Serikali iache kunyanyasa watumishi, Mfumo wa PEPMIS hauna uhusiano na mshahara wa Mtumishi alioufanyia kazi mwezi mzima

Daktari unapata wapi muda wa kupiga porojo!? madaktari ni watu ambao wako very strict and are mostly busy na ni nadra kujihusisha na debate ambazo ni nje ya profession yao, kama wewe ni MD ni katika wale incompetent ambao wanategemea kufanya uchawa au kujipendekeza ili wafikie malengo yao.
 
Mkuu Mimi kwa MD nilivuka zamani sana Mimi Ni MMED(Paediatric) with Neonatology Fellowship..(Kama unajua nazungumzia nini Utanielewa)
So kwa Lugha rahisi ni Superspecialist..

Sasa kwanini nazungumzia mfumo na kuujibia hapa kwa sababu sio tu kuufahamu ni jukumu langu kufanya Hivyo..

Kwa Mfumo mimi ni mmoja wa niliojaribu kuusimamia kwa kiasi chake najua udhaifu wake na najua uimira wake..
Kama kuna shida yoyote ya Mfumo nipo kusaidia..

NIna postGraduate Diploma pia kwenye Maswala ya Utawala (Maana naona umeuliza na kunihoji na pia Kusema nafanya vitu nje ya peoffesional yangu)..

Hapana hicho nachokifanya ni ndani ya majukumu yangu..
Nakaribisha kama una swali..
Asante
 
Huu mfumo ni mwepesi sana HAMKUJIPANGA.

Watu waliofanikiwa kuhama taasisi moja kwenda nyingine hamjahamisha mishahara yao .

Watumishi hao wapo taasisi nyingine na supervisor wa hao watumishi wapo taasisi nyingine. HAMKUJIPANGA.
 
Huu mfumo ni mwepesi sana HAMKUJIPANGA.

Watu waliofanikiwa kuhama taasisi moja kwenda nyingine hamjahamisha mishahara yao .

Watumishi hao wapo taasisi nyingine na supervisor wa hao watumishi wapo taasisi nyingine. HAMKUJIPANGA.
Mkuu Mishahara huamishwa na Katibu Mkuu Utumishi baada ya kufungwa kwa Data za Pande zote mbili Ulikotoka na unakoenda..

Waajiri wako wa zamani na mpya lazima wakubaliane kufanya hivyo...

mwajiri wa zamani akikufungia data Atastopisha Code na Subcode (Au kiswahili Kasma)..
Hivyo waajiri wapya wataomba kupewa kasma mpya kwa Check number yako..
So Katibu wa Utumishi ataprovide kama taakavyopokea..

So jaribu kutrace process kama zimefanyika ngazi zote mwajiri wa sasa na mwajiri wa zamani...

kama tayari data zako zimefungwa au bado zipo kwenye Taasisi ya zamani

Shukrani
 
Sio kazi ya mtumishi husika.

Ni jukumu la mwenye kila mamlaka kutimiza wajibu.

Na kwa hakika hujajibu nilichokuuliza, hao maafisa utumishi wa taasisi wana kazi nyingi, katibu mkuu utumishi ana kazi nyingi. Na uhalisia ni kwamba waliohama ni wengi na mishahara yao haijahama kulingana na huo mchakato, kwenye PEPMIS hawa watumishi wapo dilema, otherwise wanajaza details tofauti na utendaji wanaofanya kulingana na mazingira tofauti ya kazi.
 
Wakuu wa idara semina mwezi mzima,watumishi wa chini semina dakika 20 na wengine hata dakika 1 ya semina hawajaipata.
 
Nimekujibu labda kama umechagua kutokubali jibu
 
Mifumo haionani, SIO.

Mfumo wa ess wote upo chini ya UTUMISHI sasa hamjamuwekea kitufe cha muheshimiwa Katibu mkuu kubonyeza ili kuruhusu kuhama kwa taarifa za mtumishi.

Hata huku kwenye salary portal ya kwenye mfumo haifanyi kazi ukiomba salary slip utakaa zaidi ya dakika 20 na hupati.

Huko kwenye uhamisho watu ndio hata kuonana hawaonani, supervisor wenyewe kuona maombi ya watu wao ni kwa taabu mno.

Kwaio pesa za bando la kufanya kazi na kujaza ni hizi hizi za salary ya urefu wa kwamba ?



KIZURI HAKITAKI HARAKA

huu mfumo sio wa kupigiwa chapuo za haraka hivi, mpaka kutishiana kufungiana posho.


Kuna harufu ya UPIGAJI kama sio UJUAJI.
 
Mkuu Uko sawa bado kuna baadhi ya mifumo haisomani na hii ni kutokana na kuwa na Developers tofauti bado serikali inaweka Mazingira sawa iweze kuonana..

Hata kwenye uhamisho kutumia ess...

Nafikiri unafahamu kuwa kuna stage ambayo mkuu wa Tasisi yeye hafanyi aprove kwemye mfumo huo wa ess bali yeye ataidhininusha maombi ya watumishi chini ya mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS)...
("Ambapo taarifa hutumwa huko baada ya mtumishi kukamilisha Approve zote za wahitajika")

ambao humo ndo nilikupa maelezo ambayo nilkuambia kuhusu kufunga data..
Sasa humo kwenye mfumo wa Taarifa za mishahara humo ndo huabdilisha kasima na mengineyo....

Kwahyo baada ya Muombaji wa Uhamisho maombi yake yakipita kote Mkuu wa Taasisi anatakiwa aingie kwenye Mfumo wa HCMIS, Ili abadilishe huko na Utumishi wataona na wataapprove ..

Asante
 
Ngoja Wagome watatuhudumia wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…