Serikali iache kunyanyasa watumishi, Mfumo wa PEPMIS hauna uhusiano na mshahara wa Mtumishi alioufanyia kazi mwezi mzima

Serikali iache kunyanyasa watumishi, Mfumo wa PEPMIS hauna uhusiano na mshahara wa Mtumishi alioufanyia kazi mwezi mzima

Hilo ndio tatizo lenu mnao jiona mnajua kufuata sheria kwa upande mmoja na kusahau upande wa pili wa sheria hizo hizo
Ndo maana nimeweka Hoja mezani Leta Sheria upande wa pili tuzijadili kwa Hoja..

Bila kuonea upande wowote nitafurahi sana tukienda kwa hoja na kisheria..
Karibu

Ila bila kusahau ni kwamba Wote ambao hawatalipwa mshahara sio Waajiriwa peke yao hata waajiri pia ambao wafanyakazi wao Hawapo kwenye mfumo..
Screenshot_20240222_103230.jpg
 
Habari Mkuu!
Kabla sijachangia chochote ningependa kufanya Rejea ya Nyaraka zifuatazo.....
(NA NAPENDA KUSEMA NIKO OPEN KWA MJADALA WENYE HOJA)

Rejea KANUNI ZA KUDUMU ZA UTUMISHI WA UMMA 2009 (standing order for Public Services ya mwaka 2009) Kanuni D.42 na pia unaweza ukasoma kuhusu Kanuni za Perfomance appraisal zote Zipo kwenye D.62 Mpaka D.75

Pia SERA YA MENEJIMENTI NA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA Toleo la 2 la September 2008 Sura Ya nne Sera namba 4.16 "Tathmini ya Utendaji kazi" nitakuomba Usome pamoja na KANUNI ZA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI (KANUNI ZA UTENDAJI BORA), ZA MWAKA 2007 Zilizoandaliwa chini ya kifungu cha 99(1) cha SHERIA YA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI, 2004 (Na. 6 YA MWAKA 2004) na TANGAZO LA SERIKALI NA. 42 (Lililochapishwa tarehe 16/2/2007)
Soma kanuni namba 36 na 37..

Haitoshi pia Unaweza ukasoma Kanuni kuhusu Utoaji wa Mishahara Iliyo chini ya Kanuni za Kudumu za utumishi wa umma 2009 (Standing order for Public servants 2009) kanuni namba E.3

Nimesikitika Sana kuona Wewe unayesema unaweza kuwasaidia Watumishi haki zao umeshindwa kujua Vyote unavyosema Vimewekwa chini ya Sheria na Kanuni za Kiutendaji za utumishi na hazipo.kwa bahati mbaya..

Mtumishi anaposhindwa kutimiza wajibu wake kama Mtumishi Sheria na taratibu zimewekwa wazi kuwa Ni lazma apewe maonyo na moja ya maonyo Ukishindwa kutimiza wajibu ni Onyo la kushindwa kupokea Mshahara ambalo lilo chini ya SHERIA YA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI Sheria no 366 kifungu no 26 mpaka 28...

Kanuni zote na sheria zote nilizotaja zinaonyesha umuhimu wa Tathmini ya utendaji wa mtumishi Hivyo mtumishi kushindwa kutoa tathmini ya utendaji kazi wake ni ishara kwamba ameshindwa kufanya kazi au ameshindwa kufanya majukumu yake, Kwa kuhudumia Umma...

Lakini kushawishi watumishi waipinge serikali Itawaponza kwa sababu inaenda kinyume na sheria na KANUNI ZA MAADILI YA UTENDAJI KATIKA UTUMISHI WA UMMA Toleo la mwaka 2023..
Kanuni ya pili
View attachment 2911917

LAkini pia Mtumishi lazma akubali kupimwa utendani kazi wake maana ni wajibu kufanya hivyo sio ombi wala Hiyari
Kanuni hiyo hiyo kanuni ya 1 inamtaka mtumishi kufata taratibu na kufanya wajibu wake View attachment 2911931

Kama mtumishi ataona Anaonewa au uamuzi wa nyaraka hauko sahihi au Sheria ina unyanyasaji au maagizo yana changamoto au Hakutendewa hali kwa sehemu yoyote KANUNI HIYO YA MAADILI INAMPA UWANJA WA KUAMDIKA BARUA KWA KATIBU MKUU AU MWAJIRI WAKE KUELEZA DUKUDUKU LAKE..
View attachment 2911938
Siasa za hovyo sana hizi utitiri wa kanuni usio leta matokeo.
Ccm imewaharibu sana.

