Serikali fuatilieni hizi kampuni za kitapeli zinazodai zinakopesha mitandaoni, mama zetu wanalizwa vibaya sana

Serikali fuatilieni hizi kampuni za kitapeli zinazodai zinakopesha mitandaoni, mama zetu wanalizwa vibaya sana

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Hizi kampuni fake zinadai zimesajiliwa na serikali lakini zinafanya kazi ya utapeli, zipo nyingi, cjui tala imarisha maisha. Tulia mikopo online na zingine zinatumia majina ya Jokate Mwegelo na kuna hawa wanatumia matangazo na video za watu mashuhuri kwa kuziedit.

Watanzania wamepigika wanaamini kila kitu ni fursa jambo ambalo sio kweli. Kuna dada anaitwa Lilian jana kashawishiwa na kampuni moja jina ninalo, kwamba aweke kuanzio cha milion 2 apewe mkopo wa milioni kumi kapigwa kapoteza fahamu kwa sababu hiyo pesa na yeye alikopa sehemu. Kwanini polisi mnashindwa kupambana na wizi wa mitandaoni?

Serikali yetu inamifumo yote lakini inaacha makanjanja wanawaliza watu mitaani ,onyo na angalizo hakuna taasisi inaweza kumkopesha mtu online labda songesha ya Vodacom.
 
Back
Top Bottom