Serikal itenge budget ya trillion 2 na zaidi kwa ajili ya kununua squatter mfano Manzese, Kigogo n.k ili kuziboresha

Serikal itenge budget ya trillion 2 na zaidi kwa ajili ya kununua squatter mfano Manzese, Kigogo n.k ili kuziboresha

Tatizo lako ni kuwa haujui kujenga hoja. Haujatoa mfano wowote wa Beijing kuhusu mipango miji. Kusema kuwa walivunja nyumba haitoshi.
Ulichofanya ni kuleta picha za CBD ya Beijing kana vile ni mfano wa kuigwa.

Shida ya " wasomi" kama wewe ni kutegemea copy and paste. Master plan sio picha za majengo na mitaa. Nyinyi mnapenda kuwadanganya watu kwa kuwapa majibu mepesi kwenye maswali magumu. Wakati wenzetu wanajikita katika kutumia Masterplan kuboresha maisha ya wasio na uwezo, wewe unakuja na jibu jepesi la tununue nyumba zao na kuzivunja. Mnapoulizwa nini itakuwa hatma ya wapangaji mnakuja na jibu jepesi kuwa watajijua!

Meya wa New York amejipatia sifa kwa kuwa na mikakati ya kuboresha maisha ya wakazi wa jiji lake. Mojawapo wa vitu vya kwanza kufanya ni kuja na mkakati wa kuwa na sehemu za kujisaidia za public zinazofikika kwa urahisi. Ana hakikisha mashimo ya barabarani yanazibwa. Ana hakikisha kuwa anawapa unafuu wapangaji wa nyumba wenye kipato cha chini na kuwabana wanaomiliki nyumba wahakikishe zina hali nzuri.

Ukienda Ulaya wanazungumzia namna ya kufanya huduma zote zinafikika kwa urahisi na kwa usalama. Wanazungumzia watawalindaje wanaotembea kwa miguu na wanaopanda baiskeli.

Haya ndio mambo ambayo yanatakiwa yawe kipaumbele na sio hizi hadithi za Ali Nacha kuwa mbinguni ni Dubai na Beijing.

Hauwezi kuwa na mji bora bila kuhakisha kuwa wale wanyonge katika jamii nao wana nafasi katika jiji lao.

Amandla...
Sasa kuna miji bora na ya kisasa kama ya china
Kuna nchi inafikia china kwa highway na subway za train za umeme duniani
Kuna mambo mengi sana hujui
 
Dhati inatakiwa iendane na kujua ukubwa wa tatizo na kujipanga vizuri. Hauwezi kutatua matatizo kwa wanasiasa kuwaambia watu waje na mawazo kwa malipo ya shilingi milioni 10.

Amandla...
Heading inasema kuwekwe budget na hakuna sehemu kumetajwa million 10 ila umeamua tu kuichomekea kama kawaida yako
 
Ndio maana zimetajwa Trillions kama fidia na miundombinu.
Dhamira ya mabadiliko haipaswi kuambatana na dhuruma. Mbali na yote hayo, NI JAMBO LINALOWEZEKANA, LIKO NDANI YA BAJETI YETU.
Tatizo la afrika kila ukitaka kufanya jambo wataibuka watu ambao watatengeneza mazingira lionekane ligumu na haliwezekani kama huyo anaitwa fundi

Ukweli ni kwamba serikali zetu watu weusi hawana dhamira ya kweli ya mipango miji wameshakubaliana hali iendelee hivi hivi kama ilivyo
 
Fidia kwa mwenye nyumba itamsaidiaje mpangaji? Na hata kwa wenye nyumba, wengi wao hazitawasaidia kitu.

Kariakoo , Msasani na maeneo mengi watu walilipwa pesa ambazo walidhani ni nyingi lakini wengi waliishia kuamini kuwa ni za majini maana hazikuwasaidia kitu.

Kulikuwa na Tanzania Housing Bank ambayo ilikuwa inawakopesha watu ili wajijengee makazi nafuu lakini nayo ikafilisika bila mafanikio yeyote.

