Serikali: Daraja la Tanzanite kuanza kutumika Feb 1, magari kupita bure

Serikali: Daraja la Tanzanite kuanza kutumika Feb 1, magari kupita bure

Kwani alitoa hela yake mfukoni au ni hizi hizi kodi za watanzania!! Wapongezwe watanzania kwa kuchangia maendeleo ya nchi yao!! Hongereni sana Watanzania, keep it up!!
 
Baada ya millardayo na Msigwa na mitandao mbalimbali kupost kukamilika daraja za surrender 100% ya comment zinampongeza kumlilia na kumkumbuka Mwana mwema wa Afrika mkombozi wa kweli aliyepata kuishi R.I.P J.P.M
Acha upotoshaji basi! Mnaompongeza na kumlilia ni nyinyi mnaotumia hilo daraja. Kwa sisi ambao tuko Mikoani, hilo daraja lina tija gani?
 
Baada ya millardayo na Msigwa na mitandao mbalimbali kupost kukamilika daraja za surrender 100% ya comment zinampongeza kumlilia na kumkumbuka Mwana mwema wa Afrika mkombozi wa kweli aliyepata kuishi R.I.P J.P.M

Basi Mimi sio Mtanzania, maana 100% ya wa Tanzania ningekuwepo!
 
Ndio plans zililizopo hizo mkuu...

Bado: Kamata, Tabata, Fire, Mwenge, Morocco, Magomeni Mapipa/Usalama

Tayari: Ubungo, Tazara

Zinazoendelea: Chang'ombe, Uhasibu
Watujazie na sisi huku njia panda ya Area C, Wajenzi na Daraja la bahiroad
 
Vilivyobakia kumalizwa sasa hivi vinadema dema. Kuisha haviishi.

Sasa hivi tuna kazi ya kukopa lakini kinachofanyiwa mikopo hiyo hatukioni, baraka ya makongamano ya kusifiana na kuvalishana uchifu hewa.
Kasi imepungua sana...hadi wakenya wanatucheka saizi wakati enzi za magu Pichu zilikua zinawabana.
 
Serikali kupitia kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Mbarawa leo Jan. 30 imetangaza kukamilika kwa 100% kwa daraja la Tanzanite lililojengwa juu ya bahari kutoka Aga khan hadi Oysterbay Jijini Dar Es Salaam na sasa magari yataanza kupita bure kuanzia Feb. Mosi mwaka huu.
Sisi wa Busisi tunaanza lini kuvuka
 
Sasa mbona alisema wagogo wanaonewa sana ikiwemo yeye...
Wanaonewa vipi mkuu. Mfano mdogo tu wakudhihirisha hawaonewi ,Wamejengewa shule na mabweni ya free ,wana madarasa yenye vifaa vyote bado Limzazi linamshawishi mtoto ajifelishe akawe boi wa wengine au akaolewe na mijitu ya look inafurahia kwa kikopo kimojja cha ulanzi bila kujali mateso ya maisha yooote ya mtoto.
 
.
FEVxAyHX0AMo2D5.jpg
 
Daraja lillilopo kwa matajiri kupita bure ila lile la hoehae kigamboni unalipia.
Acheni kulialia. Kigamboni bridge limejengwa na nssf kutumia michango ya wafanayakazi, lazima michango hio irudi. Tanzanite limejengwa kwa kodi za watanzania kwanini walipie tena kupita?

Kwanini mnachukia matajiri? Wao hawastahili kutumia Kodi wanazolipa? Halafu kuna mahali masikini amekatazwa kutumia hilo daraja? Kwa akili yako watumiaji Hilo daraja watakuwa wakazi wa Masaki na Oysterbay tu?
 
Back
Top Bottom