Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Katika haya makanisa ya kilokole unaweza ukacheka sana yale yanayoendelea haswa ifikapo Jumapili. Wale wapambe wa mchungaji wakiliona gari la bei mbaya haraka sana wanawasogeza waumini ili lipite na aliyepo ashuke na aende kukaa katika sehemu maalum.
Kwa mchungaji na wasaidizi wake kuliona gari zuri la kisasa ni ujio wa neema fulani. Bahati mbaya kwa waumini wamekuwa sawa na waliofanywa misukule, hawaelewi kwamba wametekwa akili zao.
Serikali haiumizwi na mateso wanayoyapata wananchi wanaofanyiwa vitendo hivi vya kishenzi kwa kudanganywa wakatoa hicho hicho kidogo wanachokipata kwa taabu?.
Ifike mahali tujipunguzie hii mizigo ya dhambi kwa kutumia jina la Mungu. Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Serikali haiyaoni haya madudu ya wachungaji mpaka wanafikia kujiita kiboko ya wachawi?. Ubinadamu umepotelea wapi yarabi!.
Serikali yetu haina ule uthubutu kama alioufanya Rais Paul Kagame kule Rwanda kiasi cha kufungia makanisa ya kitapeli mengi tu. Siuoni huo uthubutu ikiwa Rais SSH anamtuma mkuu wa mkoa Chalamila kwenda kuchangia masuala ya kanisa.
Wanasiasa wanatembelea ule umaarufu wa wachungaji wakisahau kuwa wanaoumia ni wananchi wa kawaida wenye kupata pesa kwa jasho jingi. Hata kuamua kumfungia huyo kiboko ya wachqwi ni maamuzi ya kinafiki tu, ya kisiasa yasiyotoka mioyoni mwao.
Serikali inafanya lolote lile ili iweze kuendelea kuwa na uhalali wa kuchaguliwa katika miaka ya uchaguzi, baada ya hapo ni mwendo wa kufungia vioo haya mateso ya hao wanaoumizwa na wachungaji matapeli wanaoibuka kama uyoga.
ikifikia Jumapili pale Kawe hapafai kwa foleni na wingi wa waumini wanaotoka kuacha pesa zinazowatajirisha hawa wachungaji. Wao wanateseka na umaskini wao na wachungaji wanaendelea kutajirika kwa ukosefu wa maarifa wa waumini.
Siuoni ujasiri wa Rais Kagame akiwa nao Rais SSH au yoyote yule wa Tanzania. Mungu tunamhitaji siku zote kwa ustawi wa Tanzania lakini tumefungulia sana mlango masuala ya dini kiasi cha matapeli kuendelea kuwaumiza waumini wanyonge waliokata tamaa za kimaisha.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.