Serikali acheni kujifanya hamtuoni wahitimu, tupeni ajira, hali ni mbaya mtaani

Wana haki ya kulalamika unajua kwanini, psychology ni kitu very strong wala sio jambo la kuli overlook!

Toka umezaliwa ukajitambua unamuona baba anaamka asubuhi anawasha pikipiki au gari anaenda kazini. Au anafatwa na gari kila asubuhi. Ukipeleleza unaambiwa baba yako ni mhasibu anafanya kazi bandarini baba yako ni msomi, ukicheki kwa wajomba system ni hio hio, baba wadogo system ni hio hio.

Mama unayeshinda nae muda mwingi anakwambia ukianza shule usome ili upate ajira nzuri kama kaka yako si unaona anajenga nyumba yake sahizi. Its been a recurring statement for years na kweli unaona kaka na dada zako wamesoma wakamaliza shule wakapata kazi na maisha wana full control mara paap wana magari mara wameoa life linaendelea wana kila wanachokitaka kupitia kazi.

Katika situation kama hii hiki kitu kimejengeka kwenye saikolojia ya mtoto toka mdogo kwamba kumbe the right path ni kusoma kwa bidii! Inafikia wakati mtoto ametimiza wajibu wake vizuri kashakuwa mtu mzima sasa muda wa kupata ajira ili nae aanze kumenye ghafla hajira hazipo? Omba huku na kule hola serikali haitoi ajira.

Hivi unafikiri ni jambo jepesi kumwambia mtu wa hivi ajiajiri? Wengine hata talanta ya kuuza pipi hawana ghafla umwambie eti ajiajiri maanake aanze kuuza ice cream na karanga barabarani kitu ambacho hakikuwahi kupita hata kwa bahati mbaya kichwani mwake? Hii ni kansa ambayo matibabu yake ukifosi kuiunguza umeua mgonjwa straight away!

Mtu kasoma ili afanye kazi ofisini hati ghafla ajiria hamna easily tu mkajiajiri vijana?
 
Hivi vipengele nilishawahi kutoa muongozo wa katiba uweje miongoni mwa mapendekezo lilikuwa hilo la utaratibu wa kurithishana madaraka.

Maana familia zile zile ndio zinazungukia kwenye system ya nchi. Wazee kwa watoto kama vile watanzania wengine hawana haki. Hili lazma lifanyiwe mabadiliko kisheria.
 
Kweli nafikiria ni kuvaa mabomu tu mzee maana hamna namna! Yani maisha yamekaa kisengelenyuma sana mkuu!

Kuna haja ya ku temper na system maana ukiifata system haikupi matokeo instantly. Get rich or Die Trying ndio falsafa ambayo pengine itatuokoa vijana wa leo.
 
idadi ya wahitimu waliopo mtaani ni kubwa kutokana na hali ya utoaji wa ajira iliyopo tangu mwaka 2015, to make it simple, chukua idadi ya wanao maliza kila mwaka kotoka vyuo vilivyosajiliwa na serikali katika ngazi ya cheti hadi elimu ya juu.

kuhusu sheria inayoitaka serikali kuajiri unaweza kuniambia ni kifungu gani cha sheria kilichotumika kuwaajiri waajiriwa waliopo makazini? ukishapata jibu la hapa utagundua kuwa ni wajibu wa serikali kusimamia raslimali za nchi na kuhakikisha zinawafaidisha wanachi katika nyanja mbali mbali ikiwepo kutoa ajira kwa wale walio na taaluma kama sehemu ya kurudisha kodi iliyokusanywa kwa wananchi.

kuhusu ambao wameishia ngazi za chini, sijawabagu ila ni kwamba katika andiko langu nimekusudia kupaza sauti ya wahitimu, nao wanayo nafasi ya kupaza sauti zao, uzi mmoja hautoshi kuwasemea wadau wote walio waathirika wa elimu

kuhusu kufuta shule, si busara, ila kinachotakiwa ni kubadilisa mfumo wa elimu uliopo ili kumsaidia mwanafunzi aweze kukabiri mazingira kupitia taaluma anayoipata akiwa shule, kwani mfumo uliopo ni wa nadharia kwa asilimia zaidi ya 80 kuliko vitendo hii ni kwa maslahi mapana ya kizazi kilichopo na kijacho ikiwa serikali itaamua kufumbia macho suala la ajira kama ilivyofanya hivi sasa.

sijaweza kutoa takwimu mahususi kwa njia ya namba kwenye swala la idadi ya wahitimu waliopo mtaani lakini kwa faida ya wote kama taifa, unaweza kwenda kwenye mamlaka husika kuomba idadi hiyo ambayo ni kubwa sana, na kuileta hapa na hivyo kusaidia mjadala kuwa na mashiko zaidi.

tulijege taifa pamoja
 
Kujilipua ndio njia iliyobaki, ndio maisha halisi ya soko la kibepari bora ufe katika harakati za kujaribu kujitoa kwenye umasikini vinginevyo tutaishia kupoteza muda na kuwa frustrated na mfumo tulioaminishwa ni sahihi wakati haupo tena...hizo ajira zenyewe zinazoliliwa ni mizinguo unakuta hela unayolipwa inaishia kutumika kama nauli na kununulia maji ili uendelee kupiga kazi, ukipata msala mdogo tu mpaka uanze kukopa na kuchangisha kwa majamaa na rafiki.
 
Serikali gani duniani inaweza kutoa ajira kwa wahitinu wote?,acha ujinga pambana na hali yako

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Mambo yakibadilika inatakiwa mtu ndio abadilike ilikuendana na uhalisia.
Kusubiri mambo yabadilike yarudi kama zamani ama yawekama unavyowaza wewe( fantasy) huko nijitoa kafara bila agano.

Kwa ishu uliyoiweka mezani kwenye hii comment yako ipo sawa kabisa.
Ila ikumbukwe sio kila familia inabahati ama ilibahatika kuwa na mema ya aina hiyo kwa kuwa na ndugu ama wazazi waliopata ajira Serikalini na sehemu zozote zile zenye maana. Tuachane na hii kwa sababu sio moral of the story.
Kitu kikubwa ambacho kinatakiwa kifanyike kwa kijana uyo aliepigwa chuma kizito ni
Kubadilisha paradigm
Inatakiwa abadili mtazamo wake ( maisha, kipato, mafanikio) kutoka kwenye fantasy na kwenda kwenye uhalisi wa wakati ulipo mana mkeka wake ushachanika njia ya kupata ajira yakuridhisha moyo wake ni nyembamba sana.
Muhimu ni kurudi kwenye basics za maisha, yakutafuta mia 2 mia 2.
Muda mwengine kikubwa uhai🤣🤣😂
 
Hii ni sahihi kabisa,ajira ziwe za muda mfupi na zenye ujira mzuri, ili wengine waingie kwenye system nao .Hata bungeni Iwe miaka 5 mtu anaondoka.
 
Hii ni sahihi kabisa,ajira ziwe za muda mfupi na zenye ujira mzuri, ili wengine waingie kwenye system nao .Hata bungeni Iwe miaka 5 mtu anaondoka.
hili linaweza kufanyika kuanzia ajira zijazo (if only zitatolewa) na kuendelea.

watu wanaopinga utasikia wanakuambia eti hakuna nchi iliyoendelea inayofanya hivi, sijui ni nani alitufunga akili na kutuambia kila kinachofanywa na nchi nyingine ni muafaka na kwetu.
 

Kwenye sufuria watakusikia kwa maneno tu kweli mjomba?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…