Serengeti: Tundu Lissu akumbuka shambulio dhidi yake, amtaka Rais mpya na IGP mpya kuwakamata Wahusika

Serengeti: Tundu Lissu akumbuka shambulio dhidi yake, amtaka Rais mpya na IGP mpya kuwakamata Wahusika

Acha roho mbaya mkuu. Kiburi cha uzima na cheo ulichonacho ni kwa neema tu.
Nitakufa kweli lakini kwa namna Lissu anavyompaka Rais samia shombo, sioni haja ya kuwakamata watu hao.

Samia ndiyo alimtembelea hospitali mara 2, akalipa stahiki zake alizodhulumiwa na Magufuli, akamfanya arudi toka ukimbizini. Lakini pamoja nayote hayo Lissu akipanda kwenye majukwaa domo lake ni kumkejeli Rais Samia kwa maneno machafu.

Sioni rofauti ya IQ kati ya Mdude na Lissu. Kuna wakati nasema pengine nafuu Magufuli angemmaliza tu
 
Wawakamate? Thubutu labda uingie mfumo mpya kbs wa utawala!! Nb: Nakuhakikishia fuatilia comments hapa utawagundua wahusika kwa namna moja ama nyingine [emoji116][emoji116][emoji116]
Wewe ni mjinga tu
 
Rais Samia ni mwanasiasa Lissu ni Mwanasiasa pia. Mashambulizi ya kisiasa ni jambo la kawaida.

Mbona mnataka kumdogosha Rais? Kwamba asisemwe? Akisemwa mnadai eti ni mwanamke.

Rais ni Mtu Mkubwa kwenye Nchi anapaswa kujibu hoja zinazoibuliwa upande wa pili.
Wako wa kumsema na tunaelewa lakini siyo Lissu, alipaswa kuwa na chujio ya maneno
 
Mnataka ashukuru nini hata waliotaka kumuua hamuwstafuti wakati uwezo mnao?
Awatafute mwenyewe na awakamate sasa. Huwezi kumsaidia kichaa asiyetambua juhudi zako. Asubiri mpaka CHADEMA itakapo chukua madaraka
 
View attachment 2742023

Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi kwenye mkutano Mkubwa wa hadhara , Makamu Mwenyekiti wa Chadema , amesema kwamba , Tangu aliposhambuliwa kwa Risasi hakuna yeyote aliyekamatwa wala hakuna uchunguzi uliofanyika hadi sasa .

Amedai kwamba hapo awali , alidhani haukufanyika uchunguzi kwa vile aliyewatuma wauaji wakati huo alikuwa Rais , kwahiyo ingekuwa vigumu kujikamata na kwamba IGP wa wakati huo alikuwa Sirro , lakini sasa Rais ni Samia na IGP ni Wambura .

Tundu Lissu ameendelea kuhoji kwamba , Sasa kama viongozi wale wa zamani wamebadilika na wale wabaya wameondoka , hawa wema akiwemo tunayesema NANI KAMA MAMA , Mbona wahalifu hawa hawakamatwi ?

Ujumbe wake huu hapa

View attachment 2742019
Rekebisha heading!!

Lissu anawezaje kukumbuka mauwaji dhidi yake?

Alikufa na akafufuka?
 
Hivi Rais Samia anaanzaje kuanza kuwakamata waliomshambilia Lissu mwaka 2017 kwa namna anavyomtukana majukwaani.

Hili jitu kweli likishambuliwa na watu wa Magufuli lakini halina shukrani. Wachana nalo
Bandari isitutenganishe pesa huisha lakini Tanzania itabaki vile vile
 
Kwani kuna ugumu gani ?
Kamanda nguli wa ufipa nadhan unatambua vzr tu kua.. jambo hawawez chunguza wala kukamata wahusika! Au mnataka mletewe wahusika raia wa Cambodia?👇👇👇 Ishi humo!!
 

Attachments

  • - KumbukiziMTAFUTANO.jpg
    - KumbukiziMTAFUTANO.jpg
    68.9 KB · Views: 2
Rekebisha heading!!

Lissu anawezaje kukumbuka mauwaji dhidi yake?

Alikufa na akafufuka?
Heading iko sawa mipango ya yule dhalimu mwendazake ilikuwa ni kumuua na kumzika kijijini kwake Ikungi. Ila kwa mapenzi ya Mungu alinusurika
 
Kama anathibitisha aliewatuma wauaji kafa, watamkamata nani sasa? Yeye akitaka aseme aliyewatuma kafa, ila waliotumwa wapo ambao ni fulani na fulani. Wakishaitwa nao watasema kama walitumwa kweli au hapana.
Nukuu (comment #2): "Wawakamate? Thubutu labda uingie mfumo mpya kbs wa utawala!! Nb: Nakuhakikishia fuatilia comments hapa utawagundua wahusika kwa namna moja ama nyingine 👇👇👇"
 
Mtuhumiwa kafa Sasa hapo Kuna kesi gani? Maana ndio anawajua aliowatuma
Nukuu (comment #2): "Wawakamate? Thubutu labda uingie mfumo mpya kbs wa utawala!! Nb: Nakuhakikishia fuatilia comments hapa utawagundua wahusika kwa namna moja ama nyingine 👇👇👇"
Quote Reply
 
Nimeshangaa sana mtu anakumbukaje mauaji yake wakati anakuwa ameshakufa
 
Back
Top Bottom