Serikali haioni huu utapeli wa wachungaji? Au wao ya kwao mazuri hivyo wananchi watajijua wenyewe?

HUYU ALIKUWA ANAPIGWA PINI KALI SANA POO YAKE ILIKUWA NI KUUNGANA NA WATESI
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.

Siwezi kuunga mkono mateso ya wote wanaokosa maarifa. Nitakuwa kwa vitendo sikubaliani na mateso ya Yesu msalabani aliyekufa na kufufuka kwa ajili ya mamilioni ya watu.
 
Serikali hasa ile ya JPM (RIP), iliwapigania sana wanyonge ila haya makanisa wanawaona wanyonge kama "malofa fulani". Hawapeleki fungu lililoshiba kanisani. Naomba serikali iwakalie kooni, TRA wawe mlangoni na kapu lao, jamaa wanachuma sana tena kilaiiiiiiiiiiini!
Mke wa JPM ni sehemu ya haya makanisa hivyo hata yeye aliunga mkono wanachokifanya wachungaji.
 
wajinga ndio waliwao kama ww hujaweza kwenda kwann wao waende kwani hawana akili..... kwahyo mnasubiri raisi aseme hataki makanisa ili mumseme na uislamu wake.... ukiacha hisia ukaangalia uhalisia utajifunza haya mambo mtu halazimishwi ni tamaa zake za mijujiza na mafanikio bila kazi acha waliwe vichwa
Samia anapita mle mle alipopita hayati JPM, alishawahi kusema yeye na hayati ni kitu kimoja.
 
Kagame aliyafunga makanisa 400 baada ya kuwataka wanaoyaendesha kuonyesha vyeti vya theolojia. Wakijipunguza wenyewe na Rwanda ina makanisa machache yamebakia.

Dini ni biashara katika hali ngumu ya kiuchumi ya kidunia ya miaka ya sasa. Wateja ni mamilioni ya watu wanaoishi kwa shida wakitafuta riziki kwa ugumu usioweza kuelezeka.

Tatizo ni maarifa, wengi wetu hatuna hayo maarifa na kibaya zaidi serikali inayoongoza inaendelea kujiweka katika hali ya kuutumia ujinga wa wengi kama mtaji wa wao kuendelea kuwepo madarakani.

Waumini wa Mwamposya kule Moshi walikanyagana wakigombea mafuta yenye upako na watu kadhaa wakafariki dunia, ulisikia kauli yoyote ya maana kutoka seriikalini?. Kwa kanisa la Mwaposya kusababisha mauaji ya raia wasio na hatia alipaswa kushtakiwa kwa Manslaughter lakini serikali ilifumbia macho kwa sababu huyu mchungaji ni sehemu ya wale wanaoiombea serikali katika vipindi mbalimbali.
Unadhani Kagame alikuwa sahihi? Hiyo digrii ya theolojia anatoa nani? Kuna mtaala mmoja kwa madhehebu yote? Serikali inajua mtaala upi unapaswa kutumiwa na madhehebu yote?

Kwanini usiishauri serikali iongeze kiwango cha elimu na ubora wa maisha ili kupunguza ujinga na umaskini ambao unasema ni chanzo cha wahubiri matapeli?
 
Katika haya makanisa ya kilokole unaweza ukacheka sana yale yanayoendelea haswa ifikapo Jumapili. Wale wapambe wa mchungaji wakiliona gari la bei mbaya haraka sana wanawasogeza waumini ili lipite na aliyepo ashuke na aende kukaa katika sehemu maalum.

Kwa mchungaji na wasaidizi wake kuliona gari zuri la kisasa ni ujio wa neema fulani. Bahati mbaya kwa waumini wamekuwa sawa na waliofanywa misukule, hawaelewi kwamba wametekwa akili zao.
Kuna kanisa nimekwenda leo wenye magari wanapewa seats maalumu
 
