Serikal itenge budget ya trillion 2 na zaidi kwa ajili ya kununua squatter mfano Manzese, Kigogo n.k ili kuziboresha

Serikal itenge budget ya trillion 2 na zaidi kwa ajili ya kununua squatter mfano Manzese, Kigogo n.k ili kuziboresha

Leo na kesho mtu kama huyu anakua kiongozi ni hasara kwa taifa na maumivu kwa wananchi
Nyinyi ndio mnatia hasara nchi hii kwa miradi isiyo na kichwa wala mbele. "Wasomi" kama nyinyi ndio mliotufijisha hapa. Mna tumiq maneno msio yajua kutudanganya kuwa mnajua mnachosema.

Mimi sina elimu, nina uzoefu. Na huo uongozi siwezi kupewa. Mtapewa watu kama nyinyi ambao mmenda shule lakini hamjaelimika.

Amandla...
 
Mtu anayekuambia higway hazina faida kesho amekuwa kiongozi si hasara kwa nchi
Sijasema hazina faida. Nimesema hazichangii ubora wa miji. Ndio maana watu wanaojielewa hawajisifu kuwa miji yao ina highway na flyover. Miji inayosifiwa kama Copenhagen, Vienna , Vancouver n.k. inasifiwa kwa maisha bora ya wakazi wake na sio hizo highways. Hakuna hata mji mmoja wa China ambao upo katika kumi bora za the most livable cities in the world.

Miji inayojitambua inawekeza katika ujenzi wa njia za baiskeli, bustani za umma, shule bora, upatikanaji wa maji safi, treatment ya maji taka na sio upuuzi wa kujipendekeza kwa wenye nazo.

Amandla...
 
Waingereza walipokuwa wanaendeleza jiji la Dar es Salaam kutoka pale alipoacha mjerumani waliongozwa na dira ya " Garden City" yaani jiji la bustani. Ndio maana sehemu zao za makazi zilikuwa na green areas nyingi. Oysterbay na Upanga hayakujengwa maghorofa marefu ya makazi. Apartments blocks zilikuwa hazizidi ghorofa 3, na nyingi zilikuwa na bustani. Mfano wa apartments za wakati ule ni zile za Leaders Club Kinondoni.

Hata baada ya uhuru dhana hiyo iliendelea. Mfano mzuri ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambacho kilikuwa na mapori, bustani, streams ndani yake. Maghorofa ya wanafunzi yalizungukwa na maeneo ya kupumulia.

Sasa hivi, hawa wasomi wetu, wanajaza majengo katika maeneo ya bustani. Wanatoa vibali vya kujenga majengo yenye ghorofa zaidi ya 30 bila kujali mazingira yake.

Hicho ambacho wasomi wetu wanaona kuwa ni maendeleo ni balaa tupu. Proposals kama hizo ziliisha jaribiwa Marekani na Ulaya na sasa hivi wanajuta.

Ila sikio la kufa halisikii dawa. Kwa vile tunaishi katika enzi ya usanii basi proposals kama hizi zitapokelewa vizuri na wana siasa wetu. Tumeisha ona kinachoendelea Sinza.

Amandla...
 
Hatuzungumzii CBD ya mji. Tunazungumzia mahali wanakoishi watu wa kawaida. Usidanganywe na yale majengo ya biashara. Beijing sio mfano mzuri. Mfano bora zaidi ni Singapore. Na hata wao wanajutia walivyo bomoa makazi ya zamani na kujenga maghorofa.
Tunachopaswa kufanya ni kutafuta solution zitakazoendana na uwezo wetu na zitakazo wawezesha wakazi wa Dar es Salaam kuishi maisha yenye staha, afya na usalama. Matokeo ya kukurupuka ndio yametuletea vertical slums za Kariakoo, Upanga na sasa hivi Oysterbay inaelekea huko huko.

Amandla...
Kwanini wajutie kujenga maghorofa?
 
