kuoga yameelekezwa kwenye chamber ndogo ya mstatili kisha ndo yaingie kwenye shimo la mduara na ukiangalia kulikuwa na uwezekano wa kuyatenganisha,mafundi ndo tatizo haikupaswa kuwa hivi.
 
Kwa ujenzi wa kisasa una weka chumba kimoja kwa taka za ndani ya mwili kinyesi na mkojo na za nje kuoga kupiga mswaki n.k angalizo kama hauna hela za kutosha ni bora ukajenga kwa kutenganisha kwa sababu maji ya taka ya nje mwili na manisha yenye sabuni na kemikali kama shampool zina weza kuingia kwenye sinki la choo na kupelekea kuua backteria wanao mengenya kinyesi na kupelekea choo kujaa haraka ni hayo tu
Jibu hili kidogo lina mantiki kitaalamu.
Wengine wamepuyanga tu hakuna aliyetoa jibu lenye uzito.
 
Aisee maada nzuri sana hii, hata mimi kiukweli sion haja ya Kujenga choo na bafu kwa kutofautisha, hapo inatakiwa choo na bafu viwe chumba kimoja ila kama utataka kuwe na vyumba viwili basi kila chumba kiwa na choo na bafu humohumo kwani matumizi ni yaleyale, haiwezekani unaingia hiki kwa matumizi mengine halafu ukimaliza unatoka na kuingia chumba kingine kuoga huo ni usumbufu usio na maana....

Hapa nimepata hilo wazo punde hiki chumba cha bafu humu ndani nitamuita Fundi tujadiriane ili ikiwezekana kilekebishwe kiwe kinatoa huduma zaidi ya moja
Uko sahihi mkuu.
Hata mimi nyumba yangu vyoo vyake nimejenga hivyo.
Yaani kuna vichumba viwili public toilets ambacho kila kimoja kina choo na bafu ni humo humo,na nje ya nyumba tena kuna vingine viwili vya staili hyo hyo.
Maana mimi huwa nikiamka kwenda kuoga huwa namaliza kila kitu humo humo,nitaanza kuswaki kisha nakata gogo halafu namalizia kuoga.
Huwa sipendi nikate gogo nimalize halafu nivae nguo nitoke niingie chumba kingine kwa ajili ya kuoga tena inakuwa ni usumbufu usio na faida.
Sasa ukishakuwa na vyoo viwili vyenye bafu humo hata uwe na familia kubwa hakutakuwa na foleni ya kwenda chooni maana vyoo na bafu vipo vingi.
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Katika ujenzi wa kisasa, kuna umuhimu gani wa kuwa na choo pamoja na bafu "separately" katika nyumba ambazo ni self-contained? Kwanini hivyo nyumba viwili visiwe na matumizi yanayofanana?

View attachment 1587202

Yaaani yale yanayofanyika bafuni yafanyike pia kule chooni na yale ya chooni pia yafanyike bafuni.

Kwanini baadhi ya watu hupendelea kuwa na chumba kimoja ambacho kinakuwa na matumizi ya namna zote mbili ila wengine hutenga vumba viwili vikiwa na matumizi mawili tofauti?

WATAALAM WA MASUALA YA UJENZI PAMOJA NA DESIGNING MSIPITE BILA KUTOA UFAFANUZI JUU YA HII TREND.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE.
MARAHABA
 
Mbona siku hizi tunajenga tu hivo, unakuwa na 2 combined choo na bafu, instead ya choo na bafu separately.
Hii inafaa kama unanyumba ya watu wengi ila kama ni 3bedroom house unaweka tu 1combined choo na bafu na master pia yenye combined choo nabafu


Mkuu dist111 upo sawa but master yenye combined choo na bafu hiyo ni gharama bora gharama utakayotumia kujenga bafu kwenye master ukajenge choo nje kwa ajili ya wageni,kiusalama inashauriwa siyo kila mgeni anatakiwa atembee hovyo kwenye nyumba yako wengine wanaweza kuwa wachora ramani ukashangaa usiku unavamiwa na wezi.
 
Hakika mkuu una haki ya kuitikia na very soon utaingizwa kwenye rekodi za dunia....
IMG_20201002_091053.jpg
 
Mkuu dist111 upo sawa but master yenye combined choo na bafu hiyo ni gharama bora gharama utakayotumia kujenga bafu kwenye master ukajenge choo nje kwa ajili ya wageni,kiusalama inashauriwa siyo kila mgeni anatakiwa atembee hovyo kwenye nyumba yako wengine wanaweza kuwa wachora ramani ukashangaa usiku unavamiwa na wezi.
Mkuu mbona ni kawaida master kuwa na bathroom yake? Una maana wewe master bedroom yako haina bathroom yake? Mimi naona ni vizuri kuwa na master yenye bathroom yake na bathroom ingine ya jumuia.
NB: bathroom namaanisha kuna Choo na bafu humo humo.
 
Back
Top Bottom