Mleta mada umewahi kujiuliza idadi ya Watu walikwenda Kwa waganga kutambika Kimya Kimya?
Umewahi jiuliza idadi ya Watu walikwenda Kwa Babu wa Loriondo walikuwa wangapi Miaka hiyo?
Ukiacha idadi ya wanakwenda Kawe Hadi Kuna foleni, vipi calibre zao??
Tunapenda Kumsifu Kagame lakini hatujafanya detailed analysis ya nini hasa kilifanyika Rwanda...Kagame ametembea kwenye Sheria.Bunge lilipitisha Sheria.Majengo ya Ibada yawe na standards,Wachungaji wawe na standards.Period.Kama Jengo halikidhiviwangi fungal.
Issue za Imani siyo vitu rahisi.Wakati mwingine tunatumia mihemko kuwahukumu watu na Serikali.Yule anayewahi spidi Kwa Mchungaji,na anayewahi Kwa wapiga ramli,na anayewahi pub,wote Wana shida zinafanana ila wamechagua Njia tofauti.
 
Katika haya makanisa ya kilokole unaweza ukacheka sana yale yanayoendelea haswa ifikapo Jumapili. Wale wapambe wa mchungaji wakiliona gari la bei mbaya haraka sana wanawasogeza waumini ili lipite na aliyepo ashuke na aende kukaa katika sehemu maalum.

Kwa mchungaji na wasaidizi wake kuliona gari zuri la kisasa ni ujio wa neema fulani. Bahati mbaya kwa waumini wamekuwa sawa na waliofanywa misukule, hawaelewi kwamba wametekwa akili zao.

Serikali haiumizwi na mateso wanayoyapata wananchi wanaofanyiwa vitendo hivi vya kishenzi kwa kudanganywa wakatoa hicho hicho kidogo wanachokipata kwa taabu?.

Ifike mahali tujipunguzie hii mizigo ya dhambi kwa kutumia jina la Mungu. Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Serikali haiyaoni haya madudu ya wachungaji mpaka wanafikia kujiita kiboko ya wachawi?. Ubinadamu umepotelea wapi yarabi!.

Serikali yetu haina ule uthubutu kama alioufanya Rais Paul Kagame kule Rwanda kiasi cha kufungia makanisa ya kitapeli mengi tu. Siuoni huo uthubutu ikiwa Rais SSH anamtuma mkuu wa mkoa Chalamila kwenda kuchangia masuala ya kanisa.

Wanasiasa wanatembelea ule umaarufu wa wachungaji wakisahau kuwa wanaoumia ni wananchi wa kawaida wenye kupata pesa kwa jasho jingi. Hata kuamua kumfungia huyo kiboko ya wachqwi ni maamuzi ya kinafiki tu, ya kisiasa yasiyotoka mioyoni mwao.

Serikali inafanya lolote lile ili iweze kuendelea kuwa na uhalali wa kuchaguliwa katika miaka ya uchaguzi, baada ya hapo ni mwendo wa kufungia vioo haya mateso ya hao wanaoumizwa na wachungaji matapeli wanaoibuka kama uyoga.

ikifikia Jumapili pale Kawe hapafai kwa foleni na wingi wa waumini wanaotoka kuacha pesa zinazowatajirisha hawa wachungaji. Wao wanateseka na umaskini wao na wachungaji wanaendelea kutajirika kwa ukosefu wa maarifa wa waumini.

Siuoni ujasiri wa Rais Kagame akiwa nao Rais SSH au yoyote yule wa Tanzania. Mungu tunamhitaji siku zote kwa ustawi wa Tanzania lakini tumefungulia sana mlango masuala ya dini kiasi cha matapeli kuendelea kuwaumiza waumini wanyonge waliokata tamaa za kimaisha.

Mungu Ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Serikali haina mamlaka ya kuzuia imani ya mtu, ikimzuia imani yake inabidi imtafutie imani mbadala ambayo serikali inaona ndio ya kweli. Kumbuka serikali haina Dini.
 
Mambo ya PK mwachie mwenyewe. Ni kweli Kuna matapeli. Lakini Kushughulikia makanisa Kwa nchi kama TZ inahitaji intelligence ya Hali ya juu sana siyo kukurupuka kama unavydhani Mkuu. Mojawapo ya tatizo la Gen Z Kenya ni mgogoro wa Ruto na hayo unasema makanisa ya kilokole! Tanzania tusifike huko tafadhali.
 
