Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Wana haki ya kulalamika unajua kwanini, psychology ni kitu very strong wala sio jambo la kuli overlook!umenena vyema. Kunawatu sio wahitimu wa vyuo( vya Kati wala vikuu) wapo mtaani maisha yanasonga.
Ila wasomi wetu( wahitimu) wanalalama kila uchwao.
Inawezekana vyeti vyao ni leseni ya kuilaumu Serikali na ambao hawajaenda chuo leseni hiyo hawana ndio maana wamekaa kimya.
Toka umezaliwa ukajitambua unamuona baba anaamka asubuhi anawasha pikipiki au gari anaenda kazini. Au anafatwa na gari kila asubuhi. Ukipeleleza unaambiwa baba yako ni mhasibu anafanya kazi bandarini baba yako ni msomi, ukicheki kwa wajomba system ni hio hio, baba wadogo system ni hio hio.
Mama unayeshinda nae muda mwingi anakwambia ukianza shule usome ili upate ajira nzuri kama kaka yako si unaona anajenga nyumba yake sahizi. Its been a recurring statement for years na kweli unaona kaka na dada zako wamesoma wakamaliza shule wakapata kazi na maisha wana full control mara paap wana magari mara wameoa life linaendelea wana kila wanachokitaka kupitia kazi.
Katika situation kama hii hiki kitu kimejengeka kwenye saikolojia ya mtoto toka mdogo kwamba kumbe the right path ni kusoma kwa bidii! Inafikia wakati mtoto ametimiza wajibu wake vizuri kashakuwa mtu mzima sasa muda wa kupata ajira ili nae aanze kumenye ghafla hajira hazipo? Omba huku na kule hola serikali haitoi ajira.
Hivi unafikiri ni jambo jepesi kumwambia mtu wa hivi ajiajiri? Wengine hata talanta ya kuuza pipi hawana ghafla umwambie eti ajiajiri maanake aanze kuuza ice cream na karanga barabarani kitu ambacho hakikuwahi kupita hata kwa bahati mbaya kichwani mwake? Hii ni kansa ambayo matibabu yake ukifosi kuiunguza umeua mgonjwa straight away!
Mtu kasoma ili afanye kazi ofisini hati ghafla ajiria hamna easily tu mkajiajiri vijana?