Serikali iache kunyanyasa watumishi, Mfumo wa PEPMIS hauna uhusiano na mshahara wa Mtumishi alioufanyia kazi mwezi mzima

Wenye mamlaka wapumbavu sana, fikiria tu mshahara wenyewe mkia wa mbuzi halafu uutumie kuhangaika na huo upumbavu wao, maisha yenyewe gharama juu, wanadhani kila mfanyakazi ana maisha mazuri kama wao, hawajui kuna watu hawana hata 500 ya vocha
Tatizo la utendaji duni wa watumishi wa umma wa nchi hii si mambo ya mifumo hiyo wanayowaza kuitumia kuwabana tatizo ni kwamba serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kuwalipa watumishi stahili zao . Suala la malimbikizo ya mishahara serikali imewekeza sana kwenye propaganda za kusema tunalipa tunalipa ! Wakati ukifika kila mamlaka za serikali za mitaa kuna maelfu ya watumishi hawajui kwa nini hawalipwi na watalipwa lini ni kizungumkuti
 
Hivi wanazuia kweli au 😂
Mimi nilijaribu saa zima na sikuweza
Hapana watatolewa mfano wachache tu!
ila Itabdi Nyie wengine muandike barua kwa Wakurugenzi wenu kutoa sababu kwanini hamjajiunga..
Maana nao wataandika Barua Kwa katibu mkuu-Utumishi Kujieleza kwanini surbonates wao hawajasajili mfumo
 
Serikali ingetumia muda huu kutafakari kwa kina nini kifanyike ili kuachana mfumo wa kikokotoo ambao umewaacha wastaafu hoi licha ya kutumikia nchi hizi kwa uadilifu na uzalendo mkubwa .Mtu anatumikia miaka 30 plus anaambulia pensheni ya mkupuo vihela vichache kama milioni 18.My foot
 
Na kuongezea tu. Hela za bando wamewapa watumishi ..? Swali lingine wakumbusheni kuwa kuna watumishi wamehama kutoka halimashauri moja kwenda nyingine huku mishahara yao haijaweza kuhamishwa mpaka sasa hivi. Hao nao wasipo jisajili kwenye huu mfumo mtawakata mshahara wao. .? Hili taifa linaongozwa na mazwazwaaaaa waropokaji wakurupukaji. Kaeni kwa kutulia na mjitafakari
 
Jambo jipya huwa na changamoto mitazamo tofauti ila baada ya muda tutazoea tuu.
 
Outliers have a special way of dealing with them.
Wahusika/Viongozi watajua Nini chakufanya.
 
Hivi wanazuia kweli au 😂
Mimi nilijaribu saa zima na sikuweza
Wamesharuhusu Mfumo kwa sasa unaweza kujaza majukumu na kuedit progress zako na kuweka majukumu ila Mfumo utakuwa wazi mpaka Ijumaa saa kumi na mbili kujaza majukumu..
Na kama umeshajaz andika progress na Weekly report
 
Lile Lisimbachawene ni punguani snaa ana roho mbaya kama Jobu sijui mijitu ya Dodoma ikoje.

Aliwahi kusema kwamba eti Watumishi wasitumie simu Wakiwa kazini Hadi watoke
 
Watumishi wao wanalia mishahara duni huku gharama za maisha zikiongezeka na kile kikotoo cha kustaafu ni cha kinyonyaji, haya ya mfumo hayana maana kwao.
Serikali ijikite kushughulikia hayo na si kusumbua watumishi na mambo ya mifumo mpaka wakose muda wa kuhudumia wateja wao
 
Lipeni kwanza mishahara ambayo TUCTA wanapendekeza ikiwemo ile nyongeza ya 23%, posho na likizo kwa wakati, rudisheni kikokotoo kilichokuwepo, halafu mje na mifumo.
Ni kweli siyo kwenye nyongeza ya 23percent mnabadili gear angani na utekelezaji wake kuwa 2.3%
 
Inchi imejaa uhuni mwingi sana hii,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…