Unadhani Kagame alikuwa sahihi? Hiyo digrii ya theolojia anatoa nani? Kuna mtaala mmoja kwa madhehebu yote? Serikali inajua mtaala upi unapaswa kutumiwa na madhehebu yote?

Kwanini usiishauri serikali iongeze kiwango cha elimu na ubora wa maisha ili kupunguza ujinga na umaskini ambao unasema ni chanzo cha wahubiri matapeli?
Ni kweli cha muhimu ni elimu, tumeichezea sana tangu tupate uhuru. Kila Rais mpya anakuja na sera mpya.

Ndalichako alionekana hafai wakati wa Kikwete alipokuja Magufuli akamuibua tena. Siasa kila mahali bila ya kuangalia madhara na faida zake.

Kagame alikuwa sahihi aliondoa huu ujinga unaojificha katika kivuli cha masuala ya dini. Wanyarwanda wanawekeza akili zao katika kuwa wabunifu na kukwepa kutawaliwa na ujinga mwingi unaozama katika hulka za kilokole.
 
Mambo ya PK mwachie mwenyewe. Ni kweli Kuna matapeli. Lakini Kushughulikia makanisa Kwa nchi kama TZ inahitaji intelligence ya Hali ya juu sana siyo kukurupuka kama unavydhani Mkuu. Mojawapo ya tatizo la Gen Z Kenya ni mgogoro wa Ruto na hayo unasema makanisa ya kilokole! Tanzania tusifike huko tafadhali.
Mgogoro wa Ruto unasababishwa na Kenya kutokuwa na chama chenye muundo halisi wa kisiasa, wana vyama vya maslahi ya kutaka kuingia ikulu na vimeshapoteza ile misingi ya kisiasa.
 
Serikali haina mamlaka ya kuzuia imani ya mtu, ikimzuia imani yake inabidi imtafutie imani mbadala ambayo serikali inaona ndio ya kweli. Kumbuka serikali haina Dini.
Humo humo kwenye imani kunakuwa na kichaka cha kutunza ujinga wa kijamii.

China na India hawaamini uwepo wa Mungu ambaye sisi tunamuamini na wametuacha mbali kimaisha.
 
Mleta mada umewahi kujiuliza idadi ya Watu walikwenda Kwa waganga kutambika Kimya Kimya?
Umewahi jiuliza idadi ya Watu walikwenda Kwa Babu wa Loriondo walikuwa wangapi Miaka hiyo?
Ukiacha idadi ya wanakwenda Kawe Hadi Kuna foleni, vipi calibre zao??
Tunapenda Kumsifu Kagame lakini hatujafanya detailed analysis ya nini hasa kilifanyika Rwanda...Kagame ametembea kwenye Sheria.Bunge lilipitisha Sheria.Majengo ya Ibada yawe na standards,Wachungaji wawe na standards.Period.Kama Jengo halikidhiviwangi fungal.
Issue za Imani siyo vitu rahisi.Wakati mwingine tunatumia mihemko kuwahukumu watu na Serikali.Yule anayewahi spidi Kwa Mchungaji,na anayewahi Kwa wapiga ramli,na anayewahi pub,wote Wana shida zinafanana ila wamechagua Njia tofauti.
Mawazo yako mazuri lakini tunarudi kule kule' ukosefu wa maarifa.
 
Huyu kiboko ya wachawi anaendelea kutoa video zake ambazo zinaudhalilisha utu wa watanzania wengi. Yeye anacheka na marafiki zake lakini hao waumini wake (wajinga) wanaendelea kuishi maisha ya msoto.

Ifike mahali serikali yetu kwa ukubwa wake ionee aibu pale video za kudhalilisha utu wa watanzania zinapoendelea kusambazwa. Dini ni mtaji na ushahidi ni namna huyu mpumbavu kutoka DRC anavyoendelea kuwakashifu watanzania.

Serikali ijipange kikamilifu na sio kuishia kuwatazama wafuasi wa hawa wachungaji kama vile ni kura zao za miaka ya uchaguzi, Hawa wananchi ni zaidi ya hizo kura zao, hao wachungaji wasiogopwe kwa sababu ya ushawishi wao katika miaka ya uchaguzi.

Kuna maisha baada na kabla ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom