Serikali: Agosti 23, 2022 ni siku ya mapumziko

Serikali: Agosti 23, 2022 ni siku ya mapumziko

Nadhani hakujiridhisha vya kutosha kutoa lile tamko kuwa Siku hiyo isiwe ya Mapumziko na ndio Maana Boss wake kupitia Rais akajiridhisha na kuipitisha iwe siku ya Mapumziko
... lakini pia kwa hadaa za CCM kuna uwezekano ilifanywa hivyo by design; you know why!
 
Mmepata mapumziko sio tena muanze kupuyanga, kaeni mtulie tuwakute nyumbani.
 
Watanikuta lodge room no 5 na beby wangu
Lodge ziruhusiwe kupokea wateja pls
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluh Hassan ameridhia Agosti 23, 2022 kuwa siku ya mapumziko.

Lengo ni kufanikisha zoezi la sensa linalotarajiwa kuanza siku hiyo kwa kuwapokea makarani wa sensa na kutoa maelezo sahihi.

Hivi karibuni Kamisaa wa Sensa 2022, Anne Makinda alinukuliwa akisema Agosti 23, 2022 haitakuwa Siku ya Mapumziko, hivyo kila mmoja ataendelea na shughuli za kimaendeleo.

Pia, soma: Umuhimu wa mapumziko siku ya Sensa
Hili ni zoezi muhimu sana katika kufanikisha maendeleo ya jamii mama watanzania tunajiandaa kuhesabiwa kwa maendeleo ya jamii
 
Back
Top Bottom