#COVID19 Serikali: Chanjo ya Corona iliyoruhusiwa ni kwa wafanyakazi wa Balozi na taasisi za nje, kwa Watanzania bado hatujaamua

#COVID19 Serikali: Chanjo ya Corona iliyoruhusiwa ni kwa wafanyakazi wa Balozi na taasisi za nje, kwa Watanzania bado hatujaamua

Ndio tabu ya kufanya jambo ambalo wewe mwenyewe huna imani nalo unafanya kwa ajiri ya kuwaridhisha wengine.
Kwa hili dunia imegawanyika sipokuwa sisi tusio na mbele wala nyuma. KInachoshangaza China ambako Corona ilianzia hawana mpango na chanjo za ulaya na US. Hata Russia haina mpango na chanjo zao.

Serikali ilete chanjo zote. Binafsi nitaikubali ya China au Russia
 
Hilo nalo tatizo wengine hamuamini chanjo za Ulaya na wengine hawaamini chanjo za China.
 
Taifa la Marekani linatimiza unabii wa siku za mwisho kuhusu ujio wa serikali ya mpinga Kristo likitumia nguvu za kijeshi, kiuchumi, sayansi & teknolojia na ushawishi wake wa kimataifa

UFUNUO 13
15 Mnyama wa pili alipewa uwezo wa kuipa uzima sanamu ya mnyama wa kwanza. Kisha sanamu ikaweza kuongea na kuamuru watu wote ambao hawakukiabudu wauawe.

16 Pia mnyama wa pili aliwaamuru watu wote, wakubwa na wadogo, matajiri na maskini, walio huru au watumwa, wawekewe alama kwenye mikono yao ya kulia au kwenye vipaji vya nyuso zao.

17 Hakuna ambaye angeweza kununua au kuuza bila ya kuwa na alama hii. (Alama hii ni jina la mnyama au namba ya jina lake.)

18 Kila mwenye uelewa anaweza kujua maana ya namba ya mnyama. Hili linahitaji hekima. Namba hii ni namba ya mtu. Nayo ni 666.

Tunaanza na misemo ya uhiari wa kupata chanjo na tena kwa baadhi tu ya watu wanao husika na mambo ya nchi za nje na uhusiano wa kimataifa. Lakini kifuatacho kutakuwa hakuna uhiari tena bali sharti la lazima ili kuweza kuchangamana na kupata huduma zote za kijamii.

Muda wa kutimilika kwa unabii umefika, bado tu tamko litakaloazimiwa na Umoja wa Mataifa. Ndipo kile kilichopo "behind the scene" kwenye "lobbying & advocacy" juu ya chanjo hii itakapo kuja kudhihirika.
 
Ni hiari sasa ukiwa front mfano vyombo ulinzi usalama mipakani waongoza watalii hoteli za kitalii ......wahudumu afya hao ni lazima
Ni hiari sasa ukiwa front mfano vyombo ulinzi usalama mipakani waongoza watalii hoteli za kitalii ......wahudumu afya hao ni lazima
Kwanini kuwalazimisha watu wakati hata waliochanjwa wanaendelea kuugua na kufa.Acheni mambo hayo Mungu atawahukumu vibaya sana,jueni kuwa nyie ni wanadamu tu.
 
Kwanini kuwalazimisha watu wakati hata waliochanjwa wanaendelea kuugua na kufa.Acheni mambo hayo Mungu atawahukumu vibaya sana,jueni kuwa nyie ni wanadamu tu.
Usiogope kivuli halazimishwi mtu ambae hayupo front....kumbuka watalii hawatakuja Taifa linahitaji weka mambo imani na Mungu twende na sayansi kwanza.....Gap dola za utalii tunaliziba vipi ? Advantage majirani watakwala dola zote dunia kijiji tunategemeana sana tutajifungia humu na imani zetu ......haiwezekani wewe mwananchi kawaida hutalazimishwa zile kada za front lazima ....
 