Kwanini wajutie kujenga maghorofa?
Maghorofa yalijengwa kwa ajili ya watu wasio na uwezo mkubwa. Kosa walilofanya ni kuwa waliangalia physical needs peke yake na sio social needs.

Kama sisi tunavyoangalia nyumba za Manzese, tunaangalia ubora wa majengo lakini hatuangalii sehemu yake katika jamii.

Kwa mtazamo wangu watu wanaoishi uswazi wana mshikamano zaidi kuliko wanaoishi katika magorofa ya Upanga.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa Marekani. Magorofa yalivunja mshikamano uliokuwepo awali. Na kwa kukosekana na mshikamano uhalifu ukaongezeka. Watu wakawa wanakabwa kwenye korido na ngazi ( lifti mara nyingi zilikuwa hazifanyi kazi) na drug dealers wakazifanya himaya yao. Umbali wake kutoka sehemu za ajira zilichangia. Baada ya muda wale raia wema wakahamia kwenye suburbs ili kuwakimbia watukutu. Gangs zikatawala.

Baada ya kuelemewa waliamua kuvunja baadhi zake ( Cabrina Green Chicago) na kujenga majengo ambayo yatawawezesha wakazi wake kujenga sense ya community.

Maghorofa yakijengwa kwa umakini yanaweza kuboresha maisha ya wakazi wake. Shida ni kuwa sisi hilo hatulioni. Maghorofa ya NHC ya zamani ni tofauti na haya wanayojenga siku hizi. Sasa hivi NHc wanaondoa zile sehemu za jamii zilizokuwepo na kujenga maghorofa. Inasikitisha sana.

Amandla...
 
Mambo mazuri yanagharama tatizo letu waafrika na watanzania tunataka mambo mazuri ila hatutaki kuingia gharama

Changamoto ya Tanzania tunataka kuboresha maeneo ya makazi ya watu kupitia waekezaji kitu ambacho sio sahii sababu nguvu ya waekezaji sio kubwa kihivyo lazima mipango miji na maboresho ya makazi ya watu yawe reflected kwenye budget
👇👇👇👇👇
Kama serikali inaweza tenga trillion 1 za safari basi trillion 2 zipo ndani ya uwezo wetu kwa mapato hayahaya kama tukiamua

Kwenye huu uzi tutumie dsm kama case study maeneo yafuatayo
Serikali itakua inanunua haya maeneo kwa awamu na sio mara moja
  • Manzese
  • Tandale
  • Kigogo
  • Magomen
  • Kigogo
  • Kinondon
  • Mwananyamala
  • Mabibo
  • Ubungo
  • Sinza
  • Buguruni
  • Vingunguti
  • Keko
  • Kurasin
  • Mchikichini nyuma ya soko la karume

Hayo maeneo yanaharibu sana mandhari ya mji ni squatter kuondoa hizi squatter na kujenga upya inawezekana ila kuna gharama kama nchi lazima tuingie

Kwenye kila budget tutenge sh trillion 2 na zaidi hii ni kwa ajili ya
  1. kuwalipa watu fidia wanayoishi kwenye hayo maeneo
  2. Kujenga miundombinu mipya kama ya sewage, fiber, maji, barabara ambazo zitakuwa na sehemu za pedestrian

Baada ya hapa wanapewa makampuni kujenga na sio watu binafsi sababu ukiwapa watu binafsi wajenge hawataweza kufuata standard ambazo tumejiwekea na tutajikuta tumerudi kulekule

Makampuni binafsi watafanya yafuatayo
  1. Watajenga urban corridor barabara ya morogoro, kigogo, tandale na kinondon
  2. Watajenga park nyingi tu za kisasa
  3. Watajenga nyumba za watu wa hali ya chini bei yake isizidi million 20
  4. Watajenga nyumba za middle class
  5. Watajenga nyumba za watu wa hali ya juu
Nyumba zikamilika zitauzwa kwa cash au mkopo (mortgage) na nyumba za hali ya chini bei yake isizidi million 20

