Sensa 2022: Tanzania ina idadi ya watu 61,741,120

Sensa 2022: Tanzania ina idadi ya watu 61,741,120

Zile sms zakualikana uwanjani mbona zilitosha kutua hizi taarifa
Au basi watumie televisheni ya taifa kutupa taarifa na vyombo vingine vya habari vingealikwa
Tunasubiri shughuli ingine basi
 
Mada imeandikwa kuwa mwaka 2025 watu watakuwa 67m hiyo ni ongezeko la watu 6m kutoka idadi ya leo. Sasa itakuaje kwa miaka 25 (2025-2050) watu waongezeke kwa 60m wakati kwa miaka 10 (2012-2022) watu wameongezeka sio zaidi ya 12m.?
Hakuna sehemu serikali imesema watu watakuwa milioni 150
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitangaza Matokeo ya Sensa na Watu na Makazi ya Mwaka 2022 katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma leo tarehe 31 Oktoba, 2022



Samia Suhuhu Hassan - Rais
Nataka niitangazie dunia kuwa Sensa ya watu na makazi ya 2022 imefuata vigezo vilivyowekwa na umoja wa mataifa.

Tumeandika historia kwa mara ya kwanza tangu tupate uhuru, tumeweza kupata idadi ya majengo yote pamoja na anwani za makazi.

Leo hii tumefika ukingoni mwa zoezi la sensa tulilofanya kwa ufanisi mkubwa. Sensa hii imefuata vigezo vyote vya kimataifa.

Kwa mamlaka niliyopewa na katiba ya JMT ya mwaka 1977, nawatangazia kuwa Tanzania ina idadi ya watu 61,741,120.

Watu 59,851,347 wapo Tanzanzia bara na 1,889,773 Tanzania zanzibar.

Wanawake wapo 31,687,990 sawa na asilimia 51 ya watu wote na wanaume ni 30,530,130 sawa na asilimia 49 ya watu wote.

Kati ya mwaka 2012 hadi 2022, ongezeko la watu ni 19,812,197 sawa na asilimia 3.2

Tanzania bara, mkoa wa DSM unaongoza kwa watu nchini, wapo 5,383,728 sawa na asilimia 8.7 ya watu wote nchini, na mkoa wa pili ni mwanza wenye wakazi 3,696,872 sawa na asilimia 6.

Idadi ya mejengo ni 14,348,372 ambapo Tanzania bara yapo 13,907,951 na Zanzibar yapo 440,421

Vituo vya kutolea huduma za afya vipo 10067 ambapo zahanati zipo 7889, vituo vya afya 1490 na hospitali 688.

Upande wa shule, zipo 25,626 ambapo shule za msingi zipo 19,769 na shule za sekondari zipo 5857

Makadirio yanaonesha kuwa hadi kufikia mwaka 2025 Tanzania itakuwa na watu 67,962,097 na hadi kufikia mwaka 2050 idadi itafikia 151,252,429.

Asanteni kwa kunisikiliza, Mungu aibariki nchi yetu, Mungu aibariki Afrika. Asanteni sana kwa kunisikiliza.

Hiyo ongezeko la watu milioni 19.8 Mbona sio sahihi?
 
Huko unakoita kufuja pesa nako kunachochea uchumi.

Imagine wewe Leo ingekuwa kampuni yako inalipwa kutokana na mapambo Tu ya event husika, ungesema kuna ufujaji? serikali ikitumia hela zinarudi Kwa wananchi...ni Bora government spending kuliko kubana bana matumizi kupita kiasi
Bora umewambia kuna watu wanadhani hela zinapatikana mtaani kutoka mbinguni,hawajui kuwa serikali isipo spend hela hata mtaani zitakosekana.
 
Bora umewambia kuna watu wanadhani hela zinapatikana mtaani kutoka mbinguni,hawajui kuwa serikali isipo spend hela hata mtaani zitakosekana.


Hili somo humu Sana Kwa mijitu inayopenda kukosoa kila kitu
 
Daaah hizo hesabu zao zipo sawa kweli!!!! Mboni wanichanganya jamani
 
Back
Top Bottom