Septemba 07, 2022 ndiyo iPhone 14 inazinduliwa. Wapenzi wa iPhone tukutane hapa kujuzana prices and specs

Septemba 07, 2022 ndiyo iPhone 14 inazinduliwa. Wapenzi wa iPhone tukutane hapa kujuzana prices and specs

Usd 700 umezitolea wapi mkuu?, ninachojua ni kwanzia usd 999-1099, kwa Pro na Pro max
Ngoja tuone
inbound5776735548881602126.png
 
Hivi hapa bongo kuna authorized apple reseller where i can trade in simu niliyonunua USA? Achana na wale wa Mwenge na Makumbusho.
Migombani street mikocheni ipo, mlimani city ila naona jamaa wa pale kama janja janja mingi kama duka la ki. Koo
 
2.5 ml ni bei ya kawaida sana wengi hawashindwi kuafford ila ni ile ego kwamba bora ninunue tofali au kiwanja!
Lakini unaunua simu ya 2.5 unazalisha au show off! Mie mwenyewe huenda nikatoka kwenye huo utumwa wa hizo simu za bei.. Simu ya laki tisa ina kila kitu nahitaji
 
2.5 ml ni bei ya kawaida sana wengi hawashindwi kuafford ila ni ile ego kwamba bora ninunue tofali au kiwanja!
yah kuna kasauti tu kanakufokea kimya kimya kwamba unatembeaje na simu ambayo ni sawa na tofali 2500??basi unajikuta unakosa ujasiri wa kwenda dukani unabeba zako infinix la laki na 80 unaunga wasap🤣🤣🤣
 
Constraint ni hela na choices tu mkuu,

Kuna kipindi nilikuwa nasema sioni umuhimu wa kununua TV, kila kitu nitakuwa na stream kwenye PC.

Sasa bwana kuna rafiki yangu akatoka mkoa akapita kuja kunisalimu, alivyokuta na stream TV online kupitia PC akaniuliza why? Nikamwambia sioni umuhimu wa ku-spend extra income kununua TV wakati kila kitu napata kupitia PC.

Jamaa yangu aliniangalia sana alafu akacheka, akaniambia " Pesa inapoishia, na akili huishia hapo hapo" . Niliitafakari uhalisia wa kauli yake to some extent nikaona ina make sense kabisa, nikaona isiwe tabu kabisa, nikafanya maamuzi.

Kwenye maisha inategemea mtu ana-value nini, na kwendana na hoja za kila mmoja ukizipima unaweza kukuta kila mmoja ni sahihi kwa njia yake, na huo ndo upekee wa maisha.

Ingawa binafsi kununua simu ya 3-4M ni hapana, ila sishangai mtu anaponunua as long as inampa furaha na comfortability. Sometimes life is too short to complicate it.
 
Back
Top Bottom