yah kuna kasauti tu kanakufokea kimya kimya kwamba unatembeaje na simu ambayo ni sawa na tofali 2500??basi unajikuta unakosa ujasiri wa kwenda dukani unabeba zako infinix la laki na 80 unaunga wasap🤣🤣🤣
Constraint ni hela na choices tu mkuu,
Kuna kipindi nilikuwa nasema sioni umuhimu wa kununua TV, kila kitu nitakuwa na stream kwenye PC.
Sasa bwana kuna rafiki yangu akatoka mkoa akapita kuja kunisalimu, alivyokuta na stream TV online kupitia PC akaniuliza why? Nikamwambia sioni umuhimu wa ku-spend extra income kununua TV wakati kila kitu napata kupitia PC.
Jamaa yangu aliniangalia sana alafu akacheka, akaniambia " Pesa inapoishia, na akili huishia hapo hapo" . Niliitafakari uhalisia wa kauli yake to some extent nikaona ina make sense kabisa, nikaona isiwe tabu kabisa, nikafanya maamuzi.
Kwenye maisha inategemea mtu ana-value nini, na kwendana na hoja za kila mmoja ukizipima unaweza kukuta kila mmoja ni sahihi kwa njia yake, na huo ndo upekee wa maisha.
Ingawa binafsi kununua simu ya 3-4M ni hapana, ila sishangai mtu anaponunua as long as inampa furaha na comfortability. Sometimes life is too short to complicate it.