Uchaguzi 2020 Sera ya majimbo itaua utaifa na uzalendo

Uchaguzi 2020 Sera ya majimbo itaua utaifa na uzalendo

Nimesikia chama kimoja kinazungumzia nchi kuigawa kwenye majimbo ya kiutawala na uendeshaji. Kwangu mimi kwa nchi ambayo imekuwa kwenye utawala wa mikoa kwa miaka zaidi ya 50 na kwa mfumo wa kugawana mapato kupitia serikali kuu na serikali za mitaa kwa baadhi ya mapato haileti mantiki kubadili mfumo kwenda kwenye majimbo ambayo yanaweza kuua utaifa na kuleta mfarakano. Mfumo wa sasa unaondoa u-mimi na maendeleo ya uchumi yanayopishana- Regional economic imbalances - ambao utaacha baadhi ya maeneo kwenye umasikini mkubwa. Baadhi ya athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na:

1. Maeneo yenye raslimali kidogo kuendelea kuwa maskini na maeneo mengine kuwa tajiri na hivyo kuwa na mchango mdogo wa GDP

2. Ajira ndogo kwenye baadhi ya maeneo yenye raslimali chache na hivyo ongezeko la idadi ya watu kwenye maeneo yenye utajiri wa raslimali

3. kila jimbo kuwa na sheria zake za kiutawala, bunge dogo, polisi nk hali inayoweza kujenga mwelekeo wa kujitenga. Rejea matatizo yakujitenga kwa Biafra Nigeria miaka ya nyuma.

4. Nchi zenye majimbo mf Msumbiji hazina hakikisho la maendeleo endelevu kuzidi ambazo hazina utaratibu huo ie Tanzania

5. Mfumo huo utakuwa na gharama kubwa kuuanzisha

Kimsingi hadi sasa mfumo uliopo hauna shida changamoto kubwa ni kuweka mifumo mizuri ya udhibiti matumizi na mapato ya serikali kwa kuyagawa kwa haki ili kila eneo la serikali liweze kunufaika. Na hususani kuimarisha mfumo wa Halmashauri uweze kukabiliana na changamoto za kiuchumi kwa kila eneo. Iwapo kuna changamoto za mgawanyo sawia basi tupitie upya sera na sheria zetu ndani ya mfumo uliopo tuboreshe.

6. Hata hivyo, Kwa maoni yangu badala ya utawala wa majimbo ni afadhali kuweka kanda za kiuzalishaji ili kuchochea uchumi wa kimaeneo kulingana na mazingira ya kiuchumi na uzalishaji kwa kila eneo.
 
Attachments

Kenya enzi ya KANU ilikuwa nchi ya kijinga kwelikweli ila baada ya mabadiliko ya katiba Kenya unaiona sasa ilipo? Yani khaya mazimwi yoooteee yameondoka sisi tumebaki na hili la CCM tumeling'ang'ania.
Hata Mimi nashangaa
 
Kwani sera ya majimbo inasema hakuna kuoana??? China Mtu wa Shanghai hawezi kuoa Beijing??? Ndo unavyoelewa hivyo Sera za majimbo wewe kilaza wa Lumumba???
Vilaza wa ufipa mnashindwa kabisa kuisoma Tanzania mnabakia kuja na mifano ya China na Marekani😂😂.
 
Marekani china Japan Indian na Nchi nyingi Duniani wanatumia mfumo wa majimbo na Hakuna Tatizo lolote
Historia zao na misingi ya mataifa yao ni tofauti na sisi. Jitahidi kwanza kutafuta elimu pana ya maisha ya watu kabla ya kukurupuka kuiga mifumo yao ya kiserikali.
 
Akili mbovu kabisa hizi..... Kanyaga twende Tundu Lissu hakuna tena teuzi za kizembezembe......

Waliopanic na sera ya majimbo ni ma rc, dc, ded na watoto wao......

Tunamtaka Tundu Lissu sio huyu dikteta na mharibifu wa uchumi wa nchi na watu wake
 
Hivi nyinyi mataga akili zenu za kijani kibichi hazielewi sio ? Jimbo lenye mikoa mitatu Mpaka mitano Lina ukabila gani , nyinyi CCM si ndio mmeleta ukabila kila mkoa na kabila lake ?
 
Kenya enzi ya KANU ilikuwa nchi ya kijinga kwelikweli ila baada ya mabadiliko ya katiba Kenya unaiona sasa ilipo? Yani khaya mazimwi yoooteee yameondoka sisi tumebaki na hili la CCM tumeling'ang'ania.
Ukiongea hivi mbele ya watu wa turkana watakuuwa
 
Hivi mfumo wa Majimbo wa Kanisa Katoliki, Lutherani (kule unaitwa Dayosisi), Moravian, SDA, TAG nk. nao huwa unaua uzalendo wa kiimani miongoni mwa wakristo?
 
