Serikali fungeni shule na vyuo kuokoa maisha

Serikali fungeni shule na vyuo kuokoa maisha

Ni upambuvu kufunga shule na vyuo kwa Sababu ya vijimafua visivyoweza kuua hata kifaranga cha kuku!!
 
Tunazidi kupoteza nguvu kazi ya taifa! Hii siyo habari njema hata kidogo! Wizara ya afya, funga shule na vyuo. Watoto na vijana wanapata sana covid lakini, haina madhara makubwa kwao!

Covid haina madhara makubwa kwa vijana na watoto, wanaugua na kupona tena bila dawa za maana. Tatizo ni kuwa, wanaambukizana na kuileta majumbani na kuwaambukiza wazazi na watu wenye umri mkubwa nyumbani.

Hii ndo balaa! Kama tutaweza kudhibi maambukizi kwa watoto na vijana, tutakuwa tumefanikiwa sana kuokoa maisha ya watu wazima wanaojikinga katika familia. Shule na vyuo wafunge mwezi mmoja tu, maambukizi yatapungua.
acha ujingasababu ya kufunga ni nn.tanzania ipo salama.ndo nchi pekee Africa na duniani kote yenye usalama kwa sasa.
 
Unazungumzia wizara ya afya ipi hiyo? Tanzania imejaa wapumbavu ndiyo maana Taifa limefika hapa lilipo sasa hivi,ina maana huna habari kuwa Tanzania inaongozwa na mtu mmoja? Yaani unahitaji kuwa na PhD kujua kuwa wizara zote Tanzania zinaongozwa na mtu mmoja?
Hawataki kuhimiza watu wavae barakoa wanawe mikono kwa bidii wamekalia kutegea wafe kwa wingi wapate fedha tokea WHO
 
Kufikiri kufunga shule na vyuo kwa ugonjwa ambao hujui hatima yake ni ufinyu wa kufikiri. Wewe una kazi nzuri na una uhakika na kesho yako jua kwamba hizo ni ajira za watu!

Kuna watu wanalisha familia zao kwa hizo ajira, toka corona ilivyoanza mwaka 2019 decemba duniani kote, mpaka leo nchi zilizofunga shule na vyuo Hawajui nini hatima yake, kwa hiyo wewe endelea kujikinga kivyako sio kuhamasisha wenzako wapoteze ajira.
Mbona shule zilipofungwa kwa mara ya kwanza hawakupoteza ajila? Zifungwe hata week mbili kupisha Elimu ya usafi tahadhari ipite sawasawa kisha zifunguliwe
 
1. Waanze kutangaza cases daily na wapi zimepatikana. Wataalamu wa kupambana na magonjwa ya milipuko wapewe confidence na uhuru wa kufanya kazi zao bila kusubiri ruhusa kutoka kwa wanasiasa

2. Weka bylaws kila mtu avae barakoa kwenye public. Mkaidi akamatwe na kulipa faini

3. Wageni kutoka nje wote waje na negative certificate za COVID with immediate effect. Ambae hana arudishwe na ndege aliyokuja nayo

4. Wafanyakazi waanze kuingia ofisini kwa shift na wengine wafanyie home ili kupunguza mikusanyiko. Hakuna haja ya kujazana ofisini

5. Public transport zianze kubeba watu nusu ya uwezo wake

6. Funga clubs kwa mwezi mmoja

Kuna mengi ya kufanya ila kiburi cha Magufuli ni tatizo. Sasa katwaliwa Eng. Kijazi. Who next?
Huko kote walipofanya hayo ,hawajafa saaana kivile na sasa hivi hawana corona kabisa....
 
Huko kote walipofanya hayo ,hawajafa saaana kivile na sasa hivi hawana corona kabisa....
Mfumo wa shule za Tanzania ni wa hovyo hususani shule za Serikali ambazo wanafunzi hubanana sana darasani idadi kubwa ya wanafunzi kwenye darasa moja
 
Na mikusanyiko yote isiyo na ulazima ipigwe stop
Huko mitaani stand za mabasi kwenye pool Table kuna mikusanyiko mingi inayoeneza maambukizi hususani wamasai walinzi ambao hulala chini ya miti wakiwa wamerundikana kwa wingi
 
Wanafunzi wangapi wamefariki kwa corona?
Mzee acheni maswali ya kishetani Yaani kila anayekufa wakuletee list nyumbani kwako? Hata maambukizi ya walimu wafanyakazi wa mashule uletewe list hapo nyumbani kwako?
 
Kufikiri kufunga shule na vyuo kwa ugonjwa ambao hujui hatima yake ni ufinyu wa kufikiri. Wewe una kazi nzuri na una uhakika na kesho yako jua kwamba hizo ni ajira za watu!

Kuna watu wanalisha familia zao kwa hizo ajira, toka corona ilivyoanza mwaka 2019 decemba duniani kote, mpaka leo nchi zilizofunga shule na vyuo Hawajui nini hatima yake, kwa hiyo wewe endelea kujikinga kivyako sio kuhamasisha wenzako wapoteze ajira.
Wewe ndio una ufinyu wa akili, yani nyie watanzania dah wacha tu.... shule na zifungwe ili kudhibiti ugonjwa usije ukasambaa sana. lakini hata hivyo wakati nchi zote za africa mashariki zilikuwa za pambana kwa njia moja au nyingine nyie mlikuwa mkitukejeli tu.... watanzania aiseee... wacha tu.... najua sasa mbona nyinyi nchi maskini ingawa mna rasilimali chungu nzima....ni kwa sababu ya upumbavu umekithiri zaidi
 
Mfumo wa shule za Tanzania ni wa hovyo hususani shule za Serikali ambazo wanafunzi hubanana sana darasani idadi kubwa ya wanafunzi kwenye darasa moja
Tulijionea mwaka jana haohao watoto shule zilipofungwa ndo wakawa wanazagaa mitaani kama vile hawana wazazi,,,,,....acha tubet
 
Naona mmegawanyika sana,wengine shule zifungwe wengine zisifungwe, corona ndio atakuwa mwamuzi nyie endelea kubishana
 
Back
Top Bottom