Serikali fuatilieni hizi kampuni za kitapeli zinazodai zinakopesha mitandaoni, mama zetu wanalizwa vibaya sana

Wewe utakuwa ndio tala yenyewe hakuna mtu aliweka pesa akapewa mkopo wake ni matapeli huo ni uongo hakika
Hapana mimi siye, ila sikushauli uende huko mkuu..

Kama unataka mkopo watafute Hawa, ingawa wana riba kubwa sana. πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
 
Watu waache tamaa,utapeli upo mpaka kanisani na haya yote ni kutaka mafanikio ya haraka,serikali ifanyeje ikiwa watu wenyewe wana vichwa vigumu,mara pakua mkwanja,mara vuka na chako yaani ilimradi tafrani,
Eti unaweka kianzio tena 2M ndo upate mkopo serious?mnailaumu bure serikali

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Serikali iache ku deal na Tundu Lissu huko Loliondo ikusaidie vimikopo vidogo dogo vya biashara ya vitumbua?
Hizo mirofinance inatoa mikopo midogo, mikopo ya kuzungumzia ni ile ya MABENKI kamili , tena kuanzia milioni 50 kuendelea si mikopo ya kununulia IST.
 
Kwa nini ulikopa umeshindwa kuwalipa ndio unawaita matapeli?ila riba zao ni kaushA damu na wanapiga simu hao na vitisho juu
Je, wako kisheria !!? Kwa maana wana Kibali cha BOT, Leseni ya Biashara toka BRELA, TIN number !!?? Na je Sera yao (Company's Business/Lending Policy) inawaruhusu kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria na taratibu !!!??? Kama sivyo kuna tatizo mahali na ukitapeliwa kwa asilimia kubwa, ni jambo la kujitakia.
 
mimi naona ni ujinga wetu ndiyo kwa kiwango kikubwa unatufanya tutapeliwe.

Kabla ya kupewa mkopo hebu jaribu kuuliza kwanza, ni bora ulipe japo vishilingi vidogo ili mwanasheria aupitie na akupe fikra zaidi.

Lakini wewe ukiambiwa utapewa mkopo ulipe kwa miaka 10 unaona siyo shida matokeo yake unakuja kulalama humu ambapo hatuwezi kutoa msaada wo wote.
 
Kukopa kwa ujumla ni janga kwa kweli. Ni muhimu kuyaelewa masharti ya mikopo unapotaka kukopa. Mikopo huwa hailengi kumsaidia anayekopa, bali ni kutatua tatizo aliyonayo kwa kipindi hicho na kuongezea matatizo mengine mbele ya safari. Nidhamu ni kuchukua mkopo pale ambapo it's a matter of life and death. Na ujue kwamba utasumbuka sana kuurudisha mkopo
 
TALA TANZANIA = Nadaiwa 500000/-
Mtandao X = Nadaiwa 780000/-
😊😊😊😊😊😊
Unawezaje kukukopa hadi kufikisha kiwango hicho?
Ninavyojua wanakutegeshea ahadi za kukopa kiwango kikubwa lakini ukitaka kiwango hicho wanakupatia pesa ndogo sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…