Duh!
Kwa kweli leo nimecheka, tena sana! Na hapa kwenye hayo maneno niliyo nyanyua ndipo mbavu zilikaribia kuvunjika kabisa!
Kinacho changia nicheke hivi, ni kukusoma wewe kwenye mada kama hii uliyo ileta leo hapa; tofauti, tena mbali kabisa na zile tulizo zoea kukutana.
Niwe mkweli wa nafsi yangu, ninakubaliana kabisa na maudhui ya mada yako hapa. Lakini, kama ujuavyo, na katika mwelekeo ule ule unao elezwa na mistari niliyo nukuu hapo juu; makanisa haya ni biashara, tena biashara zakulaza akili za watu, na hasa waliochanganyikiwa na hali ngumu za maisha. Husemwa, "Wajinga ndio waliwao",...; na kama ujuavyo kwenye nchi yetu hii, muumini mkubwa wa "ujinga" wa waTanzania ni CCM na serikali yake, ambayo kwa bahati nzuri au mbaya umeikutanisha na washirika wenzake katika kuwalaza akili waTanzania.
Sikuendelea kusoma hayo mengine huko chini, lakini nahisi mwelekeo wake ni huo huo nilio upata tokea huko juu hadi hapo nilipo ishia na kunukuu hayo maneno uliyo andika wewe.
Sijui hili taifa tutaishia wapi, iwapo kila mwenye nafasi anatafuta ku'take advantage' ya hawa maskini; siyo kwa mali tu, bali hadi kwenye fikra!