Hiyo bajeti ya kutoa matrilioni kila mwaka ni ya nchi gani? Nchi ambayo miaka 65 baada ya uhuru imeshindwa kujenga waste treatment plant Dar es Salaam na kuishia ku pump kinyesi kibichi baharini? Nchi ambayo kuhudumia oxidation pond ni mtihani.

Kuweni realistic.

Amandla...
Ndio maana zimetajwa Trillions kama fidia na miundombinu.
Dhamira ya mabadiliko haipaswi kuambatana na dhuruma. Mbali na yote hayo, NI JAMBO LINALOWEZEKANA, LIKO NDANI YA BAJETI YETU.
 
Sasa kuna miji bora na ya kisasa kama ya china
Kuna nchi inafikia china kwa highway na subway za train za umeme duniani
Kuna mambo mengi sana hujui
Nachelea kukuita mshamba lakini sinabudi.

Highway zinasaidia nini mjini? Kuna subway isiyotumia treni ya umeme? China ina zaidi ya watu zaidi ya watu bilioni 1.42. Ina miji zaidi ya 18 yenye watu zaidi ya milioni 10. Unadhani hiyo miji itasafirishaje wakazi wake kwa wingi na haraka bila kutumia treni za umeme?

Ni kweli kuwa kuna mambo mengi siyajui lakini kwenye hili najua kuliko wewe.

Amandla...
 
Heading inasema kuwekwe budget na hakuna sehemu kumetajwa million 10 ila umeamua tu kuichomekea kama kawaida yako
Ndio maana nina wasiwasi na ubora wa elimu yako.

Milioni 10 haihusu bandiko lako bali ni kiasi ambacho kiliahidiwa na mwanasiasa mmoja kwa yeyote atakayekuja na dawa ya kutatua tatizo la foleni Dar es Salaam.
Mimi naishia hapa.

Amandla...
 
Nachelea kukuita mshamba lakini sinabudi.

Highway zinasaidia nini mjini? Kuna subway isiyotumia treni ya umeme? China ina zaidi ya watu zaidi ya watu bilioni 1.42. Ina miji zaidi ya 18 yenye watu zaidi ya milioni 10. Unadhani hiyo miji itasafirishaje wakazi wake kwa wingi na haraka bila kutumia treni za umeme?

Ni kweli kuwa kuna mambo mengi siyajui lakini kwenye hili najua kuliko wewe.

Amandla...
Kwamba highway hazina msaada mjini
Kwamba ile highway ya kuanzia kimara mwisho mpaka kibaha haina msaada kwamba serikali inapokuwa bize kutanua barabara ni wajinga aisee hizi akili sijui ni za wapi
 
Fidia kwa mwenye nyumba itamsaidiaje mpangaji? Na hata kwa wenye nyumba, wengi wao hazitawasaidia kitu.

Kariakoo , Msasani na maeneo mengi watu walilipwa pesa ambazo walidhani ni nyingi lakini wengi waliishia kuamini kuwa ni za majini maana hazikuwasaidia kitu.

Kulikuwa na Tanzania Housing Bank ambayo ilikuwa inawakopesha watu ili wajijengee makazi nafuu lakini nayo ikafilisika bila mafanikio yeyote.

Hiyo bajeti ya kutoa matrilioni kila mwaka ni ya nchi gani? Nchi ambayo miaka 65 baada ya uhuru imeshindwa kujenga waste treatment plant Dar es Salaam na kuishia ku pump kinyesi kibichi baharini? Nchi ambayo kuhudumia oxidation pond ni mtihani.

Kuweni realistic.

