Serekali pigeni marufuku huu wimbo, unaniaribia watoto

Serekali pigeni marufuku huu wimbo, unaniaribia watoto

dr namugari

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2022
Posts
10,466
Reaction score
18,206
Nyimbo sijui Nani kaimba ila Ni nyimbo maarufu Sana tu " huu mwaka eeh "

Nikinukuu baadhi ya verse
" Ukipata jimama likoboee ,likupe pesa utoboe "

Sasa mttoto amekuwa ikiimba Sana hi verse. Na kwa kwa kifupi haina maaadili na nyimbo Ni nzuri ila msatari huu ktk wimbo siyo siyo mzuri.

Haya Ni maneno ya Bab mwenye nyumba akilalamikia wimbo huu kukosa maadili
 
Ni shida sana Jana kuna jirani nilikuta anamchapa mtoto wake ambaye alikuwa anaimba nyimbo ya nasikia nyee.
Hawa basata wameshindwa kazi
 
Mhubiri 1:9 Yaliyokuwako ndio yatakayokuwako,
yaliyotendeka ndio yatakayotendeka;
duniani hakuna jambo jipya.
,
 
Nikisema uhuru wa Tanganyika umezidi mnacheka! Haya oneni sasa!
 
Sasa inashida gan si inawafundisha ujasiriamali
 
na hizi nyimbo zitazidi siku hadi siku kutokana na kukosa chombo cha usimamizi kichochotambua kazi yake
 
Serekali ndio nini mkuu??
Anyway basata ni kikundi ambacho kipo chini ya mamlaka ya shetani, hivyo usione ajabu kuona wasanii wakicheza wakiwa wamevaa chupi / boksa tu, tena usione ajabu wasanii wakiimba lugha za matusi na wakapewa kibali cha kutoa video hiyo, maana haya yote ni mapenzi ya yule mwaribifu.
 
Yaan tuendako ni bora kupata watoto wa kike tuu...nimekaona katoto ka kiume kanacheza wimbo wa Zuchu unaitwaje cjui sasa pale anapoimba miuno sijui vibuno kitoto hata miaka 3 sizan kama kamefikisha...kanakatika haswa
 
Back
Top Bottom