Na mfumo huu utafanyika mbeya, mwanza, dodoma, arusha yaani nchi nzima

Tukiweza kutenga sh trillion 2+ na baadae itaongezeka zaidi ya trillion 20 basi kwa mda wa miaka 20 ijayo sehemu kubwa sana ya nchi kutakuwa kumepangiliwa vizuri na kupendeza

Hii ndo njia waliyotumia china kuifanya nchi yao kuwa nzuri mfano ukiangalia beijing ya miaka 1950 ilikuwa ni squatter na mji ulikuwa mbaya sana ila ukiangalia beijing ya leo imejengwa sana

NA HAYO MAENEO YAOTESHWE MITI WAKATI WA MCHANA UTAFIKIRI UPO NDANI YA OVEN
Naamini umelenga Serikali ya North Korea sio Bongo Land, There is a paucity of budget sufficient.
 
Ku save kwenye kitu gani? Kutumia billion 200 kwa mwezi ili kununua nyumba Manzese hakuna tofauti na kuwanunulia wakuu wa wilaya mashangingi. Mtu hau save kwa kuacha kula.

Amandla...
Sasa Kuna shida gani kutoa huduma hiyo kwa raia?
Hivi huoni kweli Fursa zinazoweza kuzaliwa kwenye makazi yaliyopangiliwa? Hujui kuwa hata Uzalishaji Mali unapungua penye mipango miji Duni wakati huo expenditure inakua?
 
Sijasema hazina faida. Nimesema hazichangii ubora wa miji. Ndio maana watu wanaojielewa hawajisifu kuwa miji yao ina highway na flyover. Miji inayosifiwa kama Copenhagen, Vienna , Vancouver n.k. inasifiwa kwa maisha bora ya wakazi wake na sio hizo highways. Hakuna hata mji mmoja wa China ambao upo katika kumi bora za the most livable cities in the world.

Miji inayojitambua inawekeza katika ujenzi wa njia za baiskeli, bustani za umma, shule bora, upatikanaji wa maji safi, treatment ya maji taka na sio upuuzi wa kujipendekeza kwa wenye nazo.

Amandla...
Kutochangia ubora means hazina umuhimu
Kwa hiyo ulitaka ubungo kuwe na barabara mbili

Hiyo vancouver, vienna haifikii ukubwa wa dsm kwa population ya watu million 6

Unavyosema uweke njia za baiskeli, bustan za umma hayo maeneo unayapataje kama sio kuwalipa watu fidia ili uyapate na kumbuka wewe unapinga fidia
 
Kutochangia ubora means hazina umuhimu
Kwa hiyo ulitaka ubungo kuwe na barabara mbili
Highways hazina umuhimu katika kuboresha maisha ya mkazi wa jijini. Umuhimu wake ni kwenye kuunganisha miji.
Hilo la barabara mbili silielewi.
Hiyo vancouver, vienna haifikii ukubwa wa dsm kwa population ya watu million 6
Population za Vancouver Metropolitan area na Vienna ni zaidi ya watu milioni mbili. Shida sio idadi bali ni namna tunavyohudumia waliokuwepo na hao watakaoongezeka.
Unavyosema uweke njia za baiskeli, bustan za umma hayo maeneo unayapataje kama sio kuwalipa watu fidia ili uyapate na kumbuka wewe unapinga fidia
Njia za baiskeli zinakuwa integrated katika hizo zilizopo. Sehemu nyingine barabara zilizopo zina geuzwa kuwa za pedestrians. Kwa sababu hiyo hamna haja ya kulipa fidia. Sehemu za awali za bustani zifufuliwe na kuendelezwa kwa faida ya wananchi. Maeneo kama Biafra zigeuzwe kuwa bustani badala ya kuzifanya show room. Fukwe za baharini ziboreshwe na ziwe public kama sheria zinavyotaka.

