Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kwamba siku ya zoezi la sensa ya watu na makazi Agosti 23,2022 ni siku ya mapumziko ili kuwezesha zoezi hili lifanyike vizuri.
Sasa hivi huna tena sababu ya kutoshiriki kwani tarehe 23 ni siku ya mapumziko hivyo ni heri ukabaki nyumbani na kuwapa ushirikiano makarani watakao kuja kuuliza maswali siku hiyo.
Rais Samia amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha analiletea taifa maendeleo, hivyo hatua yake ya kutaka sensa ifanyike amelenga kufahamu idadi ya wananchi wake ili aweke mipango mizuri zaidi na hivyo ni vyema akaungwa mkono.