Serikali iache kunyanyasa watumishi, Mfumo wa PEPMIS hauna uhusiano na mshahara wa Mtumishi alioufanyia kazi mwezi mzima

70% ya vishikwambi vilikwisha kufa miezi miwili tangu wapewe.

Yale madudu ni mabovu hatari. Serikali ilipigwa aisee.
 
Sa mtafanyeje kazi kubembelezana.kama ni mfanyakazi hewa si ujulikane,zilipita tama za kufutwa utumishi na watu maisha yaliendelea,
Kama unaona huwezi jaza tafsir yake ni kuwa kazini kwako huna kazi na haustahili uwepo.
 
Mwezi huu ni kujibebea tu mademu watumishi wa UMMA wasiokamilisha kujaza kwani hawana mshahara, wakulungwa uelekeo ni huko kujilia mbususu kwa ulaini mtendaji wa Kijiji au mwalimu Eliza
 
Tatizo wao wapo maofisin huko wanadgani watumishi wote wanaishi mtumba, hili swala wamelikurupukia sana hawakufabya maandalizi yeyote sasa wafunge msahara wa mtumishi kwa kigezo hicho ndio wanaonesha hilo takwa la sheria analo lisema simbachawene lipo wapi
 
Hawa kwa kukurupuka kila uchwao!
IGA imeishia wapi zaidi ya matatizo matupu!
Ubabaishaji hadi lini jamani viongozi!
 
Ule mfumo naona uko fair ila hauna umuhimu mkubwa kivile kiasi cha kuwataka au kulazimisha watumishi wote wautumie
 
Mimi nilijaza bila kupata maelekezo kutoka kwa mtu yeyote na nilitumia simu tu. Kama kuna mtumishi kashindwa kujaza basi ni mtumishi wa darasa la saba labda
 
Technophobia ni mbaya sana zaidi ya 70% ya watumishi wa umma wanakumbwa na huu ugonjwa. Hawataki teknolojia kila ubunifu wao ni kuupinga tu siyo kwa hoja ila ni kwa hofu. Waziri big up endelea kukaza hapohapo tunahitaji kubadilika
 
Habari Mkuu!
Kabla sijachangia chochote ningependa kufanya Rejea ya Nyaraka zifuatazo.....
(NA NAPENDA KUSEMA NIKO OPEN KWA MJADALA WENYE HOJA)

Rejea KANUNI ZA KUDUMU ZA UTUMISHI WA UMMA 2009 (standing order for Public Services ya mwaka 2009) Kanuni D.42 na pia unaweza ukasoma kuhusu Kanuni za Perfomance appraisal zote Zipo kwenye D.62 Mpaka D.75

Pia SERA YA MENEJIMENTI NA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA Toleo la 2 la September 2008 Sura Ya nne Sera namba 4.16 "Tathmini ya Utendaji kazi" nitakuomba Usome pamoja na KANUNI ZA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI (KANUNI ZA UTENDAJI BORA), ZA MWAKA 2007 Zilizoandaliwa chini ya kifungu cha 99(1) cha SHERIA YA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI, 2004 (Na. 6 YA MWAKA 2004) na TANGAZO LA SERIKALI NA. 42 (Lililochapishwa tarehe 16/2/2007)
Soma kanuni namba 36 na 37..


Haitoshi pia Unaweza ukasoma Kanuni kuhusu Utoaji wa Mishahara Iliyo chini ya Kanuni za Kudumu za utumishi wa umma 2009 (Standing order for Public servants 2009) kanuni namba E.3

Nimesikitika Sana kuona Wewe unayesema unaweza kuwasaidia Watumishi haki zao umeshindwa kujua Vyote unavyosema Vimewekwa chini ya Sheria na Kanuni za Kiutendaji za utumishi na hazipo.kwa bahati mbaya..

Mtumishi anaposhindwa kutimiza wajibu wake kama Mtumishi Sheria na taratibu zimewekwa wazi kuwa Ni lazma apewe maonyo na moja ya maonyo Ukishindwa kutimiza wajibu ni Onyo la kushindwa kupokea Mshahara ambalo lilo chini ya SHERIA YA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI Sheria no 366 kifungu no 26 mpaka 28...