Ma

Marekani jimbo.moja ni sawa na Tanzania moja sasa utalinganishaje?
Ulinganisho wa ukubwa sio issue, Logic inabakia pale pale kuwa, nchi inagawanywa katika kanda zenye mifumo ya kujitawala ndani kwa ndani ili kurahisha maendeleo ya watu badala ya kuwa na mtawala mmoja (Rais) mwenye kuamua hadi choo cha kijiji kijengwe wapi na lini.
 
Ukiangalia kwa makini utaona CCM ndio inatengeneza mazingira ya watu kutaka majimbo.

Rais anasema kama huchagui chama chake hakuna maendeleo. Kuna maana gani kwa wakazi wa Mbeya Mjini kulipa kodi zoooote na wasipate maendeleo badala yake zipelekwe kwa wanaompenda Rais na chama chake?

Ni ujinga na dharau kubwa sana kwa viongozikuona kwamba wanawea kupinga jambokubwa kama hili kwa hoja mfu na nyepesi sana. Suala kubwa ambalo watawala waliopo wanafanya ni kuondoa uwajibikaji kwa wapiga kura na kupeleka maamuzi kwa mtu mmoja tu ambaye anaweza kujitoa ubinadamu na kujipachika uungu. Hali hiyo huleta kundidogola watu waliojuu ya sharia, upendeleo, ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi bila kujali matakwa ya wananchi. Hali hiiitaleta mfarakano mgawanyiko na kuondoa Amani ya mnchi
 
sisi chadema imetuacha vibaya hio sera.tumekua kituko huku mtaaan.sitoki nje.sera mbaya
 
Vilaza wa ufipa mnashindwa kabisa kuisoma Tanzania mnabakia kuja na mifano ya China na Marekani😂😂.
Wewe ulitaka tulinganishe na nini??? Endeleeni kupiga kelele tunajua kisu cha Lissu kimegusa mfupa. Ndo mwisho wenu kutapanya hela za kodi za watanzania mtakavyo
 
sisi chadema imetuacha vibaya hio sera.tumekua kituko huku mtaaan.sitoki nje.sera mbaya
Tangu lini umekuwa chadema??? Kati ya Sera Nzuri zinazoleta ufumbuzi wa kudumu wa ubaguzi wa Ccm na matumizi mabaya ya kodi za watanzania ya CCM ni sera ya majimbo. Ndo mana mnaweweseka nayo humu
 
Nimesikia chama kimoja kinazungumzia nchi kuigawa kwenye majimbo ya kiutawala na uendeshaji. Kwangu mimi kwa nchi ambayo imekuwa kwenye utawala wa mikoa kwa miaka zaidi ya 50 na kwa mfumo wa kugawana mapato kupitia serikali kuu na serikali za mitaa kwa baadhi ya mapato haileti mantiki kubadili mfumo kwenda kwenye majimbo ambayo yanaweza kuua utaifa na kuleta mfarakano. Mfumo wa sasa unaondoa u-mimi na maendeleo ya uchumi yanayopishana- Regional economic imbalances - ambao utaacha baadhi ya maeneo kwenye umasikini mkubwa. Baadhi ya athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na:

1. Maeneo yenye raslimali kidogo kuendelea kuwa maskini na maeneo mengine kuwa tajiri na hivyo kuwa na mchango mdogo wa GDP

2. Ajira ndogo kwenye baadhi ya maeneo yenye raslimali chache na hivyo ongezeko la idadi ya watu kwenye maeneo yenye utajiri wa raslimali

3. kila jimbo kuwa na sheria zake za kiutawala, bunge dogo, polisi nk hali inayoweza kujenga mwelekeo wa kujitenga. Rejea matatizo yakujitenga kwa Biafra Nigeria miaka ya nyuma.

4. Nchi zenye majimbo mf Msumbiji hazina hakikisho la maendeleo endelevu kuzidi ambazo hazina utaratibu huo ie Tanzania

5. Mfumo huo utakuwa na gharama kubwa kuuanzisha

Kimsingi hadi sasa mfumo uliopo hauna shida changamoto kubwa ni kuweka mifumo mizuri ya udhibiti matumizi na mapato ya serikali kwa kuyagawa kwa haki ili kila eneo la serikali liweze kunufaika. Na hususani kuimarisha mfumo wa Halmashauri uweze kukabiliana na changamoto za kiuchumi kwa kila eneo. Iwapo kuna changamoto za mgawanyo sawia basi tupitie upya sera na sheria zetu ndani ya mfumo uliopo tuboreshe.

