Serikali acheni kujifanya hamtuoni wahitimu, tupeni ajira, hali ni mbaya mtaani

Ukija na mawazo kama haya ....utajikuta uko kusikojulikana punde unakula mijeledi....

But this is the way to go. Shida ni na tumfunge kelele.
 
this is the right time to change our future as graduates, if we wait for fate to decide we might find that it is too late to fulfil our dreams, we have a country vast of resources we dont deserve this kind of treatment from the people we have trusted with power.
 
Bora kuwapiga mawe kama ulivyosema...kulalamika tunhaitoshi. Hii mijitu ni mibinafsi haijawahi kutokea. Hapo hapo mtu akistaafu eti anaongezewa muda kwa mkataba!
Mi nilishauri kipindi flani hizi kazi pia ziwe za mkataba sio za kudumu ambapo mtu anajiachia tu kwakuwa anajua ataondoka ofisini akiwa mzee 😅!

Mikataba iwe ya muda mfupi 3-5 yrs kulingana na productivity na malipo yawe mazuri ili watu wakiondoka maofisini wakajiajiri mtaani maana wanaondoka na mitaji mizuri. Kuna watu wengi walipinga sana hili sababu ya kuprotect mkate wao eti ooh ufanisi utakuwa hamna sijui uzoefu utapatikana vipi? Training si zipo ama internsihip programs!

Mishahara iwe standardized tu kuendana na hali ya maisha na iwe flat kulingana na level ya elimu! Degree au zaidi wale 6M, Diploma 3M kila mwezi! Mtu akipiga 3 yrs lazma atakuwa ana pension nzuri tu ya kuendeleza maisha apishe wengine. Sio kumkalisha mtu miaka 60 ofisini kisha hataki kuondoka anaogopa moto wa mtaani😅ila ndio kinara wa kuwaambia watoto wa wenzie wajiajiri wakati yeye kamchomeka mwanae kwenye system.
 
Ukija na mawazo kama haya ....utajikuta uko kusikojulikana punde unakula mijeledi....

But this is the way to go. Shida ni na tumfunge kelele.
Kweli mkuu nchi yetu ngumu sana ila Mungu atasaidia tu
 
Its easy to be patient if your earning something and progressing with life. The issue is time bruh! Time waits for no man.
 
niliwahi pia kugusia hili, nilishambuliwa vikali
 
Kikubwa
1.mitaala ibadilike
2.Muhitimu aweze kukopeshekeka na serikali ,kama unasoma kwa mkopo wa HESLB kwa kati ya 10M-20M lakini ukimaliza na kutaka kuanzisha biashara hata ya 4M huwezi pata mkopo kirahisi
3.Baadhi ya fani zifutwe au zipunguziwe idadi ya wanafunzi mfano waalimu wa sanaa wapo kibao ajira Hamna lakin vyuo vinadahili bado idadi kubwa ya wanafunzi
4.Fani za kilimo na ufugaji ziongezewe nguvu kwa uwekezaji mkubwa ilii zizalishe ajira zaidi kwa fani nyingine .

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Kama si la serikali tozo wanachukua za nini na kodi wanachukua za nini? Hizi serikali zetu za kiafrika zimedumaza watu wengi sana aisee!

Fuatilia system za nchi zilizoendelea halafu uone kama swala la kipato sio ishu!
umenena vyema. Kunawatu sio wahitimu wa vyuo( vya Kati wala vikuu) wapo mtaani maisha yanasonga.
Ila wasomi wetu( wahitimu) wanalalama kila uchwao.
Inawezekana vyeti vyao ni leseni ya kuilaumu Serikali na ambao hawajaenda chuo leseni hiyo hawana ndio maana wamekaa kimya.
 
and thats the very prob which should be put into consideration. time time time
Time ndio kila kitu,

imagine wewe unatakiwa uwe patient toka una 26yrs mpaka unafika 30 yrs holaa wakati madogo kibao wako nyuma wengine wana 23yrs mpaka 25 yrs wanachomoka vyuoni kuna kazi zinataka vijana wa maximum 27yrs wewe ushakuwa obsolette how can you be patient in that situation?

Tunakwenda kwenye zama ambazo itakuwa ukivuka 35yrs huajiriki siku si nyingi. Ila hao viongozi wao washaiba na wana investments kubwa ambazo kupitia tu position zao wana control na sokoni wao ndio wana priorities. Watoto wao hawana shida anachagua kama kazi anachomekwa mahali tu serikalini humo ama biashara aanchiwa investment flani asimamie.
 
Mkuu naona kama unamfokea mdau!

Embu twende pole pole sababu tunajadili jambo la muhimu hapa.

Kudai kitu kama haki, ni lazima uwe na kifungu cha sheria unanukuu kusapoti hoja yako.

Kuandika tu bila kunukuu kifungu chochote cha sheria kinachoilazimisha serikali kukupa haki unayoidai, nami nitasema ni malalamiko yasiyo na mashiko.

Uzi wako una point za msingi sana, isipokuwa umeuandika kibaguzi saazingine kwa kujua ama bila kujua.

Ipo hivii: kundi lenu la vijana wa kTz mnaochipuka kila mwaka ambao ndiyo nguvu kazi inayotegemewa ni kubwa sana.

Kuna waliomaliza vyuo na wengine kuishia elimu ya chini ambao sijasikia mahali popote ukiwasemea namna gani serikali imewaandalia kutumia nguvu kazi yao kujiletea maendelea yao na ya nchi kwa ujumla .

Je ni kweli kabisa kila mhitimu sheria inasema aajiriwe na serikali?

Je takwimu ya kila mwaka ya wasomi wanaozalishwa ni kiasi gani, inalingana na soko la ajira?

Je kama soko la ajira likiwa chini na idadi ya wahitimu ipo juu, serikali isitishe kusomesha watoto kwanza hadi waliomaliza masomo wapate ajira?

Je serikali isomeshe watoto kwa idadi ya nafasi za ajira zitakazo kuwepo nk nk?

Je ni nini kifanyike?

Ninajua ukijibu maswali haya, nitapata msingi wa kujadili hoja yako kwa hekima
 
Waziii mkuu.

Yaani Mimi huwa nashangaa, mtu ana miaka zaidi ya sitini lakini bado yupo ofisi fulani!!! eti yeye ni mzoefu kwahiyo hakuna haja ya replacement, mtu akifikisha miaka sitini Kama ilivyo kwa watumishi wengine basi astaafu apishe wengine.

Kuna lingine unakuta mtu alikuwa mbunge kipindi fulani, baadaye huyohuyo anakuwa DC mahali fulani, akitoka huko utasikia mara RC mahali, haitoshi utasikia balozi mahali fulani, kumbe huyu alipokuwa mbunge alitumikia taifa na kula cake yake kabisa, Basi uDC apewe mwingine.

Mwisho, kuna hili la watu wa ukoo fulani wenyewe ndo viongozi miaka yote, anatoka babu anamwachia mwanae, mwanae naye anamwachia mjukuu wa babu.

Kama taifa lazima tuyaangalie mambo haya, hili taifa ni la watanzania wote.
 
Kwa maisha ya sasa hapa bongo, Ili uwe tajiri inabidi uwe mbele ya muda na ili uwe mbele ya muda inabidi uwe tayari kupita njia za panya ilimradi utoboe...hilo ndio somo wengi tunachelewa kulipata hakuna tena maisha ya mstari ulionyooka eti usome chuo, ufaulu,uajiriwe , upige kazi, upande daraja, ustaafu....hayo maisha hayapo tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…