Serikali iache mzaha; kuruhusu watoto waliopewa mimba kurudi shule ni anguko la taifa la kesho

Lengo la adhabu ni kuonya ama kufundisha!

Katika kutoa funzo adhabu hio lazma iwe na hali flani ya kuumiza kinamna flani yani lazma imgharimu mtu ambaye ametenda hilo kosa na kumfanya ajutie uzembe wake.

Kama tutaruhusu watoto wakike warudi shule na vijana waliowatia mimba waachiwe waendelee kupeta mtaani! Sheria ifumuliwe sio mlete upendeleo wa kishamba.
 

Binti chini ya miaka 18 unaanzaje kumhukumu na kumuadhibu wakati tunakubaliana sio makosa yake?
 


Hapa Hatuzungumzii kufaulu au kufeli, kwani Nani kasema Mwanafunzi aliyepewa mimba hawezi kufaulu??

Hapa tunazungumzia habari za kosa na adhabu yake.

Hakuna binti anaweza akawa mdogo lakini akwa mkubwa kibaolojia, binti Yeyote mwenye uwezo wa kubeba mimba ni Mkubwa kiasili. Hayo ya kusema ni mdogo ni kulingana na mtazamo au maoni ya watu lakini kiasili ni Mkubwa.

Mtoto hawezi beba mimba Mkuu. Labda useme akili ndio yakitoto,
Lakini mbona Hilo hata wenye umri mkubwa wapo wenye akili hizo za kitoto?
 
Mkeo amevamiwa na majambazi nyumbani wakambaka na kumpa maambukizi, basi na wewe ni sawa kuja kumpa talaka kwa uzembe wake....
 


Ndio hapo sasa.

Hawawezi onea Vijana wakiume Kwa visingizio visivyo na maana.

Hata Vijana wakiambiwa wajieleze hawatakosa chakusema.

Ni mwanaume gani asiyejua kimbembe cha hamu ikipanda mwilini?

Kama ni adhabu watoe Kwa wote.
Wakishindwa wafute Kwa wote
 
Mkeo amevamiwa na majambazi nyumbani wakambaka na kumpa maambukizi, basi na wewe ni sawa kuja kumpa talaka kwa uzembe wake....


Ndio maana nimeandika kuna Exceptional chini Kabisa na nimeshasema kuwa Bahati nzuri no kuwa wanaopitia hayo ni wachache.

Kitoto unakikanya kila siku kinang'ang'ania maghetto ya wanaume alafu useme kimebakwa. Embu tuweni Sirius bhana.
 
Binti chini ya miaka 18 unaanzaje kumhukumu na kumuadhibu wakati tunakubaliana sio makosa yake?


Kuanzia miaka 15 mbona mtu anajitambua kabisa.

Labda wenye matatizo ya Akili ambao ni exceptional.

Wewe ulivyokuwa na miaka 15 ulikuwa haujitambui?

Anyway kujitambua kunatokana na mazingira mtu amekulia.

Kuna wengine mpaka miaka 30 hawajitambui kutokana na kutofunzwa vyema tangu wakiwa watoto.

Waulize waalimu wao ndio wanajua mtoto wa miaka 15 anafaa kuhukumiwa au laa.
 
Naomba kufahamu kiongozi! Kijana miaka 16 na Binti miaka 16 akapata mimba wote wakiwa shule. Kijana huwa anchukuliwa hatua gani?
 
Ndio maana nimeandika kuna Exceptional chini Kabisa na nimeshasema kuwa Bahati nzuri no kuwa wanaopitia hayo ni wachache.

Kitoto unakikanya kila siku kinang'ang'ania maghetto ya wanaume alafu useme kimebakwa. Embu tuweni Sirius bhana.

Katika hali hiyo sasa, tunapaswa kukukamata wewe mzazi na kukufunga maana umeshindwa kumlea mwanao kiasi cha kukushinda akiwa chini ya 18yrs....

akisha kuwa chini ya 18yrs tafsiri ya kisheria ni mtoto ambaye anahitaji uangalizi na ulinzi wa jamii...
 
Taifa ililishaanguka kabla ya kufika kesho. Ngoja watoto wakimbizane na hatima ya maisha yao.
Wazazi wanapaswa kuwalea watoto katika maadili mema, wanapaswa kujua madhara ya kupata mimba na sio kuwahukumu kwa kuwakosesha fursa ya kuendelea na masomo.
 
Malawi now wanafikiria uwekezaji wa BANGE.......kila mmoja apambanie ya kwake......nashauri wapunguze ile 30yrs.....wahasiwe kabisa....then apewe mtoto amtunze
 
hii pia ni njia nzuri....wazazi wawajibishe...wote wawili.......kuna adabu itajirekebisha kdg
 
We naye una mindset ya 20th century!! Kwamba eti aliyezaa hana maadili ila wasiozaa wana maadili? Kwani issue ni ngono au mimba? Kwamba wanao sex na condom hao wana maadili si ndio?

Anyway unaposema wasichanganywe, kwani watoto washule hawaishi mtaani? Hawaoni mabinti wengine wakizalia nyumbani kiasi kwamba waje kuharibiwa shuleni sio mtaani??

Ww ungeshauri wanawake wajengewe mabweni ili wawe wanasoma huko huko wanarudi likizo tu pengine ita control muingiliano na wahuni wa mtaani ila kudai kwamba kuwachanganya ndio sababu ya maadili kushuka ni mentality ya ajabu sana.
 
Ndio maana ya Adhabu,
Lengo la adhabu ni kukuonya na kumfundisha mtu.

Huyo binti na kijana kila mmoja atumikie adhabu yake ili iwe fundisho Kwa wengine.

Elimu pasipo na maadili haina maana yoyote.
Lete stats za kuonyesha hiyo adhabu imesaidia maadili kusimama
 
Hata Maghufuli hakuwazuia kupata elimu alikuwa anasema akipata mimba atolewe huko elimu akaendelee nayo kwenye kundi la wakubwa, maana elimu siyo lazima itolewe na mwalimu hata yeye anaweza akawa anawaelimisha wenzie jinsi ya kupata mtoto mwisho wa siku kila mhitimu anarudi nyumbani akiwa na ufaulu wa elimu na malezi ambayo siyo sahihi kabisa kwa jamii zetu, nami naunga la kuwakazia watambue ni kosa kuzaa ukiwa unasoma kwa kumtengenisha na aliokuwa nao.
 
Mabeberu wamesema sasa kama kweli mnaweza kujisimamia mambo yenu ya ndani ebu jaribuni na hilo tuone sasa kama huwezi kujisimamia kaaa utulie ili wakubwa waamue juu ya hatma yako
 
hili taifa lishaanguka siku nyingi mkuu
yaani tunaenda kwa matamko ya watu, akiamka anaamua tu anavyojisikia
Kwani Tz, ina kitu gani cha kipekee, kwani mbona nchi nyingine za kiafrika wameruhusu, na kielimu, kiuchumi wako juu zaidi yetu!!yaani hii nchi huwa tunajifanya kama ina upekee wa aina yake vile!??
 
Nashauri watoto wako wakipata mimba ndio wasirudi shule, ila watoto wa sisi wenzio wakipata mimba bado tunawapenda watimize ndoto zao, waendelee kuupewa nafasi nyingine ya kusoma. sioni shida yeyote mtoto aliyepata mimba kuendelea na shule, shida hiyo ipo kwenye vichwa vya watu wa aina yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…