G.Man
JF-Expert Member
- Feb 9, 2014
- 1,040
- 2,157
Mambo vipi,
Moja kwa moja kwenye mada. Juzi nikiwa kwenye daladala nikasikia watu wakilaumu Serikali kwamba ''Heri Magufuli alivyo kuwepo, saivi watoto wametakiwa kulipa michango ya kama 22k shuleni'', sikuweza kuchangia neno lakin niliwaza sana, Seriously! mchango kama huo kwa mwaka kwaajili ya mwanao kupata elimu unaonekana ni uonevu!
Naishauri Serikali kama ina nia njema ya kuwapa wananchi maendeleo ya Kifikra bila kuangalia mtaji wa kura, irudishe ada shuleni na kutumia hizo pesa kuboresha mifumo ya kielimu kama kuajiri walimu wa kutosha. Kulikoni mpaka leo kuendelea kutegemea mikopo na wahisani hata kujenga vyoo. Tunabembelezana sana kwenye mambo ya msingi kisa tu wanasiasa wanataka Kura. Nafahamu kuwa zipo kaya Masikini sana lakini kunaweza kukawa na mpango maalumu kwa ajili ya watu kama hao.
Kuna wakati nilimsikia Waziri wa TAMISEMI akisema wanafunzi waruhusiwe kwenda shule bila Uniform.! Siku nyingine hawa si watasema hawana kalamu alafu waambiwe hata wasipoandika hamna shida?! Sasa kwa hali kama hiyo kwanini serikali isichukue tu ada alafu wa provide wenyewe Uniform na vitendea kazi kama madaftari?
Hivi wale watoto wanaolipiwa 30mil kwenye International Schools ndo unataka wawe na soko sawa la ajira na wanetu hawa wa kajamba nani?
Si bure tunasoma ili tu kuhitimu na ndio maana hatuna uwezo wa kufikiri kwa kina na kuhoji mambo yanayohitaji uwezo mdogo tu wa akili, zaidi tunafata mkumbo.
Mungu atusaidie!