Waziii mkuu.
Yaani Mimi huwa nashangaa, mtu ana miaka zaidi ya sitini lakini bado yupo ofisi fulani!!! eti yeye ni mzoefu kwahiyo hakuna haja ya replacement, mtu akifikisha miaka sitini Kama ilivyo kwa watumishi wengine basi astaafu apishe wengine.
Kuna lingine unakuta mtu alikuwa mbunge kipindi fulani, baadaye huyohuyo anakuwa DC mahali fulani, akitoka huko utasikia mara RC mahali, haitoshi utasikia balozi mahali fulani, kumbe huyu alipokuwa mbunge alitumikia taifa na kula cake yake kabisa, Basi uDC apewe mwingine.
Mwisho, kuna hili la watu wa ukoo fulani wenyewe ndo viongozi miaka yote, anatoka babu anamwachia mwanae, mwanae naye anamwachia mjukuu wa babu.
Kama taifa lazima tuyaangalie mambo haya, hili taifa ni la watanzania wote.