Hizi kanuni zingezingatiwa na Mawaziri, wakurugenzi wa ngazi zote, RCs ,DCs na DAS's wala msingekuwa mnahangaika na walimu.
.kusingekuwa na mfumko wa bei, elimu dhaifu, wizi, usisadi na utawala usiozingatia usawa na sheria. Rushwa na matumizi mabaya ya ofisi visingekuwepo.
 
Ndo maana nimeweka Hoja mezani Leta Sheria upande wa pili tuzijadili kwa Hoja..

Bila kuonea upande wowote nitafurahi sana tukienda kwa hoja na kisheria..
Karibu

Ila bila kusahau ni kwamba Wote ambao hawatalipwa mshahara sio Waajiriwa peke yao hata waajiri pia ambao wafanyakazi wao Hawapo kwenye mfumo..
View attachment 2912013
Hasimamishiwi mtumishi yeyote mshahara kwa ajili ya jambo hilo, february hiyo utarudisha mrejesho hapa.
 
Sa mtafanyeje kazi kubembelezana.kama ni mfanyakazi hewa si ujulikane,zilipita tama za kufutwa utumishi na watu maisha yaliendelea,
Kama unaona huwezi jaza tafsir yake ni kuwa kazini kwako huna kazi na haustahili uwepo.
Hiyo ni kwa mujibu wako wewe mwenye akili ndogo ya uelewa wa mambo, watu hawa lalamikii kujiunga bali wana lalamikia matatizo ya matumizibya huo mfumo ambao haujaandaliwa miundombinu nansi mfumo rafiki kwa mazingira yetu.
 
Hasimamishiwi mtumishi yeyote mshahara kwa ajili ya jambo hilo, february hiyo utarudisha mrejesho hapa.
Haya sawa Mkuu Hili linalotokea Sasa Hivi niliwahi kuwaonya Baadhi ya watumishi waliokuwa wakibeza Mfumo huu kabla hata Tamko la.wizara la kufungia mshahara Ilikuwa January I think..
Tena humu humu Jf kwenye Uzi wa Elli

Ila wengi walikuwa wabishi nasisitiza tena Jamani Jiungeni na PEPMIS na muifanyie kazi pia..
Jambo hili niliwaelekeza sana Atoto na nakumbuka nilikuwa nikmjibu Elli pia..

Kuna wakati tuache ubishi kuna wakati watumishi tunatamani kuwaambia hata vitu Vinavyopikwa Jikoni ila tukiona jnsi mlibyo tunashindwa kuwatonya niliwaambia kabla kuhusu hili swala kwahyo tulieni

Kama mna haraka hivi basi haraka sana

1. Wanunulieni watumishi wote Laptops au Vishikwambi au Simu za Android.

2. Haraka sana wapelekeeni Umeme maeneo yote wanayofanyia kazi

3. Haraka sana wainganishieni kwenye Bando la Bure la Internet la TTCL

4. Haraka sana wapeleekeeni ITs kwenye maeneo yao ya kazi ili wawaunganishe haraka sana kwenye huo mfumo (hasa kwa Watumishi wazee wale darasa la 7)

5. Fanyeni hivyo haraka sana.

Kufurahia mfanyakazi kukosa mshahala ni Roho Mbaya tu.
 