Amandla...
Hiyo inchi ina bajeti ya safari mabilioni, bajeti ya warsha na semina unnecessary mabilioni, ina tuhuma za ubadhilifu Kila mwaka mabilioni, inatoa misamaha ya kodi kiholela mabilioni, inaruhusu wizi wa rasilimali zenye mabilioni ya thamani, inaunda tume na Kamati mchongo za mibilioni, inatenga mabilioni kunyamazisha raia wake, achilia mbali utauari wa raia wake arambee moja tu imekusanya mabilioni.
Makusanyo kwa mwezi ni Tri. 3, kwa mwaka ni zaidi ya 35 T, katika ukusanyaji hapo Rushwa inaacha nje zaidi ya 20% ya kilichoaswa kukusanywa, wakati huohuo ufisadi unachota zaidi ya 20% ya kilichokusanywa. Kilichobaki finyu ndio ukionacho kwenye miradi ya Maendeleo, vipi kama tu na tungeziba mianya yote hiyo? Je, tungeshindwa kuokoa Trillion 2 tu kwa mwaka? Yaani billion 200 tu kwa mwezi?
 
Kwamba highway hazina msaada mjini
Kwamba ile highway ya kuanzia kimara mwisho mpaka kibaha haina msaada kwamba serikali inapokuwa bize kutanua barabara ni wajinga aisee hizi akili sijui ni za wapi
Highways mara nyingi zinaunganisha miji na sehemu za za nje ya miji kama ambavyo hiyo inayounganisha Kimara mwisho na Kibaha.

Hapo zamani zilijengwa kama ring roads ili kuepusha kuzipitisha katikati ya miji. Athari kubwa ya highway ni kelele za magari, uchafuzi wa hali ya hewa na upasuaji wa miji ( ni vigumu watu wasiotumia magari kuzivuka) na uvunjaji wa makazi ya watu.

Ndio maana baadhi ya miji ya Ulaya na Marekani ama inazibadilisha kuwa "boulevards" zinazo accomodate watembea kwa miguu, baiskeli,trams, bustani pamoja na magari. Barabara pana zilizojengwa na Haussmann jijini Paris zilijengwa kama boulevards na sio highways.

Miji mingine imeamua kuzipitisha chini ya ardhi ili zisiathiri miji iliyopo. Miji mingine imeondoa vyanzo vya heavy traffic ya magari makubwa kama bandari kutoka katikati ya mji na kuzipeleka pembezoni ya miji. Aidha, ujenzi wa highway umeathiri sana watu wenye kipato cha chini kwa kupunguza thamani ya makazi yao kutokana na noise na air pollution.

Amandla...
 
Hiyo inchi ina bajeti ya safari mabilioni, bajeti ya warsha na semina unnecessary mabilioni, ina tuhuma za ubadhilifu Kila mwaka mabilioni, inatoa misamaha ya kodi kiholela mabilioni, inaruhusu wizi wa rasilimali zenye mabilioni ya thamani, inaunda tume na Kamati mchongo za mibilioni, inatenga mabilioni kunyamazisha raia wake, achilia mbali utauari wa raia wake arambee moja tu imekusanya mabilioni.
Makusanyo kwa mwezi ni Tri. 3, kwa mwaka ni zaidi ya 35 T, katika ukusanyaji hapo Rushwa inaacha nje zaidi ya 20% ya kilichoaswa kukusanywa, wakati huohuo ufisadi unachota zaidi ya 20% ya kilichokusanywa. Kilichobaki finyu ndio ukionacho kwenye miradi ya Maendeleo, vipi kama tu na tungeziba mianya yote hiyo? Je, tungeshindwa kuokoa Trillion 2 tu kwa mwaka? Yaani billion 200 tu kwa mwezi?
Hatuna hizo pesa. Hizo percentages unazotumia ni za kukisia tu. Hii nchi ni maskini ya kutupwa.

Amandla...
 
Kwamba hatuwezi ku-save wala kuokoa billion 200 kwa mwezi? Huijui nchi hii hakika.
Ku save kwenye kitu gani? Kutumia billion 200 kwa mwezi ili kununua nyumba Manzese hakuna tofauti na kuwanunulia wakuu wa wilaya mashangingi. Mtu hau save kwa kuacha kula.

