Serikali: Agosti 23, 2022 ni siku ya mapumziko

Serikali: Agosti 23, 2022 ni siku ya mapumziko

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameridhia Agosti 23, 2022 kuwa siku ya mapumziko.

Lengo ni kufanikisha zoezi la sensa linalotarajiwa kuanza siku hiyo kwa kuwapokea makarani wa sensa na kutoa maelezo sahihi.

Hivi karibuni Kamisaa wa Sensa 2022, Anne Makinda alinukuliwa akisema Agosti 23, 2022 haitakuwa Siku ya Mapumziko, hivyo kila mmoja ataendelea na shughuli za kimaendeleo.

Pia, soma: Umuhimu wa mapumziko siku ya Sensa
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia Agosti 23, 2022 iwe siku ya mapumziko ili Watanzania wawepo nyumbani kwa ajili ya kuwapokea Makarani wa Sensa na kutoa maelezo sahihi.
 
Vishikwambi Hoyee
Siku Ya Kulala, Kunywa, Hesabu Kuu Sensa
 
Mkae ndani mhesabiwe sasa sio kutembea tembea.
 
Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kwamba siku ya zoezi la sensa ya watu na makazi Agosti 23,2022 ni siku ya mapumziko ili kuwezesha zoezi hili lifanyike vizuri.

Sasa hivi huna tena sababu ya kutoshiriki kwani tarehe 23 ni siku ya mapumziko hivyo ni heri ukabaki nyumbani na kuwapa ushirikiano makarani watakao kuja kuuliza maswali siku hiyo.

Rais Samia amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha analiletea taifa maendeleo, hivyo hatua yake ya kutaka sensa ifanyike amelenga kufahamu idadi ya wananchi wake ili aweke mipango mizuri zaidi na hivyo ni vyema akaungwa mkono.
 
Attachments

  • Faa2829XoAM6Nad.jpg
    Faa2829XoAM6Nad.jpg
    44.5 KB · Views: 6
Shiriki kikamilifu zoezi siku ya sensa kwa maendeleo ya taifa na yako pia. Usijipunje hakikisha unashiriki.
 
... huyu Mh nahisi huwa anapita humu JF; kuna thread inashauri hivyo. Kwa dunia ya leo mitandao ya kijamii haiepukiki; ni platform muhimu ya public kutoa opinions zao inashangaza yule aliyepita na mahafidhina wenzake walitamani ifungiwe! Viva JF.
 
Sihesabiwi me sio ng'ombe
... sensa ya watu ni miongoni mwa mambo ya kale kabisa duniani; sidhani kama wengine toka enzi na enzi hawajawahi kufikiria unachofikiria wewe. Hakikisha unahesabiwa.
 
Yule kamisaa alisema haitakuwa siku ya mapumziko, hii nchi hii
Nadhani hakujiridhisha vya kutosha kutoa lile tamko kuwa Siku hiyo isiwe ya Mapumziko na ndio Maana Boss wake kupitia Rais akajiridhisha na kuipitisha iwe siku ya Mapumziko
 
Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kwamba siku ya zoezi la sensa ya watu na makazi Agosti 23,2022 ni siku ya mapumziko ili kuwezesha zoezi hili lifanyike vizuri.

Sasa hivi huna tena sababu ya kutoshiriki kwani tarehe 23 ni siku ya mapumziko hivyo ni heri ukabaki nyumbani na kuwapa ushirikiano makarani watakao kuja kuuliza maswali siku hiyo.

Rais Samia amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha analiletea taifa maendeleo, hivyo hatua yake ya kutaka sensa ifanyike amelenga kufahamu idadi ya wananchi wake ili aweke mipango mizuri zaidi na hivyo ni vyema akaungwa mkono.
 
Attachments

  • Faa2829XoAM6Nad.jpg
    Faa2829XoAM6Nad.jpg
    44.5 KB · Views: 4
Back
Top Bottom