watu wa aina yako ni laana kwa taifa. ulichokiandika kila muhitimu anakijua.
uelewa wako duni unakufanya ushindwe kuelewa kuwa mfumo uliopo wa elimu unamuandaa mwanafunzi kuajiriwa,
kama ni kutafuta maisha nje ya ajira hata waajiriwa wanafanya hivyo matokeo yanazidi kuwa si rafiki kwa huyu muhitimu ambaye anakosa msingi wa kumuwezesha kusimama kiuchumi dhidi ya walio kwenye ajira.
mfumo wamegoma kuubadilisha ili umuwezeshe mwanafunzi kuitumikia vyema taaluma yake awapo mtaani, ajira pia wamegoma kutoa.
andiko langu halina sehemu inayoonyesha kuomba ajira mtandaoni, kupitia majibu yako naona wewe uozo mtupu
Mkuu naona kama unamfokea mdau!
Embu twende pole pole sababu tunajadili jambo la muhimu hapa.
Kudai kitu kama haki, ni lazima uwe na kifungu cha sheria unanukuu kusapoti hoja yako.
Kuandika tu bila kunukuu kifungu chochote cha sheria kinachoilazimisha serikali kukupa haki unayoidai, nami nitasema ni malalamiko yasiyo na mashiko.
Uzi wako una point za msingi sana, isipokuwa umeuandika kibaguzi saazingine kwa kujua ama bila kujua.
Ipo hivii: kundi lenu la vijana wa kTz mnaochipuka kila mwaka ambao ndiyo nguvu kazi inayotegemewa ni kubwa sana.
Kuna waliomaliza vyuo na wengine kuishia elimu ya chini ambao sijasikia mahali popote ukiwasemea namna gani serikali imewaandalia kutumia nguvu kazi yao kujiletea maendelea yao na ya nchi kwa ujumla .
Je ni kweli kabisa kila mhitimu sheria inasema aajiriwe na serikali?
Je takwimu ya kila mwaka ya wasomi wanaozalishwa ni kiasi gani, inalingana na soko la ajira?
Je kama soko la ajira likiwa chini na idadi ya wahitimu ipo juu, serikali isitishe kusomesha watoto kwanza hadi waliomaliza masomo wapate ajira?
Je serikali isomeshe watoto kwa idadi ya nafasi za ajira zitakazo kuwepo nk nk?
Je ni nini kifanyike?
Ninajua ukijibu maswali haya, nitapata msingi wa kujadili hoja yako kwa hekima