Amandla...
 
Pesa za safari trillion 1 zipo ila za mipango miji hazipo
Kwa hiyo unataka kutapanya trillion moja kwa zoezi kichaa? Hizo hizo unazosema za mipango miji zitatumiwa na wajanja kununulia ma Bentley na kusafiria.

Ukitaka kujua nchi yako, ulizia hela za fidia za walioathirika na ujenzi wa mwendo kasi zililiwa na nani? Itakuwa hivyo hivyo kwa hilo pendekezo lenu. Watakaofaidi ni slumlords, watendaji serikalini na consultants.

Mtu anayekuambia higway hazina faida kesho amekuwa kiongozi si hasara kwa nchi
 
Mambo mazuri yanagharama tatizo letu waafrika na watanzania tunataka mambo mazuri ila hatutaki kuingia gharama

Changamoto ya Tanzania tunataka kuboresha maeneo ya makazi ya watu kupitia waekezaji kitu ambacho sio sahii sababu nguvu ya waekezaji sio kubwa kihivyo lazima mipango miji na maboresho ya makazi ya watu yawe reflected kwenye budget
👇👇👇👇👇
Kama serikali inaweza tenga trillion 1 za safari basi trillion 2 zipo ndani ya uwezo wetu kwa mapato hayahaya kama tukiamua

Kwenye huu uzi tutumie dsm kama case study maeneo yafuatayo
Serikali itakua inanunua haya maeneo kwa awamu na sio mara moja
  • Manzese
  • Tandale
  • Kigogo
  • Magomen
  • Kigogo
  • Kinondon
  • Mwananyamala
  • Mabibo
  • Ubungo
  • Sinza
  • Buguruni
  • Vingunguti
  • Keko
  • Kurasin
  • Mchikichini nyuma ya soko la karume

Hayo maeneo yanaharibu sana mandhari ya mji ni squatter kuondoa hizi squatter na kujenga upya inawezekana ila kuna gharama kama nchi lazima tuingie

Kwenye kila budget tutenge sh trillion 2 na zaidi hii ni kwa ajili ya
  1. kuwalipa watu fidia wanayoishi kwenye hayo maeneo
  2. Kujenga miundombinu mipya kama ya sewage, fiber, maji, barabara ambazo zitakuwa na sehemu za pedestrian

Baada ya hapa wanapewa makampuni kujenga na sio watu binafsi sababu ukiwapa watu binafsi wajenge hawataweza kufuata standard ambazo tumejiwekea na tutajikuta tumerudi kulekule

Makampuni binafsi watafanya yafuatayo
  1. Watajenga urban corridor barabara ya morogoro, kigogo, tandale na kinondon
  2. Watajenga park nyingi tu za kisasa
  3. Watajenga nyumba za watu wa hali ya chini bei yake isizidi million 20
  4. Watajenga nyumba za middle class
  5. Watajenga nyumba za watu wa hali ya juu
Nyumba zikamilika zitauzwa kwa cash au mkopo (mortgage) na nyumba za hali ya chini bei yake isizidi million 20

Na mfumo huu utafanyika mbeya, mwanza, dodoma, arusha yaani nchi nzima

Tukiweza kutenga sh trillion 2+ na baadae itaongezeka zaidi ya trillion 20 basi kwa mda wa miaka 20 ijayo sehemu kubwa sana ya nchi kutakuwa kumepangiliwa vizuri na kupendeza

Hii ndo njia waliyotumia china kuifanya nchi yao kuwa nzuri mfano ukiangalia beijing ya miaka 1950 ilikuwa ni squatter na mji ulikuwa mbaya sana ila ukiangalia beijing ya leo imejengwa sana

NA HAYO MAENEO YAOTESHWE MITI WAKATI WA MCHANA UTAFIKIRI UPO NDANI YA OVEN
Sijaona
Gongolamboto

Kwanini?
Au kijana unaishi maeneo hayo.
 
Back
Top Bottom