Serikali fungeni shule na vyuo kuokoa maisha

Tunakimbizana? Kwani watu walikua hawafi?matajiri nyie njaaa kibao na wezi tu tena mkadandia corona ili muweze kula vizuri mikopo ya mabeberu.......bora masikini anaejielewa kuliko tajiri wa kuungaunga
 
Tatizo ni jiwe ambalo halioni, kusikia, kunusa, wala ku-test chochote.
Jiwe anahusikaje sasa jamani yani tamko la jiwe ndio litakimbiza corona au mi naona bora mambo yabaki hivi hivi akitoa tamko atazua taaruki ambayo haitasaidia chochote zaidi zaidi watu watakua wanaanguka hovyo kwa hofu. Hofu ni ugonjwa mbaya kuliko corona itakua chaos
 
Jela haitoshi kufunga shule, wacha wasome , wasomi ni wengi mtaani, lazima tutafanya replacement
 
Haya yote hayasaidii kwani nchi za wenzetu hawakufanya haya??? Korona imepungua??? Tuache kutishana bure kama ni kufa utakufa tu sio kwa korona hata malaria yatakuua tu! Tuache kujitoa ufahamu
Tuko vizuri au nasema uongo ndugu zanguuuuu
 
Tanzania ni Taifa mahili,lenye viongozi intelligent na genius,viongozi makini na wasio waoga.hata Babu yenu Kenyatta Ana appreciate Hilo.Tanzania sio manyumbu like Kenyans,ambao wazungu wakisema Jambo hakuna anayethubutu ku argue.kamwe hatuwez kufunga shule kwa vimafua hivi.Na siku zote ukiwa very intelligent tegemea maadui wengi,iko hivo ,thus why mabeberu wanatusakama weee,bt still we are so tough.Uliza SADEC,watakwambia how Tanzania tough is.
 
Lockdown is not practical.

Kwanini wazee ndo wasijifungie na kuacha watoto na vijana waendelee na shughuli zao.
 
Utakuwa imetumwa na makaburu wewe siyo bure!! Usilikuze tatizo kuliko lilivyo!!
 
nashauri tahadhari iongezwe mashuleni kuwalinda wanafunzi wetu.
wizara ya elimu ifuatilie maelekezo ya wizara ya elimu kama yanazingatiwa na kama hakuna tishio lolote la afya kwa wanafunzi wetu haswa watoto wa shule za misingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni dikiteta asiye na faida. Yaani unazuia wangu wasipate fresh air oksijeni ya Mungu. Kisa unauza barakoa?. To prevent me get fresh by mask your need to have heart of satan and devil
 
Wewe ni dikiteta asiye na faida. Yaani unazuia wangu wasipate fresh air oksijeni ya Mungu. Kisa unauza barakoa?. To prevent me get fresh by mask your need to have heart of satan and devil
You are very ignorant.
 
Imeshachelewa dawa sasa ni chanjo tu
 
Dunia nzima watu wanafungua mashule sababu wameona hakuna chochote kilichoabdirika kwa kufunga shule wewe unakuja tena hapa unasema wafunge?
Hata hao waliokuwa wanalockdown wameanza kuzifungua wenyewe japo bado Wana maambukizi mapya Killa siku! wameamua kufanya lockdown ya kichina!! Eti lockdown ya kuanzia saa tatu za usiku mpaka saa kumi za alfajiri kana kwamba kukicha corona inalala!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…