Watu wakiwa creative, bustani zinapatikana. Mojawapo ya Bustani zinazopendwa sana New York inaitwa Highline ambapo sehemu reli ilikuwa inapita iligeuzwa kuwa bustani. Hayo majibu ya fukuza, bomoa ni ya watu wasiotaka kufikiri.

Hii ni mara yangu ya mwisho kukujibu. Naona unataka kushinda vita ambayo hata hauna silaha za kukuwezesha kupigana.

Amandla...
 
Highways hazina umuhimu katika kuboresha maisha ya mkazi wa jijini. Umuhimu wake ni kwenye kuunganisha miji.
Hilo la barabara mbili silielewi.

Population za Vancouver Metropolitan area na Vienna ni zaidi ya watu milioni mbili. Shida sio idadi bali ni namna tunavyohudumia waliokuwepo na hao watakaoongezeka.

Njia za baiskeli zinakuwa integrated katika hizo zilizopo. Sehemu nyingine barabara zilizopo zina geuzwa kuwa za pedestrians. Kwa sababu hiyo hamna haja ya kulipa fidia. Sehemu za awali za bustani zifufuliwe na kuendelezwa kwa faida ya wananchi. Maeneo kama Biafra zigeuzwe kuwa bustani badala ya kuzifanya show room. Fukwe za baharini ziboreshwe na ziwe public kama sheria zinavyotaka.

Watu wakiwa creative, bustani zinapatikana. Mojawapo ya Bustani zinazopendwa sana New York inaitwa Highline ambapo sehemu reli ilikuwa inapita iligeuzwa kuwa bustani. Hayo majibu ya fukuza, bomoa ni ya watu wasiotaka kufikiri.

Hii ni mara yangu ya mwisho kukujibu. Naona unataka kushinda vita ambayo hata hauna silaha za kukuwezesha kupigana.

Amandla...
Unafananisha jiji la watu million 2 na watu million 6 serious

Sehemu kama manzese au kigogo unakuaje creative kupata bustani tofauti na kuwalipa watu fidia ili upate eneo

Ebu tuambie hiyo namna ya kuwa creative bila kutumia gharama
 
Mambo mazuri yanagharama tatizo letu waafrika na watanzania tunataka mambo mazuri ila hatutaki kuingia gharama

Changamoto ya Tanzania tunataka kuboresha maeneo ya makazi ya watu kupitia waekezaji kitu ambacho sio sahii sababu nguvu ya waekezaji sio kubwa kihivyo lazima mipango miji na maboresho ya makazi ya watu yawe reflected kwenye budget
👇👇👇👇👇
Kama serikali inaweza tenga trillion 1 za safari basi trillion 2 zipo ndani ya uwezo wetu kwa mapato hayahaya kama tukiamua

Kwenye huu uzi tutumie dsm kama case study maeneo yafuatayo
Serikali itakua inanunua haya maeneo kwa awamu na sio mara moja
  • Manzese
  • Tandale
  • Kigogo
  • Magomen
  • Kigogo
  • Kinondon
  • Mwananyamala
  • Mabibo
  • Ubungo
  • Sinza
  • Buguruni
  • Vingunguti
  • Keko
  • Kurasin
  • Mchikichini nyuma ya soko la karume

Hayo maeneo yanaharibu sana mandhari ya mji ni squatter kuondoa hizi squatter na kujenga upya inawezekana ila kuna gharama kama nchi lazima tuingie

Kwenye kila budget tutenge sh trillion 2 na zaidi hii ni kwa ajili ya
  1. kuwalipa watu fidia wanayoishi kwenye hayo maeneo
  2. Kujenga miundombinu mipya kama ya sewage, fiber, maji, barabara ambazo zitakuwa na sehemu za pedestrian