Bila shaka watanzania wanajua uwepo wa covid-19.
Katika kushughulikia issue hii ya Corona, wakati wa JPM tulikuwa na msimamo thabiti kabisa usioyumba hata kidogo.
Lakini baada tu ya kuondokewa na mpendwa wetu JPM, kumekuwa harakati za kila aina katika kushughulikia issue hii ya Corona ikiwa ni pamoja na kuleta chanjo za Corona ambazo JPM alizitilia mashaka wazi wazi.
Kwa sasa tatizo si kukataa au kukubali chanjo, tatizo ni namna chanjo zinavyotaka kuletwa kwa njia za kificho kificho.
Mwenye akili timamu yeyote angetarajia hizo chanjo ziletwe baada ya wahusika kujibu maswali machache yafuatayo:-
(1) Tulizikataa hizo chanjo na sasa tunataka kuzileta, Je,.ni lini tumejiridhisha kwamba hazina madhara kwa watakaotumia?
(2) Kama hazina madhara, kwa nini waliozitumia wanazitilia mashaka na bado wanaendelea kufa?
(3)Je, Corona kwa Nchi yetu ipo kiasi gani na inaathiri kiasi gani mpaka tunaamua kukimbilia chanjo?
(4) Kama kweli hizo chanjo zinasaidia, ni Nchi ngapi zilizotumia chanjo na sasa hakuna corona?
(5) Kama haya maswali bado hayajajibiwa, ni kwa nini tunakimbilia kuleta chanjo?
Naomba wizara ya Afya ijibu kwanza haya maswali, na majibu yawe ni ya kitaalamu zaidi ndipo wafikirie kuleta chanjo.
Mungu tunusuru na giza hili.
 
Mkuu we unakataa chanjo kwa sababu JPM alitilia shaka akazikataa au kwa sababu zina madhara? Wewe kama wewe I mean
 
Mkuu we unakataa chanjo kwa sababu JPM alitilia shaka akazikataa au kwa sababu zina madhara? Wewe kama wewe I mean
Issue siyo JPM alikataa, ninachopinga mimi kama mimi na kukimbilia chanjo kabla ya kujibu hadharani maswali yangu hapo juu.
Mfano mdogo tu ni kama vile, India wanatengeneza hizo chanjo, lakini kwa sasa ndio walioathiriwa zaidi.
Mfano mwingine ni kwamba, wakati wa msiba wa JPM, kulikuwa na umati wa watu usio na mfano. Hakuna hata mtu mmoja aliyevaa barakoa siku zile. Kama kweli Corona ingekuwa tishio kiasi hicho, ni Watanzania wangapi wangekuwa wamefariki mpaka sasa tangu msiba ulipotokea?
 
Chanjo ni hiari kwa wananchi kawaida wale front officewanakutana wGeni watalii vuombo ulinzi usalama afya ni lazima
 
Kufuatia kamati ya wataalam kutoa maoni yao juu ya mustakabli wa Tanzania kuhusu chanjo ya corona, Mh Rais ameruhusu kuingizwa kwa chanjo hizo kwa nchi za nje ambao wana watumishi wao hapa Tanzania. Huo ni mwanzo wa kuingizwa matumizi yake nchini. Nini Maoni yako kama mwananch, je upo tayari kuchanjwa endapo serikali itaidhinisha matimizi ya chanjo hizo.
 
Ni suala la muda tu .....tujiandae kudungwa tu hamna namna dunia kijiji...
Chanjo ni hiari ili maadam hauna mpango Wa kwenda kwenye nchi za watu!! Wakifanya lazimu itawalazimu waniue kwanza ndio wauchanje mwili wangu!
 
Waanze kuchanjwa WABUNGE
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji125][emoji125][emoji125]
 
Chanjo ni hiari ili maadam hauna mpango Wa kwenda kwenye nchi za watu!! Wakifanya lazimu itawalazimu waniue kwanza ndio wauchanje mwili wangu!
Vipi pepo punda ndui na chanjo za chini miaka 5 uludungwa zote? Conspiracy theory zao mvona toka 1800?
 
Chanjo ni hiari ili maadam hauna mpango Wa kwenda kwenye nchi za watu!! Wakifanya lazimu itawalazimu waniue kwanza ndio wauchanje mwili wangu!
Hawakulazimishi......mazingira ndio yatakulazimisha
 
Naishauri serikali iwapime kwa kile kipimo kipya cha kichina wale wote wanaotaka kuchanjwa ili kusiwe na ucheleweshaji wa majibu ya vipimo.
 
Back
Top Bottom