Mkuu acha chuki binafsi.
Kila Rais aliyefanya maendeleo yake kwa muda wake tulishukuru.
Mada sasani daraja la Tanzanite na si kingine chochote kilichoongelewa.
Hela ni za serikali kweli, lakini bila utashi wa viongozi watawala, pesa hizo haziwezi kujenga chochote zaidi ya kuishia mifukoni mwa wajanja wachache wenye mamlaka na
sisi raia hatuwezi kusema chochote.
Tukichongoroa midomo yetu kusema tuhuma yoyote tutaambiwa: "mwenye ushahidi apeleke mahakamani".
Sasa utaweza kutunishiana nao misuli?
Kutokana na serikali nyingi za Afrika zinavyotawaliwa kifisadi, sisi kwetu Rais yeyote anayeonesha njia na kuleta maendeleo ingawa kwa pesa zetu wenyewe sisi walipa kodi, huwa tunashukuru na kusema "ahsante".
Kwanini?
Kwa sababu pesa zetu zikitafunwa kifisadi na matumizi ya anasa yasiyokuwa ya maendeleo, hatuwezi kufanya chochote lile.