Serikali: Bei ya Mchele imefikia Tsh. 3,500, Maharage 3,500, Mahindi 1,500 kwa kilo

Wale maharage ni msosi mmoja maharufu uswahilini, ila naona nao unaenda kuonekana ni kitu cha anasa.
Wa uswahili sasa tunatakiwa tule mihogo, wali na maharage watakula wenye pesa.
 
Karibuni katika Kilimo enyi Wakazi wa mijini. Hivi sasa kilimo kinalipa
 
Sasa wewe ndo kichekesho kwa kuchagua kazi ambayo haiwezi kumudu kipato Cha kukulisha
 
Tafuta pesa mkuu chakula hata kikiuzwa 10000 kwa kilo huwezi lalamika
 
Sasa wewe ndo kichekesho kwa kuchagua kazi ambayo haiwezi kumudu kipato Cha kukulisha
Nilishakuja kukulia kwako kwamba Nina njaa ya chakula

kwa hiyo bidhaa zipande Bei tukae kimya ili tusionekane hatuna shida akili ya wapi hii ndo maana ccm watatawala mda mrefu sana kwa akili kama hizi
 
Ya ya ya ya ya ya ya ya ya alisema serikali imekomesha mfumuko wa bei tena wiki hii.Au yeye na huyu wako Babeli wanajenga mnara😳😳😳
 
Wafunge mipaka na iundwe sheria ngumu atakayekamatwa akisafirisha nafaka nje apigwe kesi ya uhujumu uchumi
kupungua uzalishaji ni sababu ambayo si halisi bali ni kwa sababu mama aliruhusu mazao yaende nje ya nchi hivyo kusababisha nakisi ya bidhaa hizo.ukienda mpaka wa mutukula,holili,namanga nk utashuhudia ni kiasi gani cha malori yanayosafirisha chakula na nafaka kwenda nje ya mipaka yetu.kwa mantiki hiyo bei ya mazao itapanda zaidi ya hivyo ilivyo kwa sasa.
 
Kalime ilinuuze buku jero,kwani kila mtu akiwa mkulima kuna shida gani si unakula mwenyewe Ili uache ulalamishi wa kipuuzi?

Ni hivi ukitaka vya buku jero kalime vinginevyo utaishia kulalama na Wala hakuna kitu kitabadilika..
mgawanyo wa kazi.
 
Ulitaka serikali ikulishe? Unamlalamikia nani bei inapangwa na soko. Pambana mwanaume katafute na shmba ulime hakuna atakayekusaidia huku na serikali haina shamba.
 
Tukiwaonya tukaitwa sukuma gang,

Ngoja sasa mnyooshwe
 
Reactions: nao
Ulitaka serikali ikulishe? Unamlalamikia nani bei inapangwa na soko. Pambana mwanaume katafute na shmba ulime hakuna atakayekusaidia huku na serikali haina shamba.
Acha ujinga bei ikipanda wanaoumia ni wote ndo maana serekali inafanya kila namna kupitia contraction fiscal na monetary policy kushusha Bei inflation ni kitu kibaya kwenye uchumi wa nchi ukienda marekani serekali Yao inapambana kushusha Bei ya vitu ikiwemo ya vyakula

Serekali ya India ilipiga marufuku uuzwaji wa ngano same kwa Indonesia ilipiga marufuku uuzwaji wa palm products

Nyerere alienda kuchukua mahindi ya yanga baada ya watu kukumbwa na bwawa la njaa mwaka 1984 kwa hiyo acha ujinga
 
Wanaonufaika na kupanda kwa bei ya vyakula si wakulima kamwe.
Kuna madalali na wafanyabiashara wa mazao ya chakula ndio wanufaika wakubwa.
Nipo kwenye sekta ya kilimo kwa miongo miwili,najua nini kinafanyika.
 
Kuelekea kiangazi siku zote bei za vyakula inapanda.
Ila tusiwe waongo, mimi nimenunua mchele tena super class pale Kawe , kilo 2,500.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…