Serikali haioni huu utapeli wa wachungaji? Au wao ya kwao mazuri hivyo wananchi watajijua wenyewe?

HUYU ALIKUWA ANAPIGWA PINI KALI SANA POO YAKE ILIKUWA NI KUUNGANA NA WATESI
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.

Siwezi kuunga mkono mateso ya wote wanaokosa maarifa. Nitakuwa kwa vitendo sikubaliani na mateso ya Yesu msalabani aliyekufa na kufufuka kwa ajili ya mamilioni ya watu.
 
Mke wa JPM ni sehemu ya haya makanisa hivyo hata yeye aliunga mkono wanachokifanya wachungaji.
 
Samia anapita mle mle alipopita hayati JPM, alishawahi kusema yeye na hayati ni kitu kimoja.
 
Unadhani Kagame alikuwa sahihi? Hiyo digrii ya theolojia anatoa nani? Kuna mtaala mmoja kwa madhehebu yote? Serikali inajua mtaala upi unapaswa kutumiwa na madhehebu yote?

Kwanini usiishauri serikali iongeze kiwango cha elimu na ubora wa maisha ili kupunguza ujinga na umaskini ambao unasema ni chanzo cha wahubiri matapeli?
 
Kuna kanisa nimekwenda leo wenye magari wanapewa seats maalumu
 
Mleta mada umewahi kujiuliza idadi ya Watu walikwenda Kwa waganga kutambika Kimya Kimya?
Umewahi jiuliza idadi ya Watu walikwenda Kwa Babu wa Loriondo walikuwa wangapi Miaka hiyo?
Ukiacha idadi ya wanakwenda Kawe Hadi Kuna foleni, vipi calibre zao??
Tunapenda Kumsifu Kagame lakini hatujafanya detailed analysis ya nini hasa kilifanyika Rwanda...Kagame ametembea kwenye Sheria.Bunge lilipitisha Sheria.Majengo ya Ibada yawe na standards,Wachungaji wawe na standards.Period.Kama Jengo halikidhiviwangi fungal.
Issue za Imani siyo vitu rahisi.Wakati mwingine tunatumia mihemko kuwahukumu watu na Serikali.Yule anayewahi spidi Kwa Mchungaji,na anayewahi Kwa wapiga ramli,na anayewahi pub,wote Wana shida zinafanana ila wamechagua Njia tofauti.
 
Serikali haina mamlaka ya kuzuia imani ya mtu, ikimzuia imani yake inabidi imtafutie imani mbadala ambayo serikali inaona ndio ya kweli. Kumbuka serikali haina Dini.
 
Mambo ya PK mwachie mwenyewe. Ni kweli Kuna matapeli. Lakini Kushughulikia makanisa Kwa nchi kama TZ inahitaji intelligence ya Hali ya juu sana siyo kukurupuka kama unavydhani Mkuu. Mojawapo ya tatizo la Gen Z Kenya ni mgogoro wa Ruto na hayo unasema makanisa ya kilokole! Tanzania tusifike huko tafadhali.
 
Ni kweli cha muhimu ni elimu, tumeichezea sana tangu tupate uhuru. Kila Rais mpya anakuja na sera mpya.

Ndalichako alionekana hafai wakati wa Kikwete alipokuja Magufuli akamuibua tena. Siasa kila mahali bila ya kuangalia madhara na faida zake.

Kagame alikuwa sahihi aliondoa huu ujinga unaojificha katika kivuli cha masuala ya dini. Wanyarwanda wanawekeza akili zao katika kuwa wabunifu na kukwepa kutawaliwa na ujinga mwingi unaozama katika hulka za kilokole.
 
Mgogoro wa Ruto unasababishwa na Kenya kutokuwa na chama chenye muundo halisi wa kisiasa, wana vyama vya maslahi ya kutaka kuingia ikulu na vimeshapoteza ile misingi ya kisiasa.
 
Serikali haina mamlaka ya kuzuia imani ya mtu, ikimzuia imani yake inabidi imtafutie imani mbadala ambayo serikali inaona ndio ya kweli. Kumbuka serikali haina Dini.
Humo humo kwenye imani kunakuwa na kichaka cha kutunza ujinga wa kijamii.

China na India hawaamini uwepo wa Mungu ambaye sisi tunamuamini na wametuacha mbali kimaisha.
 
Mawazo yako mazuri lakini tunarudi kule kule' ukosefu wa maarifa.
 
Huyu kiboko ya wachawi anaendelea kutoa video zake ambazo zinaudhalilisha utu wa watanzania wengi. Yeye anacheka na marafiki zake lakini hao waumini wake (wajinga) wanaendelea kuishi maisha ya msoto.

Ifike mahali serikali yetu kwa ukubwa wake ionee aibu pale video za kudhalilisha utu wa watanzania zinapoendelea kusambazwa. Dini ni mtaji na ushahidi ni namna huyu mpumbavu kutoka DRC anavyoendelea kuwakashifu watanzania.

Serikali ijipange kikamilifu na sio kuishia kuwatazama wafuasi wa hawa wachungaji kama vile ni kura zao za miaka ya uchaguzi, Hawa wananchi ni zaidi ya hizo kura zao, hao wachungaji wasiogopwe kwa sababu ya ushawishi wao katika miaka ya uchaguzi.

Kuna maisha baada na kabla ya uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…