Serikali iache mzaha; kuruhusu watoto waliopewa mimba kurudi shule ni anguko la taifa la kesho

andiko lako refu sana hongera kwa kuchukua muda wako kuandika hisia zako ambazo haziko kitaalamu.
Tuambie ni kwa vipi binti kuwa mjamzito/kuzaa kutampunguzia uwezo wake wa kuelewa darasani.
Unajua kuwa kuzuia watoto waliopata ujauzito ndio kunaongeza utoaji mimba na vifo,je kipi bora mtoto kurudi shule au atoe mimba na kusababisha vifo
unajua asilimia kubwa ya watoto wanaopewa ujauzito ni kutokana na unayanyasaji wa kingono ie kubakwa sasa kwanini aadhibiwe huyu aliyebakwa
je unajua kuwa kumzuia mtoto aliyepewa ujauzito kurudi shule unaongeza pengo katika usawa wa kijinsia ie angalia ratio kuna wanawake wangapi kwenye nafasi za kiuongozi
Hebu jaribu kutafakari namna bora ya mlinda mtoto wa like badala ya kumuadhibu
 
Mkuu upo sahihi , acha kuwajibu wapuuzi ambao wanatetea zinaa eti kwasababu za kipumbavu.

Kwenye mambo ya kipumbavu kama haya tutawajibu wote mnaotetea upuuzi bila kujali nafasi yako.
 
Mkuu ukishaolewa kulala uchi ni SHURTI...

Una hela gani wewe. Mabeberu walishawaoa, hamna say yeyootee.

Huna la kufanya. Mshakula hela zao.

Na mashoga wanaruhisiwa soon.

Subiri hapahapaaa..
 
Mojawapo ya madhara yanayotupata kwa kuongozwa na mwanamke, anafikiri huruma ni kuruhusu mambo ya hovyo kama hilo. Marehemu raisi Mkapa alianzisha vitu kama MEMKWA. Sasa kila msichana aliyevunja ungo atataka kujaribu kupata mimba ili ajisikilizie mabadiliko ya mwili. Ni kichocheo kwa marafiki kupata mimba
 
Ndio maana ya Adhabu

Lengo la adhabu ni kukuonya na kumfundisha mtu.

Huyo binti na kijana kila mmoja atumikie adhabu yake ili iwe fundisho Kwa wengine.

Elimu pasipo na maadili haina maana yoyote.
Umesisitiza sana kwamba Elimu pasipo na maadili haina maana yeyote, ninaomba ufafanuzi, maadili ni nini?
 
Dah Mkuu kwanza hamna anaefanya ngono akiwa hajui madhara yake labda ni kichaa tu,,,

watoto wanafundishwa toka shule ya msingi na wanajua madhara ya ngono kwa umri wao sema tu kizazi kishaoza hiki ata tukihangaika vipi amna kitu tatizo ni kumnyima haki mtot wa kiume hapo maana mwanaume ata kama alikua mtot wa miaka 17 au 16 atafungwa alafu wakike aludi tena shule
naona kuna madudu mengi hapo halafu kwa kizazi hiki cha nyoka wataigana sasa wataona kama wapo chuo kikuu akizaa mmja bas wengine wataiga sababu wanapewa room kuzidi kufanya uchafu
 
Tuma na salam
 
Mimi hili rai yangu binti aendelee na shule lakini apewe adhabu ya kutumikia jela miaka 5, jela ya watoto kisha akitoka aendelee na shule. Na kwa mwanaume miaka 30 ibaki palepale..
 
HAO WAPUUZI, MITOTO YAO ISHAPIGWA MIMBA HUKO NDO WANARUHUSU WENYE MIMBA WAENDELEE KUSOMA ILI WAWAPACHIKE MAKAZINI KAMA WAO WALIVOPACHIKWA.

WENGINE NI MAHAWARA ZAO. WAKAONA ISIWE TABU ANGALAU WAPATE KIJICERTIFICATE WAWAUNGANISHE KWENYE MICHONGO YA WATU WA MASTERS.
 
Mumbai kwa watoto wa kike ni one mistake, one goal. Serikali au jamii, haifaidiki chochote kwa kumnyima elimu binti huyu aliyepata mimba.

Ukimnyima elimu huyu mama, ndio umempeleka kwenye umaskini pamoja na mwanae. Wengi mara nyingi hukimbilia kwenye biashara ya ukahaba. Lakini akipewa second chance, hatakuwa tegemezi kwa mtu yoyote.

Hili tatizo huwa janga mara dufu kwenye familia maskini. Katika familia za waliojiweza, hili sio tatizo. Msichana atajifungua, mtoto atapelekwa kwa shangazi kulelewa, na binti atahamishwa mkoa mwingine ili amalize shule. Lakini mtoto wa maskini, mimba ndio mwisho wa ndoto zao za maisha.

Na yule kidume aliyetia mimba yupo wapi?
 

kama mtoto wa 12 anapelekewa ukuni hiyo sio kazi ya mletamada ni nyingi kaka na dada zao ndio mna matatizo.
 
Hii nchi kwa kubaniana hadi elimu duh
Dhumuni la elimu ni kutoa ujinga
Mtt akijifungua arud shule
 
na anaempa mimba mwanafunzi nae asemehewe au alipe faini au amtunze mtoto sio kumfunga na huyu unamuachia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…