Technophobia ni mbaya sana zaidi ya 70% ya watumishi wa umma wanakumbwa na huu ugonjwa. Hawataki teknolojia kila ubunifu wao ni kuupinga tu siyo kwa hoja ila ni kwa hofu. Waziri big up endelea kukaza hapohapo tunahitaji kubadilika
Hakuna mtumishi anakataa teknolojia swala ni je? Wameandaliwa kutumia hizo teknolojia? Na je? Mazingira waliyopo yanaruhusu na ni rafiki kwa hizo teknolojia?

Unapelekaje mfumo unao hitaj angalau internet speed ya 3G obove ili ufanye kazi kwenye mazingira ambayo hata 2G yenyewe kuipata ni shida? Halafu unatafuta ufanisi kwenye hilo? Hapo ni sahihi ?
 
Haya sawa Mkuu Hili linalotokea Sasa Hivi niliwahi kuwaonya Baadhi ya watumishi waliokuwa wakibeza Mfumo huu kabla hata Tamko la.wizara la kufungia mshahara Ilikuwa January I think..
Tena humu humu Jf kwenye Uzi wa Elli

Ila wengi walikuwa wabishi nasisitiza tena Jamani Jiungeni na PEPMIS na muifanyie kazi pia..
Jambo hili niliwaelekeza sana Atoto na nakumbuka nilikuwa nikmjibu Elli pia..

Kuna wakati tuache ubishi kuna wakati watumishi tunatamani kuwaambia hata vitu Vinavyopikwa Jikoni ila tukiona jnsi mlibyo tunashindwa kuwatonya niliwaambia kabla kuhusu hili swala kwahyo tulieni

Kwani tarehe za mshahar si zinakaribia utaleta mrejesho unless kama wajitoe ufahamu
 
Kama mna haraka hivi basi haraka sana

1. Wanunulieni watumishi wote Laptops au Vishikwambi au Simu za Android.

2. Haraka sana wapelekeeni Umeme maeneo yote wanayofanyia kazi

3. Haraka sana wainganishieni kwenye Bando la Bure la Internet la TTCL

4. Haraka sana wapeleekeeni ITs kwenye maeneo yao ya kazi ili wawaunganishe haraka sana kwenye huo mfumo (hasa kwa Watumishi wazee wale darasa la 7)

5. Fanyeni hivyo haraka sana.
Namshangaa sanab Simbachawene amekuwa hapo tamisemi kwa vipindi mbali mbali kweli hajui mazingira ya watumishi wake wanayo fanyia kazi? Au ndio kulazimisha mambo ili wamdanganye Rais kwamba huo mfumo unafanya kazi vizuri
 
Hakuna mtumishi anakataa teknolojia swala ni je? Wameandaliwa kutumia hizo teknolojia? Na je? Mazingira waliyopo yanaruhusu na ni rafiki kwa hizo teknolojia?

Unapelekaje mfumo unao hitaj angalau internet speed ya 3G obove ili ufanye kazi kwenye mazingira ambayo hata 2G yenyewe kuipata ni shida? Halafu unatafuta ufanisi kwenye hilo? Hapo ni sahihi ?
Vipi kuhusu Mifumo mingine waliyo nayo haifanyi kazi?
Hawatumii simu za mkononi kuingia whatsapp?
Na kufanya matumizi mengine?
 
Nashindwa kuelewa hawa viongozi huwa wana tumia akili gani katika maamuzi yao.

Msidhani kila mtu anaishi mtumba hapo dodoma muwe mnafanya tafiti za kina kabla ya kuleta hiyo mifumo yenu kwanza.

Mfumo wenu unahitaji angalau 3G au H+ Internet speed ili angalau ufanye vizuri wakati huo kuna watumishi wapo vijijini huko ambako hadi leo wanapata internet yenye kasi ya GPRS na EDGE (hilo nina uhakika nalo na ushahidi ninao).

Msitumie ubabe kwenye hili mtatesa watumishi sana, mfumo bado una shida na si rafiki kwa mazingira yetu mnalazimisha nchi kuingia kwenye teknolojia ambazo ki msingi si rafiki kwa kwa aina ya watu na miundo mbinu kifupi hamjawaandaa watumiaji wala miundo mbinu.