6. Hata hivyo, Kwa maoni yangu badala ya utawala wa majimbo ni afadhali kuweka kanda za kiuzalishaji ili kuchochea uchumi wa kimaeneo kulingana na mazingira ya kiuchumi na uzalishaji kwa kila eneo.

Yaani kuchagua viongozi itaondoaje utaifa au uzalendo. Mbona tuna mikoa !! na majimbo yatakuwa na mikoa mingi sasa itaharibu vipi utaifa. Hii ni kwa wale wasiopenda maendeleo ya wengine tu ndiyo hawataki majimbo. Huu mtindo mwa kujenga barabara kwa mapenzi utaisha maana wenyeji ndiyo watakuwa na uchungu wa sehemu yao
 
Majimbo ni kuigawa nchi kwenye majimbo kadhaa lengo likiwa ni kushusha madaraka kwa wananchi. Wawe na serikali zao ndogo za majimbo.

Ni uchoyo fulani na ubinafsi hata ukipambwa kwa lugha za kisomi.
Kuna majimbo yatakuwa maskini hasa kuna yale wategemea alizeti kama Singida kuna yale wategemea mbao mahindi na maharage kama mkoa wa njombe na Iringa na Ruvuma nk. Pesa hizo haziwezi jenga barabara wala miradi mikubwa lazima watoe kwingine

Kigoma na mawese yatawapeleka wapi watakuwa na umaskini wa kufa mtu

Swala sio tu kujiamulia kwa pesa ipi?

Nenda hata marekani uone majimbo yalivyo kuna yenye umaskini wa kufa mtu hata ukitoka Tanzania ukiambiwa kaishi kule bure utagoma
 
Bila kuficha ukweli, thinking yetu watanzania at large, ni ndogo Sana. Hivi mbona tunaogopa kufikiri na kujaribu Mambo? Hivi hata Kama ni hayo majimbo wanayoyasema Chadema( ambayo Sasa yana mfumo almost wa kile tunachoita kanda Sasa ) ukabila unakujaje hapo? Kwa maana ya Chadema, inclusivity ya watu na makabila yao ni kubwa kuliko ulivyomgawanyo wa mikoa ya Sasa. Hivi tunakwama wapi? Unajua akili inayoleta mabadiliko ni ile inayojaribu Mambo. Mbona tumebweteka tu? Tunaogopa hata kufikiri vitu vipya vinavyoweza kutupeleka mahali bora zaidi. Hivi bado unahitaji nini juu ya mfumo huu ambao upo miaka yote na tuko hapa tu. Better try new things, new ideas, etc. Kutofikiri na kutoishi kwa ubunifu ni Kama kukosa wataaluma( professionals) katika maisha ya kawaida. Wapi mtapata dawa bora ya magonjwa sugu Kama watu hawaendi maabara) wapi kilimo Cha korosho Kita advance Kama hakuna chuo Cha Naliendele utafiti( watu wanaofikiri na kujaribu new methods) za kuongeaza production? Developments of any kind is all about thinking and creativity. People who don't deeply think are non creative. No wonder, we are a status quo kind of a country. We doubt everything, we never try new systems, we fear any move that seems not to be traditional. Infact, we are people who are tradition oriented and so contented with everything, bad or good.
Hii unanikumbusha back in days wakati Baba wa Taifa alivyosema wakati fulani kwenye hotuba yake." You people, think, think, think. Aliendelea " if you don't think you will be conserved like animals.
Lakini pia kumbukeni ubongo unaoshughulishwa nao ni raslimali. Ulinganifu mahali popote haitatokea, manake hata Sasa bado watu wanalalamika baadhi ya mikoa kuwa na maendeleo kuliko mikoa mingine.
Lakini unaonaje watu wenye rasilimali ndogo wakifikiri( wakitumia brain capital ukitaka) watabadilisha maisha yao na kuja na means nyingine kwa ajili ya maendeleo yao.
Tukubaliane ndg zangu, a thinking nation is progressive and non thinking, and superficial thinking nation is automatically retrogressive.
Tusiogope kujaribu Mambo mapya.
 
Ulinganisho wa ukubwa sio issue, Logic inabakia pale pale kuwa, nchi inagawanywa katika kanda zenye mifumo ya kujitawala ndani kwa ndani ili kurahisha maendeleo ya watu badala ya kuwa na mtawala mmoja (Rais) mwenye kuamua hadi choo cha kijiji kijengwe wapi na lini.
Hakuna kitu hapo na hilo ili lianze kusaidia ni baada ya miaka mingi kwa kuwa kitakachoanza ni kuongeza ghalama za serikari badala ya hudum za wananchi.
Najua hilo litakapo washimd mtasingizia kuwa mbona serikali ya CCM imetawla miaka mingi hivyo mnahitaji muda wakati watu wanaumia.
 
Back
Top Bottom