Self-Contained Houses: Kuna umuhimu gani wa kuwa na choo pamoja na bafu "separately"? Kwanini hivyo nyumba viwili visiwe na matumizi yanayofanana?

Self-Contained Houses: Kuna umuhimu gani wa kuwa na choo pamoja na bafu "separately"? Kwanini hivyo nyumba viwili visiwe na matumizi yanayofanana?

Mkuu dist111 upo sawa but master yenye combined choo na bafu hiyo ni gharama bora gharama utakayotumia kujenga bafu kwenye master ukajenge choo nje kwa ajili ya wageni,kiusalama inashauriwa siyo kila mgeni anatakiwa atembee hovyo kwenye nyumba yako wengine wanaweza kuwa wachora ramani ukashangaa usiku unavamiwa na wezi.
Siku hizi vyoo vya nje vinajengwa na storage kabisa na ontop of it unaweka tank la kuhifadhia maji.
Kama uko vzr zaid unajenga simtank tower ambapo chini kuna choo na store juu yake unaweka reading room na juu kabisa ndo unaweka tanki la maji. Ni uwezo tu, maaidea yako kibao
 
Hebu jaribu kuwa mtulivu kwenye kuelewa hoja. Umejibiwa akija mama mkwe ameenda chooni na wewe unataka ukaoge uende kazini utamgongea umwambie toka mama nataka kuoga??? Halafu jiulize kama nyumba ina watu 8 au 10 na watoto itakuwaje???
mtoa mada anauliza kwanini hizo choo na bafu zisifanye kazi moja? yani hivyo vyumba viwili viwe vyote ni bafu na choo humo humo

Sent from my Nokia 1 using JamiiForums mobile app
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Katika ujenzi wa kisasa, kuna umuhimu gani wa kuwa na choo pamoja na bafu "separately" katika nyumba ambazo ni self-contained? Kwanini hivyo nyumba viwili visiwe na matumizi yanayofanana?

View attachment 1587202

Yaaani yale yanayofanyika bafuni yafanyike pia kule chooni na yale ya chooni pia yafanyike bafuni.

Kwanini baadhi ya watu hupendelea kuwa na chumba kimoja ambacho kinakuwa na matumizi ya namna zote mbili ila wengine hutenga vumba viwili vikiwa na matumizi mawili tofauti?

WATAALAM WA MASUALA YA UJENZI PAMOJA NA DESIGNING MSIPITE BILA KUTOA UFAFANUZI JUU YA HII TREND.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE.
Nitarudi
 
Matumizi ya choo ni machache yenye udharula fulani hivi (kumwagikia na kutaga)
Bafu lina matumizi mengi kuanxi kuoga wengine wanatumia kufulia kujiwekea usafi wa ziada ndevu na ndugu zake ndevu(wakubwa wataelewa) .
Kwa hiyo bafuninkuna uwezekano mtu kutumia muda mrefu wakati chooni kumwaga ni 1minute na gogo kama liko sawa ndani ya dk 4 mchezo umeisha!
Sasa jipendekeze fanya fussion halafu dogo kaingia huko anaoga ananyaku nakujokoa then amalizie na nyeto halafu mzee baba una mzigo wa kiporo cha maharage utajisaidia kwenye beseni
 
Yaani una maanisha kama hivi? Nafikiri ukiweka squat-toilet kama hicho ktk picha uliyoweka ni heri ujenge hivyo hivyo choo na bafu vijitenge ila ukiweka choo cha kukaa unaweza kuweka bathtub au shower box au ukatenganisha na kioo tu.
 
Attachments

  • a97d93fbe030e85a4e04d84e4cbc9067.jpg
    a97d93fbe030e85a4e04d84e4cbc9067.jpg
    25.1 KB · Views: 8
Mkuu mbona ni kawaida master kuwa na bathroom yake? Una maana wewe master bedroom yako haina bathroom yake? Mimi naona ni vizuri kuwa na master yenye bathroom yake na bathroom ingine ya jumuia.
NB: bathroom namaanisha kuna Choo na bafu humo humo.

Master nimeweka choo tu mkuu ila public ndo ipo separated bafu na choo,nadhani jenzi nyingi bongo tunafanya hivi tukiamini tunaokoa baadhi ya gharama.
 
Siku hizi vyoo vya nje vinajengwa na storage kabisa na ontop of it unaweka tank la kuhifadhia maji.
Kama uko vzr zaid unajenga simtank tower ambapo chini kuna choo na store juu yake unaweka reading room na juu kabisa ndo unaweka tanki la maji. Ni uwezo tu, maaidea yako kibao
Sure mkuu!
 
Yaani una maanisha kama hivi? Nafikiri ukiweka squat-toilet kama hicho ktk picha uliyoweka ni heri ujenge hivyo hivyo choo na bafu vijitenge ila ukiweka choo cha kukaa unaweza kuweka bathtub au shower box au ukatenganisha na kioo tu.
Sijawahi tumia choo Cha kukaa, naomba nielekezwe namna ya kukitumia!
 
Kwa kifupi mkuu ujenzi mwingi hapa bongo watu wana copy na Ku paste..
Ukiuliza kwann nyumba nyingi chini wanapaka rangi nyeusi,,au wanapaka rangi tofauti na rangi ya ukuta wa juu ,,majibu hakuna,
Nyumba nyingi ni mfumo wa sketi na blauzi..

Watu mna maneno jamani [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Master nimeweka choo tu mkuu ila public ndo ipo separated bafu na choo,nadhani jenzi nyingi bongo tunafanya hivi tukiamini tunaokoa baadhi ya gharama.
Master umeweka choo tu mkuu? Sasa ukitaka kuoga huwa unafanya nini mzee baba?
 
Back
Top Bottom