MrKanteChelsea
JF-Expert Member
- May 12, 2019
- 203
- 237
CHANZO Serengeti Media Centre na Antomatv OnlineJeshi la polisi mkoani Mara limekiri kumshikiria Gimusi Murimi 42 mkazi wa wilaya ya Serengeti kwa kumjeruhi mkewe kwa kumuingizia panga sehemu za siri kwa kumtuhumu kuchepuka wakati yeye akiwa hayupo nyumbani.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara RPC Tibishubwamu amesema mtuhumiwa huwa anaishi mkoani Geita mji wa Katoro anakofanya kazi zake kwa mara nyingi huitembela familia, Sasa tarehe 25th mwezi huu alipofika nyumbani kwake akabaini mkewe amekuwa sio mwaminifu kwenye ndoa hiyo amekuwa akichepuka yeye akiwa hayupo na kuanza kumshambulia kwa fimbo na baadae kumwingizia panga sehemu za siri na kumuumiza sana .
Mwathirika wa shambulio yupo hospitali akipatiwa matibabu huku jeshi likimshikiria mtuhumiwa huku uchunguzi ukiendelea
USSR