Kanuni zote na sheria zote nilizotaja zinaonyesha umuhimu wa Tathmini ya utendaji wa mtumishi Hivyo mtumishi kushindwa kutoa tathmini ya utendaji kazi wake ni ishara kwamba ameshindwa kufanya kazi au ameshindwa kufanya majukumu yake, Kwa kuhudumia Umma...

Lakini kushawishi watumishi waipinge serikali Itawaponza kwa sababu inaenda kinyume na sheria na KANUNI ZA MAADILI YA UTENDAJI KATIKA UTUMISHI WA UMMA Toleo la mwaka 2023..
Kanuni ya pili


LAkini pia Mtumishi lazma akubali kupimwa utendani kazi wake maana ni wajibu kufanya hivyo sio ombi wala Hiyari
Kanuni hiyo hiyo kanuni ya 1 inamtaka mtumishi kufata taratibu na kufanya wajibu wake

Kama mtumishi ataona Anaonewa au uamuzi wa nyaraka hauko sahihi au Sheria ina unyanyasaji au maagizo yana changamoto au Hakutendewa hali kwa sehemu yoyote KANUNI HIYO YA MAADILI INAMPA UWANJA WA KUAMDIKA BARUA KWA KATIBU MKUU AU MWAJIRI WAKE KUELEZA DUKUDUKU LAKE..
 
Walimu pamoja na kuwa na vishkwambi bado wanashindwa kujisajili kwenye huu mfumo?
Unafahamu idadi ya walimu Tanzania?
Unafahamu idadi ya vishikwambi vilivyogaiwa?
Unafahamu kuna maeneo walimu wanaishi hawana network hadi wasafiri unbali mrefu?

Acha dharau walimu ndio wametufikisha hapa!!
 
Wamejaa ujinga, wangekuwa na akili wangekwenda kufanya tafiti za kina kwenye vijiji vya ndani kabisa
 
Kwani TUCTA wanasemaje? acha wanyanyaswe
 
Hilo ndio tatizo lenu mnao jiona mnajua kufuata sheria kwa upande mmoja na kusahau upande wa pili wa sheria hizo hizo,
majukumu ya mtumishi umma kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma na mkataba wake wa kazi hauna kipengere kinacho fungamanisha matumizi ya mifumo ya kidijitali na Na ujira wa mtumishi husika kwa kazi alizo pangiwa kwa mujibu wa mkataba wake wa kazi.

Ikiwa mtumishi katekeleza wajibu wake ulio andikwa kwenye mkataba wake basi anayo haki ya kulipwa ujira wake kwa kazi hiyo, tambua ujira halipwi kwa kazi ya kujiunga kwenye mfumo bali yale majukumu yake aliyo pangiwa kimkataba

Mfano kama ni daktari kahudumia wagonjwa nabm taarifa za kuhudumia wagonjwa zinatumwa kwa muajiri wake kupitia takwimu za kazi zinazo tumwa kila siku kwa DMO na ametekeleza hilo kwa ufasaha na wakati huo usisahau kwamba majukumu hayo kayatekeleza kwa mkopo mwezi mzima sasa hilo la kusimamisha mshahara lina husiana nini na hilo la mfumo?

Ndio maana serikali hii inashidwa na kugalagazwa vibaya sana kwenye kesi hasa za kimataifa sababu ya wanasheria wake kushindwa kuelewa sheria vizuri na kuzitafsiri.

Lakini hakuna mtumishi anaye kataa kupimwa lakini taratibu za upimaji ziwe rafiki na tambua wakati serikali inaleta huu mfumo haijagawa vitendea kazi ili kufanikisha hilo nikiwa na maana kwamba huwezi kumlazimisha mtumishi kununua simu (smartphone) kwa pesa yake ili wewe umpime kwa mfumo ulio uandaa wewe kwa manufaa yako ,vitendea kazi unatakiwa uvilete wewe unaye taka kumpima na sio kumlazimisha atumie ujira wake kwa kazi aliiyo itumikia kwa manufaa yako.
swali? Jee? Serikali imegawa hivyo vitendea kazi vyenye sifa ya kujiunga na huo mfumo kwa watumishi wake wote? Ili wawe na uhalali wa kusimamisha huo mshahara?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…