Baada ya hapa wanapewa makampuni kujenga na sio watu binafsi sababu ukiwapa watu binafsi wajenge hawataweza kufuata standard ambazo tumejiwekea na tutajikuta tumerudi kulekule

Makampuni binafsi watafanya yafuatayo
  1. Watajenga urban corridor barabara ya morogoro, kigogo, tandale na kinondon
  2. Watajenga park nyingi tu za kisasa
  3. Watajenga nyumba za watu wa hali ya chini bei yake isizidi million 20
  4. Watajenga nyumba za middle class
  5. Watajenga nyumba za watu wa hali ya juu
Nyumba zikamilika zitauzwa kwa cash au mkopo (mortgage) na nyumba za hali ya chini bei yake isizidi million 20

Na mfumo huu utafanyika mbeya, mwanza, dodoma, arusha yaani nchi nzima

Tukiweza kutenga sh trillion 2+ na baadae itaongezeka zaidi ya trillion 20 basi kwa mda wa miaka 20 ijayo sehemu kubwa sana ya nchi kutakuwa kumepangiliwa vizuri na kupendeza

Hii ndo njia waliyotumia china kuifanya nchi yao kuwa nzuri mfano ukiangalia beijing ya miaka 1950 ilikuwa ni squatter na mji ulikuwa mbaya sana ila ukiangalia beijing ya leo imejengwa sana

NA HAYO MAENEO YAOTESHWE MITI WAKATI WA MCHANA UTAFIKIRI UPO NDANI YA OVEN
Hoja nzuri...
Hata hivyo serikali ilitakiwa itenge fedha kwanza kuzuia kuzaliwa Manzese,Tandale na Keko mpya katika kila mikoa kwa kuchukua hatua ya kupima ardhi na kugawa viwanja kiutartibu.
Kila wilaya kuna ofisi ya ardhi na watendaji na vifaa vyao,lakini kila katika kila wilaya Tanzania kuna mahali kunajengwa holela. Unaweza kujiuliza,hivi maafisa ardhi kazi yao ni nini hasa endapo wanaajiriwa na kulipwa mishahara.
Unaweza kujiuliza, Serikali inafikiria nini kwa kupuuzia kwake upimaji wa maeneo wakati madhara ya kutofanya hivyo yanajulikana kiuchumi na kiafya.
Wakikamilisha hilo ndipp waje na hiyo ya kupima na kuboresha maeneo yaliyojengwa holela.
 
Ili kuodoa ujenzi holela anayetakiwa kujenga ni kampuni na sio watu binafsi
 
Ili kuodoa ujenzi holela anayetakiwa kujenga ni kampuni na sio watu binafsi
Hata kama anayetakiwa kujenga ni kampuni,lazima ajenge eneo lilofanyiwa planning na serikali.
Hiyo Manzese, Tandale na Keko,chanzo chake ni kutopima maeneo.
Hata kama mjenzi ni mtu binafsi,endapo ujenzi utafanwa katika eneo lililopimwa,ujenzi hauwezi kuwa holela.

Tatizo lilianzia pale wahusika walipoacha kusimamia hata sheria za ujenzi ....,kwa mfano, mtu mwenye nia ya kujenga nyumba,anatakiwa kkwanza kupeleka michoro na ramani ya ujenzi anaotakiwa kufanya katika ofisi ya ardhi ili kuhakikisha kama anajenga katika eneo lililopimwa, kuona kama ramani yake imeandaliwa na msanifu anayestahili na pia endapo mchoro wake unaendana na eneo husika. Sheria haziruhusu huduma za umeme na maji kupelekwa katika nyumba iliyo katika maeneo yasiyopimwa...lakini sasa sheria hiyo haisimamiwi, na hivyo kuwafanya wajenzi holela kupelekewa hizzo huduma. Kama kampuni za maji na umeme zingeshikilia msimamo wa sheria ulivyo,watu nao wangeishinikiza serikali kupima maeneo yao.
 
Back
Top Bottom