Sensa 2022: Tanzania ina idadi ya watu 61,741,120

Sensa 2022: Tanzania ina idadi ya watu 61,741,120

Kulikuwa na haja gani ya kutumia mapesa yote yale kupata takwimu ambazo tayari mlikuwa nazo?
 
mkoa wa DSM unaongoza kwa watu nchini, wapo 5,383,728 sawa na asilimia 8.7 ya watu wote nchini, na mkoa wa pili ni mwanza wenye wakazi 3,696,872 sawa na asilimia 6.

  1. Msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia. Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa...........

SOMA ZAIDI: Source : National Bureau of Statistics - Maandalizi ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022



TOKA MAKTABA:
06 AUGUST 20202


TUNDU LISSU - MATOKEO YA SENSA YATUMIKE KUPATA IDADI SAHIHI YA MAJIMBO YA UCHAGUZI NA WAWAKILISHI BUNGENI



Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Tundu Antipas Lissu akiangalia mgawanyo wa majimbo yenye watu wengi zaidi anagundua kuwa haiwakilishi na idadi inayostahili ya wabunge. Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam Mwanzo

Mfano mkoa wa Dar es Salaam ulitakiwa kuwa na wabunge wasiopungua 25. Lakini una wabunge wachache sana wakati ina idadi kubwa ya wapiga kura .

Mkoa wa Lindi yenye wabunge 9 huku idadi ya wapiga kura ni ndogo sana. Mkoa wa Tabora ina idadi ndogo ya wapiga kura lakini ina wabunge wa kuchaguliwa 12 huku mkoa wa Tanga wenye idadi ndogo pia ya watu ina wabunge 12. Mikoa hii iliyotajwa kama mfano wa uwiano usiolingana baina ya idadi ya wapiga kura na wingi wa wabunge pia ni maeneo yaliyo ngome ya CCM.

Na kwa hiyo mgawanyo wa majimbo umeiba uchaguzi kwa kutumia mifumo ya kikatiba na kitaasisi kwa maana Tume ya Uchaguzi ni ya rais na mwenye mamlaka ya kutengeneza mikoa ni rais na mteuzi wa viongozi wa Tume ya Uchaguzi ni rais pia. Orodha ya Jumla ya majimbo ya uchaguzi kwa kufuata na tovuti ya bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni majimbo 273 : source : Parliament of Tanzania
READ MORE :
 
Sijui mimi ni wa ngapi katika hao wote,,,,,,,,,,au hatupangwi kwa umri??😀😀
 
Leo hii tumefika ukingoni mwa zoezi la sensa tulilofanya kwa ufanisi mkubwa. Sensa hii imefuata vigezo vyote vya kimataifa.

Maana ya Sensa ya Watu na Makazi

Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum.

Kwa maana nyingine, sensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi na hali yao ya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi.

Takwimu hizi za msingi ndiyo zinazoweza kuanisha mahitaji halisi ya wananchi yakiwemo makundi maalum yenye uhitaji maalum kwa mfano, watu wenye ulemavu, wanawake, watoto, vijana na wazee hivyo kurahisisha uandaaji wa sera na mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji na mazingira yaliyopo

Umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Umuhimu wa kipekee wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni pamoja na:-

  1. Kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa;
  2. Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali;
  3. Taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango katika ngazi zote;
  4. Kigawio katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi;
  5. Taarifa itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira; na
  6. Msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia. Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa...........

SOMA ZAIDI: Source : National Bureau of Statistics - Maandalizi ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022
 
Mbona ongezeko limekuwa dogo sana? Au wengine ni wale waliopubguzwa na uviko 19? Nilijua tutafika 65m
 
Fertility rate inaongezea,last sensa ilikuwa 2.7 na Kwa hesabu za Leo iko 3.2 so inazidi kuongezeka maana vijana ni wengi na wanaokufa wanakuwa wachache..
Ulitumia kiungo gani kusikia?
Hakuna sehemu wamesema Tumeongezeka 10mil

Ongezeko ni watu milioni 16+ ndani ya miaka 10

Matarajio ni kufikia watu 100+mil mwaka 2050
Mada imeandikwa kuwa mwaka 2025 watu watakuwa 67m hiyo ni ongezeko la watu 6m kutoka idadi ya leo. Sasa itakuaje kwa miaka 25 (2025-2050) watu waongezeke kwa 60m wakati kwa miaka 10 (2012-2022) watu wameongezeka sio zaidi ya 12m.?
 
Mada imeandikwa kuwa mwaka 2025 watu watakuwa 67m hiyo ni ongezeko la watu 6m kutoka idadi ya leo. Sasa itakuaje kwa miaka 25 (2025-2050) watu waongezeke kwa 60m wakati kwa miaka 10 (2012-2022) watu wameongezeka sio zaidi ya 12m.?
Unaelewa maana ya fertility rate? Nimekwambia fertility rate inaongezeka kadiri tunavyosonga mbele kwa lugha rahisi ita double..
 
Sio haba, nguvu kazi tunayo ya kutosha.
sasa tupange maendeleo.
kutoka mwaka 2012 hadi 2022 kuna ongezeko la watu 16, 812,197 sawa na 3.2%
Ongezeko kubwa la watu lisiloendana na uwezo wa rasilimali za kuwatosheleza au huduma muhimu ni hatari
 
Back
Top Bottom