Mtumishi ataesimamishiwa mshahara wake alio utumikia mwezi mzima kutokana na majukumu yake kwa mujibu wa makataba wake wa kazi kwa kisa hajajiunga na PEPMIS anione PM kwa masaada wa kisheria.
Nimesikiliza hoja za watu humu ndani hasa watumishi nimegundua kwanini hii nchi mambo mengi hayaendi isee.

hawa watumishi wanakerekwetwa sana na viongozi wao wanaona km viongozi ndio wanafaidi maslahi makubwa wao wanaumizwa kwa salary ndogo manung'uniko ni mengii yamejikita kuwazodoa wakubwa wao.

Nikija kwenye hoja ya huo mfumo mm naona hakuna sababu za msingi za watumishi kushindwa kujiunga na huo mfumo maan ukileta hoja ya maswala ya network sijui wakati watumishi karibu wote wanamiliki simu za mkononi pia sehemu zinazosumbua network hazizidi asilimia 15 ktk 100 kwa Tanzania kwa sasa.
Kuhusu kujua mfumo na kuelewa shida ni watendaji wetu wenyewe.

Serikali na viongozi shikilieni hapohapo..!
 
Vipi kuhusu Mifumo mingine waliyo nayo haifanyi kazi?
Hawatumii simu za mkononi kuingia whatsapp?
Na kufanya matumizi mengine?
Ndio ujiulize tukienda kwenye maofisi yao watumishi muda mwingi wapo wanachart nani kawafundisha na kwanini washindwe mfumo wao wa kuwatathimini utagundua kuna kitu wanajilinda nacho hapo.
 
Namshangaa sanab Simbachawene amekuwa hapo tamisemi kwa vipindi mbali mbali kweli hajui mazingira ya watumishi wake wanayo fanyia kazi? Au ndio kulazimisha mambo ili wamdanganye Rais kwamba huo mfumo unafanya kazi vizuri
Muuzaji wa mfumo anataka kuithibitishia Serikali kuwa kafanya kazi nzuri kuwauzia huo mfumo.
Anataka kumaliziwa chake haraka.
Na Kuprisenti mafanikio ya mfumo.
 
70% ya vishikwambi vilikwisha kufa miezi miwili tangu wapewe.

Yale madudu ni mabovu hatari. Serikali ilipigwa aisee.
Ile zile ni uchafu tuu hazina hadhi kabisa walimu ni kama walitupiwa! Ingekuwa ni Apple ipad wasingepewa walimu
 
Walimu pamoja na kuwa na vishkwambi bado wanashindwa kujisajili kwenye huu mfumo?

Hila huu ni uonevu mkubwa tanzania tunashida ya matumizi ya hii mifumo na huu mfumo umekuwa ukiwasumbua sana watumishi sio haki kuwanyima mshahara eti kisa hawajajisajili
Unampa mwalimu kishikwambi ili hali alipo hata umeme hakuna, mtandao hakuna. Labda hamjatembea nchi hii kuna sehemu ukienda mitandao ya simu kati ya voda, airtell, tigo na halotel, unapatikana mmoja tena kwa mbaaaaaali. tena utumie simu kiswaswadu, haya masmart phone hayashiki network.
 
Ndio ujiulize tukienda kwenye maofisi yao watumishi muda mwingi wapo wanachart nani kawafundisha na kwanini washindwe mfumo wao wa kuwatathimini utagundua kuna kitu wanajilinda nacho hapo.
Utenda kazi wa watumishi ni mbovu hivyo wanaogia kupata maksi chache kwemye mfumo wamezoea OPRAS wanajipa maksi za mezani na wanajijazia sasa huu mfumo unamtaka kujaza kila siku au kila mwezi kazi alizofanya halafu mwaka wa fedha ukiisha inajicalculate yenyewe kuonyesha Mtumishi anavyofanya kazi au uzembe wake..
SAsa wana hofu sana
 
Back
Top Bottom